Rais mstaafu wa Afrika Kusini na mwanaharakati mpambanaji wa ubaguzi, Nelson Mandela, 93, amefanyiwa upasuaji wa tumbo, tatizo ambalo limekuwa likimsumbuakwa muda mrefu na kulazimu kufanyiwa matibabu kwa njia ya upasuaji.
Msemaji wa rais alieleza kuwa Bwana Mandela ni mzima na amechangamka.
Rais huyo wa zamani aliacha kutokeza hadharani miaka minane iliyopita.
Msemaji wa Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini, Mac Maharaj, alitoa maelezo kuhusu Madiba, jina la jadi la Mandela:
"Tunachotaraji ni ushirikiano wa wananchi na vyombo vya habari, kwamba tuendeshe jambo hili sawasawa. Tutajaribu kukupeni taarifa. Sasa ninachoweza kusema ni kwamba, kwa sababu ya faragha yake na familia yake, hatutasema yuko hospitali gani na kadhalika. Rais Zuma ametuarifu kuwa Rais Mandela alipelekwa hospitali asubuhi. Kwa muda mrefu Madiba amekuwa akisumbuliwa na tumbo, na madaktari waliamua linahitaji kushughulikiwa na wataalamu. Tunamuombea afya, na kumhakikishia pendo na nia njema ya wananchi wote wa Afrika Kusini na watu katika sehemu mbali-mbali za dunia."
Keith Khoza, msemaji wa Chama cha African National Congress, aliyanukuu maneno ya msemaji wa ofisi ya Rais Zuma yanayowahakikishia wananchi na wanacchama wa chama hicho kuwa, "(Mandela) just had abdominal pains for some time now and the doctors decided a while ago that perhaps they should admit him, with a view to check those abdominal pains, so it wasn't an emergency admission," Khoza told reporters. "He's fine, he's in good health."
Mwaka 1994 baada ya uchaguzi mkuu, Mandela alichaguliwa kuwa Rais wa kwanza Mwafrika nchini Afrika Kusini.
Awali ya hapo, Mandela alifungwa na Serikali ya Makaburu kifungo cha jela miaka 30 kutokana na harakati za ukombozi na uhuru wa taifa hilo, na kupinga ubaguzi wa aina mbalimbali uliokuwa ukiwaathiri na kuwaua Waafrika Weusi. Alitumikia kifungo kwa miaka 27.
Mandela ni amewahi kutunukiwa tuzo ya Nobeli kwa juhudi zake hizo.
Source: http://www.wavuti.com
0 comments:
Post a Comment