Roberto Mancini ajilaumu kwa kutoiandaa timu dhidi ya Everton
Meneja wa Manchester City Roberto Mancini amesema anawajibika kwa kutoiandaa vyema timu yake baada ya kuteleza na kufungwa bao 1-0 na Everton.
Vinara hao wa Ligi Kuu ya England kwa sasa, bado wanaendelea kushikilia usukani wa ligi hiyo kwa tofauti ya mabao baada ya Darron Gibson kupachika bao hilo moja, wakati Manchester United waliichabanga Stoke katika uwanja wa Old Trafford.
"Huenda yalikuwa ni makosa yangu kwa sababu hatukujiandaa vizuri kwa mechi hii," Mancini aliiambia BBC.
"Nilifikiria kabla ya mchezo kwamba mambo yangekuwa rahisi, kumbe yakawa kinyume."
Mancini baadae alikiri alifanya makosa wakati wa kuiandaa timu.
"Wachezaji wangu walijituma sana uwanjani lakini nilifanya baadhi ya makosa siku tatu zilizopita kwa kuiandaa mechi hii," aliongeza.
Kiungo wa zamani wa Manchester United, Gibson alipachika bao hilo pekee kipindi cha pili na kuipa timu yake ya zamani nafasi nzuri ya kuisogelea Manchester City, wakati mabingwa hao wa Ligi ya England walipoilaza Stoke mabao 2-0 na kuziba pengo la pointi.
Mancini alikiri timu yake ilikuwa na kibarua kigumu dhidi ya timu ambayo imewahi kuifunga mara moja tu katika michezo 14 katika uwanja wa Goodison Park.
"Everton wakiwa kwao ni wazuru sana," aliongeza. "Kila wakati tunapocheza nao wanacheza vizuri sana.
CHANZO; BBC SWAHILI
CHANZO; BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment