SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, February 6, 2012

Airtel yagawa vitavu Sekondari za Manyara

Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Yaeda Ampa Mary Genda na wanafunzi wa shule hiyo wakipokea vitabu toka kwa Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde vilivyotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa shule za sekondari nne za mkoa wa Manyara ambazo ni Yaeda Ampa, Yaeda Chii , Naberera na Merelani B.w Mkapa chini ya mpango wake wa shule yetu halfa iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii.
Afisa Mahusiano wa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel ,Jane Matinde akikabidhi vitabu kwa Afisa Elimu sekondari wa wilaya ya Mbulu Mikaeli Hadu ,kwa niaba ya shule nne za sekondari zilizokabidhiwa vitabu hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni moja kwa kila shuke,shule hizo ni Yaeda Ampa, Yaeda Chii , Naberera na Merelani B.w Mkapa,Mkoani Manyara (katikati )ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw.Harry Sinjela.
Wanafunzi , walimu ,wafanyakazi wa Airtel na viongozi mbalimbali wa halmashauri ya wilaya ya mbulu mkoani Manyara wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Airtel kukabithi vitabu kwa shule 4 za sekondari zilizopo mkoani hapa, kila shule imepata vitabu vya thamani ya shilling milioni moja. 
Waliokaa kutoka kushoto ni Afisa wa uhusiano wa Airtel Jane Matinde Akifatiwa na kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya mbulu Bwana Harry Sinjela, Afisa Elimu sekondari wa wilaya ya Mbulu Mikaeli Hadu na diwani wa kata ya Yaeda Ampa Bw Marcel Malley.

0 comments:

Post a Comment