SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, February 26, 2012

MAKAMU WA RAIS DK GHARIB BILAL AKABIDHI MIZINGA YA NYUKI KWA WAFUGAJI WA KIJIJI CHASIMAMBWE MBEYA VIJIJINI, NA KUKAGUA UJENZI WA BWAWA LA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi mzinga wa Nyuki mmoja kati ya wafugaji , Salome Zumba wa Kikundi cha kinamama na Vijana cha kijiji cha Ijewe, wakati alipokuwa katika ziara yake ya mkoa wa Mbeya jana Februari 25, 2012.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo na kutazama mmoja kati ya mizinga ya Nyuki kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, kuhusu utengenezaji wa Mizinga hiyo ya kisasa na gharama nafuu, wakati alipofika kutembelea kituo cha kuahiria mifugo cha Simambwe, kilichopo Wilaya ya Mbeya Vijijini, akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Mbeya jana Februari 25, 2012. Kulia ni Mke wa Makamu wa Rais, Mama Asha Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mama Asha Bilal, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro na baadhi ya viongozi wa mkoa huo, wakitoka kukagua ujenzi wa mradi wa Bwawa la umwagiliaji  lililopo kijiji cha Rwayo, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Mbeya jana Februari 25, 2012
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akinyoosha mkono kuwasalimia wananchi wa Kijiji cha Simambwe, wakati alipowasili kijijini hapo kutembelea Kituo cha Kuahiria Mifugo na kukabidhi mizinga ya nyuki kwa badhi ya wafugaji, akiwa katika ziara yake mkoa wa Mbeya jana Februari 25, 2012.Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu Wa Rais

0 comments:

Post a Comment