Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akitoa ufafanuzi kwa wabunge leo mjini Dodoma baada ya kuzuia hoja ya mgomo wa madaktari bingwa kujadiliwa Bungeni iliyoibuliwa na mbunge wa Mbozi Magharibi Godfrey Zambi na kufafanua kuwa suala hilo tayari limeshaanza kufanyiwa kazi na Bunge ikiwemo kuiagiza kamati ya huduma za jamii kulifuatilia suala hilo kwa kukutana na pande zinazohusika na kupeleka majibu bungeni.
Naibu waziri , Ofisi ya Waziri mkuu Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Aggrey Mwanri akitoa ufafanuzi wa maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wabunge kwenye ofisi ya waziri mkuu yakiwemo masuala ya migogoro ya mipaka ya viwanja kwenye Halmashauri na manispaa ya Kigoma –Ujiji pamoja na suala la kuongeza madaktari bingwa na manesi katika manispaa ya Dodoma kufuatia ongezeko la watu na vyuo mbalimbali leo mjini Dodoma.
Mawaziri na wabunge wakifuatilia kwa makini mkutano wa sita wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma. Kutoka kushoto ni Makamu wa pili wa Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzbar Balozi Seif Ali Idd ,mbunge wa Songea Jenista Mhagama na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samueli Sitta (kulia), wengine waliokaa nyuma ni Waziri ,Ofisi ya Waziri mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu, Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi na Naibu waziri wa Kazi na Ajira Makongoro Mahanga.
Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC Taifa) wakitekeleza majukumu yao ndani ya ukumbi wa Bunge kwa kuhakikisha kuwa watanzania wanayapata matangazo ya Bunge kupitia TBC Taifa moja kwa moja kutoka mjini Dodoma.
Raia wa kigeni ambao wako nchini wakiwa ndani ya Bunge wakifuatilia kipindi cha Maswali na majibu cha mkutano wa sita wa Bunge kufuatia mwaliko wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda.
Picha na Aron Msigwa –MAELEZO
Picha na Aron Msigwa –MAELEZO
0 comments:
Post a Comment