Mwanafunzi wa shule ya Msingi Luilo Ludewa akiwa amebeba majembe baada ya naibu waziri wa Tamisemi Aggrey Mwanri kuagiza warudi madarasani Jana asubuhi.
Mwalimu wa shule ya msingi Luilo kata ya Lifua wilaya ya Ludewa mwalimu Mgaya akipita katika eneo ambalo wanafunzi walikuwa wakilima na kuacha majembe na kukimbia kujificha
Naibu waziri wa Tamisemi akiwahoji walimu na wanafunzi waliokuwa wakiwatumikisha watoto wa shule mida ya masomo jana
Wanafunzi wa shule ya msingi Luilo kata ya Lifua wilaya ya Ludewa wakilima shamba la shule mida ya masomo majira ya saa 3 asubuhi leo baada ya kufanya ziara ya ghafla eneo hilo
Wanafunzi wa shule ya Msingi Luilo Ludewa wakiwa wamejificha katika kichaka pamoja na walimu wao kumkwepa naibu waziri wa Tamisemi Aggrey Mwanri jana
Msafara wa naibu waziri wa tamisemi Aggrey Mwanri ukipita eneo ambalo wanafunzi walikuwa wakilima.Picha na Mdau Francis Godwin
=======
BAADA ya naibu waziri ofisi ya waziri mkuu Tamisemi Aggrey Mwanri kuukataa mradi wa umwagiliaji katika kata ya Lifua wilayani Ludewa uliojengwa kwa zaidi ya shilingi milinio 500 bila kufanya kazi kutoka na kubomoka kabla ya muda na ule wa ukarabati wa nyumba ya mganga kata ya Lupanga iliyokarabatiwa kwa kiasi cha shilingi milioni 7 ,mbunge wa jimbo la Ludewa acharuka mbele ya naibu waziri amkataa mhandisi wa maji na mhadisi wa ujenzi ataka naibu waziri kuwapeleka jimboni Kwake ama jimbo la waziri mkuu Mizengo Pinda.
Mbunge Filikunjombe aliwakataa wahandisi hao wawili Christopher Nyandiga wa maji na mhandisi wa ujenzi Rashid Mtamila leo katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa wakati wa majumuisho ya ziara ya siku mbili ya naibu waziri huyo katika kutembelea miradi ya kimaendeleo katika wilaya hiyo ya Ludewa.
Mbunge Filikunjombe alimweleza naibu waziri huyo kuwa wilaya ya Ludewa imegeuzwa kuwa ni shamba la bibi kwa baadhi ya viongozi wasio waadilifu ambao wamekuwa wakitumia vibaya nafasi zao kwa kuhujumu miradi ya kimaendeleo inayoibuliwa katika wilaya hiyo.
Alisema kuwa kila wakati amekuwa akiwaonya watumishi wa wilaya ya Ludewa kufanya kazi yao kwa uadilifu ila baadhi yao wameshindwa kabisa kuonyesha uaminifu katika utendaji wa kazi yao.
“Viongozi wenzangu na madiwani wangu wapo walionifuata kutaka niwatetee kwa uozo huu ila nasema heri kulaumiwa kwa kusimamia ukweli na kupinga ufisadi unaofanyika katika wilaya ya Ludewa ila nipo tayari kuendelea kufanya kazi na viongozi waadilifu “
Alisema kuwa wahandisi hao wameendelea kuwa kikwazo kikubwa katika wilaya ya Ludewa na kuwa miradi mbali mbali inayosimamiwa katika wilaya hiyo imekuwa ni mibovu na haina sifa japo imetumia fedha nyingi zaidi .
Mapema asubuhi naibu waziri huyo alifanya ziara ya ghafla ambayo haikuwepo katika ratiba katika banio la mradi wa umwagiliaji wa Lifua ambalo umejengwa na kampuni ya Summer Communication kwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 357 toka mwaka 2009/2010 bila kufanya kazi .Kitoa taarifa ya mradi huo mbele ya naibu waziri Mhandisi wa maji wilaya ya Ludewa Nyandiga alisema kuwa awamu ya kwanza ilitumia kiasi cha shilingi milioni 357,262,990 na mradi huo kukabidhiwa kwa Halmashauri toka mwaka 2010 japo hautumiki kutokana na kuvujisha maji.
Wakati awamu ya pili mradi ulijengwa na kampuni ya Tan Direct Co.Ltd ya Dar es salaam kwa gharama ya shilingi milioni 227,613,136.15 kwa kazi ya kujenga mfereji wenye urefu wa mita 1725,usakafiaji wa eneo la kuingia na kutoka kwenye daraja hilo ,ujenzi wa vigawa maji vinne na ujenzi wa vianguko vya maji vinne na ujenzi wa kivusha maji kimoja na kuwa hadi sasa mkandarasi huyo amelipwa asilimia 64.9 ya fedha zote na kazi hiyo imefanyika kwa asilimia 73.2.
Akimhoji mkandarasi huyo naibu waziri huyo Mwanri alimtaka kueleza sababu ya kulipa mamilioni ya fedha katika mradi huo bila kufanya kazi na hauna maji katika kipindi hiki cha masika ,mhandisi huyo alikana kuwa yeye si msanifu wa mradi huo hivyo hawezi kujibia swali hilo.
Akitoa majumuisho yake na maombi ya mbunge Filikunjombe ya kutaka wahandisi hao kuondolewa katika wilaya hiyo ya Ludewa naibu waziri huyo alisema suala hilo linawezekana kwani pia kwa upande wake hajapendezewa na ufisadi mkubwa uliofanyika katika miradi hiyo.

0 comments:
Post a Comment