TAARIFA KWA UMMA
Kikao cha Baraza la Chuo kilifanyika tarehe 10/01/2012 na kujadili hali ya Chuo kwa ujumla na
Serikali ya DARUSO iliwakilishwa. Hivyo basi Serikali ya Wanafunzi inapenda kuutaarifu umma yafuatayo:
1.) Serikali ya wanafunzi (DARUSO) haijafutwa, ipo na inaendelea kufanya kazi. Kuhusu taarifa zilizoenea katika vyombo vya habari kuwa DARUSO imefutwa ni uzushi na tunafanya taratibu za kuwachukulia hatua watu na vyombo vyote vya habari Vilivyoeneza uvumi huo.
2.) Serikali ya wanafunzi inaendeleza juhudi za majadiliano kuhusu hatma ya wanafunzi ambao wamefukuzwa na kusimamishwa masomo.
3.) Aidha, tunaomba wale wanafunzi wachache ambao wanaendeleza mgomo warudi madarasani na kuendelea na masomo kama kawaida. Pia serikali ya wanafunzi inasisitiza kuwa mgomo unaoendelea sio halali kwani taratibu zote za kisheria na kanuni hazikufuatwa. Kwahivyo tunawaomba wanafunzi wasitishe maandamano hayo ili kuruhusu jitihada zinazochukuliwa na viongozi wao kuzaa matunda ndani ya siku chache kuanzia leo hii tarehe 11/01/2012.
Imetolewa na:
Hassan Mustapha,
Waziri Mkuu,
UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
DAR ES SALAAM UNIVERSITY STUDENTS
ORGANISATION (DARUSO)
P. O. BOX 35080-DAR ES SALAAM-TANZANIA
www.daruso.udsm.ac.tz
0 comments:
Post a Comment