ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A LOWEST COST AND ALSO SEND TO US NEWS, EVENTS FOR MORE INFORMATION CONTACT US TELEPHONE: +919160901191 E-mail: ally.shaaban@yahoo.com | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU NA PIA TUTUMIE HABARI, MATUKIO KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI KWA SIMU: +919160901191 Barua Pepe: ally.shaaban@yahoo.com | DO YOU NEED TO CREATE BLOG CONTACT US HERE | UNAHITAJI KUFUNGUA BLOG WASILIANA NASI HAPA

Saturday, April 30, 2011

HAPPY BIRTHDAY PRINCESS ASIA MAHMOUD ZUBEIRY

Leo ni Tarehe ya kuzaliwa kwa mtoto PRINCESS ASIA MAHMOUD ZUBEIRY wa DAR-ESSALAAM-TANZANIA, ambaye leo atimiza miaka minne(4).
Mama yake mzazi Bi Dina Ismail anamtakia kila la heri, makuzi na afya njema katika maisha yake.
Blogu hii inaunganana na Familia yake, ndugu jamaa na marafiki wote kumtakia siku njema iliyo na furaha, amani na upendo. M/Mungu amjalie afya njema,maisha mrefu,hekima na busara katika siku za maisha yake.

HAPPY BIRTHDAY PRINCESS ASIA MAHMOUD ZUBEIRY

NAWATAKIA KILA LA HERI WIKIENDI NJEMA

VODACOM TANZANIA YAZINDUA RASMI SHINDANO LA UREMBO LA VODACOM MISS TANZANIA KWA MWAKA 2011

Mkuu wa Udhamini wa Kampuni ya simu za mkononi Vodacom Tanzania, Bw. George Rwehumbiza akizungumza katika hafla fupi ya kuzindua rasmi shindano la Urembo la Vodacom Tanzania kwa mwaka 2011 wakiendelea kuwa wadhamini wakuu wa shindano hilo. Bw. Rwehumbiza alisema kwamba shindano la mwaka huu lina mvuto wa aina yake kwani warembo thelathini watakaoingia fainali hawataweka kambi hotelini kama ilivyozoeleka na watakaa kwenye nyumba maalum itakayojulikana kama nyumba ya Vodacom.
Walioketi kutoka kushoto ni Mratibu wa Majaji wa kamati ya Miss Tanzania Dr. Ramesh Shah, Mkurugenzi Mtendaji wa Kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga, Mkuu wa Udhamini Vodacom Tanzania George Rwehumbiza, pamoja na Mkuu wa Itifaki ya Kamati ya Miss Tanzania Albert Makoye katika picha ya kumbukumbu na warembo mara baada ya uzinduzi.
Miss Tanzania 2007 Richa Adhia akiwa na mume wake mtarajiwa Hridhaan Dhillon.
Meneja Udhamini na Promotion wa Vodacom Bi. Rukia Mtingwa akimsikiliza kwa umakini Brother Ben Kisaka wa Jambo leo wakati wa kubadilishana mawazo katika hafla hiyo. Wengine ni Mkurugenzi wa T.H.T Ruge Mutahaba na Mkurugenzi Mtendaji wa Gazeti la Jambo leo na Mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto.
Aba Billdard kutoka Vodacom akiwa na mdau katika pozi.
Mbunifu wa Mavazi Ally Rehmtullah akiwa na Warembo waliowahi kutwaa taji la Miss Tanzania.
Wadau wakila wakinywa na kubadilishana mawazo katika hafla hiyo Linkiliyofanyika katika Hotel ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es Salaam.
Na Mo Blog.

WAFANYAKAZI IDARA YA HABARI (MAELEZO) WAMUAGA RASMI MKURUGENZI CLEMENT MSHANA

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Clement Mshana (kushoto) akikabidhiwa zawadi iliyoandaliwa na wafanyakazi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Afisa Habari Mwandamizi Bi. Anna Itenda (kulia)wakati wa hafla fupi ya kumuaga rasmi jijini Dar es salaam jana, Bw. Clement Mshana ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete kuwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
Na Michuzi.

WHO Watua Samunge

Wanasayansi wa ndani wathibitisha uwezo wake.
Mussa Juma, Samunge
Wataalamu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii pamoja na taasisi mbalimbali za afya nchini, jana walifika Samunge kuanza mchakato wa kutafiti dawa inayotolewa na Mchungaji, Ambilikile Mwasapila kama inatibu magonjwa sugu au la.Wataalamu hao walifika Samunge majira ya saa sita mchana na kusababisha kusitishwa kwa muda utoaji wa tiba ili kuwapa nafasi ya kufanya mahojiano na Mchungaji Mwasapila, kuchukua sampuli za dawa na mti ya mugariga. Baada ya mahiojiano, nao pia walipata kikombe cha tiba.
Wataalamu hao ni pamoja na Profesa Charles Wambebe wa WHO Marekani, Dk Budeba Sylvester wa Wizara ya Afya na Dk Georges Shemdowe kutoka Tume ya Sayansi na Teknolojia.Ujumbe wa huo pia ulimjumuisha, Mkemia kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Hamis Malebo.
Profesa Wambebe ambaye ni raia wa Nigeria na mtaalamu bingwa mwenye uzoefu na masuala ya tiba za asili, alisema amefika Samunge kutokana na maombi ya Serikali ya Tanzania iliyoomba msaada wa WHO, kufanya uchunguzi wa dawa ya Mchungaji Mwasapila.
''Tumekuja hapa Samunge, kufuatilia tiba hii jinsi inavyotolewa na WHO kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania itaendesha utafiti kwa kuhusisha watu waliotumia dawa, Mchungaji Mwasapila na wadau wengine ili kuona inaponyesha kiasi gani," alisema Profesa Wambebe.
Alisema wanatarajia kuwa ndani ya miezi 12 watakuwa wametoa majibu juu ya ubora wa dawa hiyo na katika kipindi cha miezi mitatu ijayo watatoa maendeleo ya utafiti ambao utakuwa unafanywa.
Alisema baada ya kukamilisha utafiti, Serikali ya Tanzania ndiyo itakayoachiwa jukumu la kutangaza dawa hiyo kama inatibu kiasi gani na kama itahitaji kuboreshwa ili iwe katika mazingira ya kisasa ni nini kifanyike.
Wagonjwa wa kisukari kuanza
Dk Sylvester alisema uchunguzi huo utaanzia kwa wagonjwa wa kisukari hasa kutokana na vipimo vyao kuwa rahisi na kufuatilia hali zao pia itakuwa ni rahisi tofauti na magonjwa mengine.
Alisema wizara ya afya inakusudia kupeleka Samunge, maabara kubwa ya kisasa ambayo wagonjwa watapimwa kabla ya kunywa dawa na baada ya kunywa watafuatiliwa kitaalamu hadi hapo itakapothibitika ubora wa dawa.
"Tunaomba wananchi wasubiri watafiti kufanya kazi kwani tayari taarifa ilitolewa kuwa dawa hii haina madhara kwa binadamu na kazi inayofuatia sasa ni kutazama ubora wake katika kutibu maradhi mbalimbali," alisema.
Babu atoa shukrani
Katika hatua nyingine, Mchungaji Mwasapila jana alitoa shukrani kwa serikali kuanzia ngazi ya Kijiji hadi wilaya kutokana ushirikiano waliompa katika msiba wa mtoto wake, Jackson (43) ambaye alifariki wilayani Babati baada ya kuugua malaria.
"Napenda kushukuru Serikali Wilaya ya Ngorongoro na Babati kwa msaada mkubwa ambao wamenipa katika msiba na kuniwezesha kufika kwa wakati na kurejea hapa, pia nawashukuru wananchi wote kwa ushirikiano walionipa," alisema Mwasapila.
Habari zaidi: Bofya Hapa

Friday, April 29, 2011

Mwanamfalme William Hatimaye Apata Mke

Mwana mfalme wa Uingereza, Prince William na Kate Middleton wamefunga ndoa katika kanisa la Westminster Abbey jijini London.
Takriban wageni 1,900 walishuhudia tukio hilo ndani ya kanisa, na mamilioni wakifuatilia majumbani mwao kwa njia ya televisheni.
Mwana mfalme William akifungishwa ndoa na Aksofu Rowan William katika kanisa la Westminster Abbey jijini London.
Maharusi hao walishangiliwa na maelfu ya watu waliojipanga barabarani kuelekea kasri ya Buckingham Palace ambako Malkia amewaandalia karamu wageni 650.
Wana ndoa hao wapya walitumia gari liliovutwa na farasi la muundo wa mwaka 1902 ambalo lilitumiwa na wazazi wake Prince William wakati wa ndoa yao mwaka 1981.
Maharusi hao baadaye walijitokeza kwenye roshani ya kasri ya Buckingham na kuwasalimu maelfu ya watu waliokwenda kuwasherehekea.
Baada ya kulishana viapo vya ndoa Askofu mkuu wa Canterbury, Rowan Williams, aliwanadi rasmi kuwa "mume na mke".
Kuanzia sasa maharusi hawa watajulikana rasmi kama Duke na Duchess wa Cambridge.
Kate akiwapunga mkono kwa furaha.
Kate ndani ya shela akiwa na mpambe wake.
William na Kate.
William na mkewe Kate wakiimba.
Baba wa Bwana harusi Prince Charles.
David Beckam na Mkewe Victoria.

SERIKALI KUANZA KUWATUMIA WAKANDARASI WAZALENDO KATIKA UJENZI WA BARABARA

Naibu Waziri wa Ujenzi Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza kwenye kikao na watendaji wa mkoa wa Singida.
Na.Nathaniel Limu, Singida.
Naibu Waziri wa Ujenzi Dk. Harrison Mwakyembe (Mb) amesema serikali inaandaa mkakati wa kupunguza gharama kubwa za ujenzi wa barabara zinazotozwa hivi sasa na makandarasi kutoka nje ya nchi.
Amesema kuendelea kulipa gharama hizo kubwa pamoja na kutekeleza masharti yanayotolewa na makandarasi hao hakutafanikisha lengo la serikali la kuwa na barabara nyingi za lami nchini.
Dk. Mwakyembe amesema hayo muda mfupi baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa ujenzi na uboreshaji wa barabara mkoani Singida iliyotolewa na meneja wa TANROADS mkoa Mhandisi Yustaki Kangole.
Akifafanua amesema makandarasi hao kutoka nje ya nchi wamepandisha mno gharama ya ujenzi wa barabara za lami, kutoka shilingi milioni 350 kwa kilomita moja mwaka 2005/2006 hadi shilingi bilioni 1.5.
Aidha Naibu Waziri huyo amesema sasa msisitizo mkubwa utaelekezwa katika kuwapatia kazi ya ujenzi makandarasi wazalendo ambao pamoja na mambo mengine wana uchunLinkgu na nchi yao.
Katika hatua nyingine Dk. Mwakyembe amesema pamoja na kushughulikia suala la kushusha gharama za ujenzi wa barabara, pia watachunguza na kufanya mabadiliko makubwa katika mikataba ambayo mingi, amedai haiionei uchungu nchi hii.
Wakati huo huo amewataka wafanyakazi waliochini ya wizara ya ujenzi kurejesha uadilifu na weledi ili kazi zinazofanywa na kusimamiwa ziwe bora kwa mujibu wa mikataba husika na ziweze kudumu kwa muda mrefu.
Na Mo Blog.

Babu Arejea Samunge, Tiba Kuanza Tena

Ambilikile Mwasapila(Babu)
Mussa Juma, Samunge
Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapila, maarufu kwa jina la 'Babu,' amerejea Samunge jana na leo anatarajiwa kuendelea kutoa tiba kwa wagonjwa waliokuwa wakimsubiri kwa siku tatu mfululizo.
Mchungaji Mwasapila aliondoka Jumanne jioni na jana alirejea kutoka wilayani Babati, mkoani Manyara alikohudhuria mazishi ya mtoto wake Jackson (43), akiwa anaongozwa na maofisa usalama na polisi.
Mchungaji Mwasapila, aliondoka kijijini Samunge saa 12:20 jioni katika gari la Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro ambalo lilibeba pia maofisa hao wa usalama, polisi na wasaidizi wake. Awali, kabla ya kuondoka Samunge, watu mbalimbali walikuwa wamejitolea kumsafirisha mchungaji huyo, lakini walizuiwa kutokana na sababu za kiusalama.
Mamia ya wananchi kutoka nchi jirani za Kenya, Uganda na Burundi, waliopo hapa Samunge, walimpokea Mchungaji Mwasapila kwa furaha kubwa wakitarajia leo kupata kikombe na kuondoka. Raia hao wa nchi jirani na Watanzania kutoka mikoa mbalimbali, wamelazimika kukaa siku mbili Samunge kumsubiri mchungaji Mwasapila arejee na kuendelea na tiba.
Akizungumza na gazeti hili jana, Msaidizi wa mchungaji Mwasapila, Fredrick Nisajile alisema walimaliza mazishi Babati juzi salama na jana walirejea Samunge wakiwa salama. "Kesho (leo) tunaendelea na tiba."
"Kesho (leo) tutatoa huduma ili kuwaondoa hawa wananchi tuliowaacha hapa Samunge,"alisema Nisajile.
Waliotibiwa kwa babu waomba tiba kuboreshwa
Baadhi ya wagonjwa wa magonjwa na Kisukari, Pumu na Saratani ambao wametumia kikombe cha Mchungaji Mwasapila, wameomba tiba hiyo kuboreshwa kitaalamu ili iweze kuwa na mafanikio zaidi.
Wakizungumza na gazeti hili, baadhi yao walisema walipotumia dawa hiyo walihisi kupona kabisa lakini baada ya muda, wakaanza kuona tena dalili za ugonjwa huo ingawa nguvu yake imepungua.
John Timoth, mkazi wa Loliondo, aliyekuwa anasumbuliwa na kisukari, alisema alikunywa kikombe hicho mwezi Februari mwaka huu na mwezi huo wote hadi Machi, sukari yake ilikwisha lakini, sasa ameanza kuona tena dalili za ugonjwa huo.
"Sasa sijui kama nilikiuka masharti ila juzi sukari ilipanda japo sio sana. Binafsi naamini dawa inaponya ila inadumu kwa muda gani mwilini, ndio nadhani uchunguzi unahitajika,"alisema Timoth.
Anastazia Maziku, ambaye mtoto wake, Isaya Maziku alikuwa anasumbuliwa na Pumu alisema baada ya kumfikisha Samunge na kunywa kikombe, alipona kabisa na kurejea hali ya kawaida, lakini sasa anaona kidogo hali inataka kurejea.
"Mwanangu karibu mwezi amekuwa vizuri tu. Juzi alipata shida ya kifua ila sio sana,"alisema Maziku.
Wagonjwa hao, ambao tayari wamepata tiba walishauri watafiti wa afya kushirikiana na mchungaji Mwasapila kuboresha tiba hiyo ili iwe ya kitaalamu zaidi.
Amir Mshana, alisema kuna wagonjwa ambao wamepona kabisa baada ya kutumia tiba lakini wengine wanaendelea kuumwa japo sio kama ilivyokuwa kabla ya kupata kikombe.
"Dawa nyingi za hospitali ni za asili ya mizizi, majani na vinginevyo, hivyo dawa hii inaonyesha inaponyesha lakini kuna baadhi wanapona moja kwa moja na wengine hali zinajirudia hivyo tafiti ni muhimu hapa" alisema Mshana.
John Ezekiel, mkazi wa Wasso, Loliondo, alisema tiba hiyo kama ikiboreshwa kitaalamu inaweza kutolewa katika hospitali na maeneo mengine kwa wagonjwa ambao ugonjwa unatishia kurejea.
Ezekiel alisema inavyoonekana mti wa Mugariga unaotumiwa na mchungaji Mwasapila, unatambuliwa na watafiti kuwa ni tiba, hivyo kama kutakuwa na maafikiano baina ya wataalamu na mchungaji huyo wanaweza kuboresha tiba hiyo.
"Hii inaonekana ni tiba na kuna mambo ya imani hapa, ila kama inawezekana ikiboreshwa iwekwe hata kwenye chupa au vidonge inaweza kuwafikia wagonjwa wengi zaidi na kutibu,"alisema Ezekiel.
Ezekiel pia alishauri kama inawezekana, wagonjwa wapewe fursa ya kurudia zaidi ya mara moja kunywa kikombe cha dawa ili waweze kupona kabisa. Hata hivyo, mchungaji Mwasapila, amekuwa akieleza kuwa mti huo unaotumika kama tiba pekee hauwezi kuponya bali nguvu za Mungu ndizo zinatumika sana.
"Wagonjwa wa kisukari baada ya kunywa kikombe anaweza kuendelea kula vitu vya kawaida bila tatizo," anasema mchungaji Mwasapila. Mamia ya watu bado wanafurika Samunge kupata tiba hiyo ya kikombe ambayo mgonjwa anakunywa kikombe kimoja pekee na haitakiwi kunywa zaidi ya mara moja.

Chanzo:mwananchi

Rais wa Shirika La Under The Same Sun Akiongea Na Watu Wenye Ulemavu Wa Ngozi Jana

Rais wa Shirika la Kusaidia watu wenye ulemavu wa ngozi linalofahamika kwa jina la UNDER THE SAME SUN,Peter Ash akizungumza jioni ya jana na baadhi ya watu wenye ulemavu wa ngozi pamoja na wanahabari huku Mkurugenzi wa Shirika hilo hapa nchini,Vicky Ntetema akimsaidia kutafsiri kwa kiswahili ili kuwaelewesha wale wasiojua lugha la kiingereza.hii ni katika hafla ya mkutano na watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Nyumbani Hotel,jijini Mwanza.Mkuu wa Wilaya ya Misungungwi,Mh. Mariam Lugairwa akizungumza katika mkutano huo jioni ya jana,ambapo aliwataka watu kujituma katika kufanya kazi ili kufanikiwa katika maisha na si kuweka dhana potofu ya kusema kwamba ili mtu afanikiwe kimaisha basi li lazima apate viungo vya albino.hii ni jioni ya leo katika hafla iliyoandaliwa na shirika la UNDER THE SAME SUN katika hoteli ya Nyumbani,jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye Ulemavu wa Ngozi Mkoani Mwanza,Alfred Kapole akizungumza wakati akifungua mkutano huo jioni ya leo.
Maafisa wa Shirika la UNDER THE SAME SUN kutoka jijini Dar wakibandika baadi ya picha ukumbini hapo.
Watoto wenye ulemavu wa ngozi ambao walihudhulia hafla mkutano kati ya Shirika la UNDER THE SAME SUN na watu wenye ulemavu wa ngozi.
Mwanalibeneke wa Libeneke la G. SENGO,Albert Sengo akiwa bize kuandika yaliyokuwa yakijiri ndani ya mkutano huo.
Na matukio michuzi

Watch A Live Stream Of The Royal Wedding!







Thursday, April 28, 2011

BARCELONA WINS 2-0 AT REAL MADRID IN A FIERY CHAMPIONS LEAGUE SEMI-FINAL FIRST LEG TIE

Lionel Messi.
Barcelona talisman Lionel Messi scored two late goals to put his side in control of their bad-tempered Champions League semi-final against Real Madrid.
The goals came after Real’s Pepe was dismissed in the 61st minute and boss Jose Mourinho was sent to the stands soon after for his protestations.
That seemed to turn the tide in Barca’s favour and they went ahead when Messi turned in Ibrahim Afellay’s cross.
Messi then added a fabulous second when he ran 30 yards before slotting in.
It was a glorious way to score his 11th goal in 11 Champions League games and by doing so made his side firm favourites to go through from the second leg at Barcelona’s Nou Camp on 3 May.
The final against either Manchester United or Schalke 04 will be played at Wembley on 28 May.

HAPPY BIRTHDAY TO YOU ALL!!

MIRAJI KIKWETE
CHIDI BENZ
PIPI

BUNGE UGANDA LAPITISHA BAJETI YA MATUMIZI YA ZAIDI YA SH. TRILLION MOJA

Bunge la Uganda.
Bunge nchini Uganda limepitisha matumizi ya ziada ya shilingi trilioni 1.7 kwa ajili ya kununua ndege (Fighter Jets) na shilingi bilioni 2.8 kwa ajili ya shere za kuapishwa kwa rais, pamoja na upinzani mkali liliokumbana nao kutoka kwa wabunge wa upinzani.
Wakijadili ripoti ya kamati ya Bajeti kuhusu matumizi ya ziada, wabunge kadhaa wa upinzani wamepinga matumizi hayo na kuapa kutohusika katika kupitisha ripoti hiyo.
Waziri kivuli wa kambi ya upinzani Oduman Okello amejaribu kulishawishi bunge hilo kupunguza bajeti hiyo kutoka shilingi bilioni 2.8 hadi shilingi bilioni 1.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, serikali ya Uganda inataka kuridhiwa kwa matumizi ya shilingi bilioni 2.8, bajeti ya ziada ya maendeleo ya shilingi trilioni 1.468 na ziada ya mapitio kwa mujibu wa sheria ya shilingi bilioni 56, inayofanya jumla ya bajeti ya ziada kufikia shilingi trilioni 1.54.
Na.Mo Blog.

Babu Aenda Msibani Chini Ya Ulinzi

Mchungaji Ambilikile Mwasapila (alishika koti),akisubili kupanda gari ili aondoka katika kijiji cha Samunge, mkoani Arusha juzi, kwenda Babati kuhudhuria mazishi ya mtoto wake,Jackson Mwasapila aliyefariki katika Hospitali ya wilaya ya Babati. Picha na Mussa Juma
Mussa Juma, Samunge
Mchungaji Ambilikile Mwasapila anayetoa tiba ya magonjwa sugu huko Samunge Loliondo, juzi jioni aliondoka hapa kwenda Babati, Manyara kuhudhuria mazishi ya mtoto wake huku safari yake hiyo ikiratibiwa na Serikali na akipewa ulinzi mkali wa maofisa usalama na polisi.
Aliondoka Samunge saa 12:20 jioni na gari la Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro akiwa na maofisa hao wa usalama, polisi na wasaidizi wake.
Kabla ya kuondoka Samunge, watu mbalimbali walikuwa wamejitolea kumpatia usafiri mchungaji huyo lakini walizuiwa kutokana na sababu za kiusalama.
"Tulikaa kama kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya, tukaona ni busara tuchukue jukumu la kumsafirisha Mchungaji hasa kutokana na sababu za kiusalama," alisema ofisa mmoja mwandamizi wa serikali wilayani hapa.
Alisema mchungaji huyo atalindwa akiwa msibani na atakaporejea Samunge.
Warundi, Wakenya, Waganda wakwama
Zaidi ya raia 100 kutoka Kenya, Burundi na Uganda, wamekwama Samunge kutokana na kusitishwa kwa tiba hiyo hadi Ijumaa.
Licha ya hatua hiyo ya kusitishwa kwa huduma kutangazwa mapema, maelfu ya watu, wakiwamo raia hao wa kigeni, waliendelea kumiminika Samunge kupata matibabu hayo.
Profesa Hakizimana Godefroid kutoka eneo la Muyumba, Burundi akiwa na ujumbe wa watu saba alisema wametumia siku saba kufika hapa na kwamba hatua hiyo imewasikitisha."Gari hili tumekodi kutoka Burundi hadi hapa, tunasikitika sana kukuta hakuna huduma na tunaambiwa ilitangazwa hapa Tanzania pekee kitu ambacho si kizuri," alisema Godefroid.
Alisema kutokana na taarifa ya tiba ya Mwasapila kusambaa karibu nchi zote za Afrika na nje ya bara,Serikali ilipaswa kutoa taarifa za kusitishwa kwa huduma hiyo katika balozi zake zote zilizopo nchini."Tumeondoka Burundi tukijua kuwa huku Tanzania tiba inatolewa tena tulijua hata siku za Pasaka tiba inaendelea. Taarifa zingesambazwa mapema tusingekuja sasa," alisema Godefroid.
Ofisa Uhamiaji ambaye yupo Samunge, Suleiman Saanane akishirikiana na polisi, juzi na jana walitumia muda mwingi kuwaelimisha raia hao wa nchi jirani juu ya kusitishwa kwa tiba hiyo na namna Serikali inavyoisimamia. Raia wa Kenya na Uganda, Peter Kimath na Joram Batengi, walishauri Serikali ya Tanzania kuipa hadhi tiba inayotolewa na Mchungaji Mwasapila wakisema, inawaponya watu na inavyoonekana, maelfu ya watu watafika Samunge.
"Hatuoni kama huyu mzee anapewa usaidizi ila tunachoona ni Serikali kukusanya kodi tu hapa ya magari na helikopta. Sasa kama wanapata fedha nyingi waitambue rasmi hii tiba na kuweka utaratibu mzuri," alisema Kimath. Batengi aliishauri Serikali kuboresha mazingira ya Samunge hasa barabara na eneo la tiba ili watu wanaotoka nchi za nje waamini kwamba tiba hiyo inaponya.
"Uganda wengi wanajua tiba hii na kuna ambao wanasema kuwa wamepona ila ukifika hapa huwezi kuamini kama tiba hii ni nzuri kwani mazingira ya hapa siyo mazuri na hata njia za kufika hapa ni mbaya sana," alisema Batengi.
Raia hao wanalazimika kubaki Samunge hadi Ijumaa siku ambayo Mchungaji Mwasapila atarejea na kuendelea kutoa tiba. Mchungaji Mwasapila anatarajiwa kurejea Samunge leo baada ya kushiriki katika mazishi ya mtoto wake Jackson (43), yaliyofanyika jana.
Msaidizi wa Mchungaji huyo, Frederick Nisajile aliliambia gazeti hili jana kuwa baada ya kurejea, wataanza maandalizi ya kuchemsha dawa ambayo itatumika Ijumaa.
Chanzo mwananchi.

CHENGE: SIJUI KAMA MIMI NI GAMBA CCM

Mh. Andrew Chenge
Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (pichani) amesema anasubiri taratibu za Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuona kama atapewa barua ya kumtaka ajivue nafasi zake za uongozi kwani hadi hivi sasa hajui kitu hicho.Kauli hiyo ya kwanza ya Chenge inakuja kipindi ambacho Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amekuwa akitangaza kwa nguvu mpango mkakati wa chama hicho kujivua gamba. Makada wa chama hicho wanaotakiwa kupima nafasi zao na uzito wa tuhuma zinazowakabili ni wale wanaohusishwa na kashfa mbalimbali zikiwamo za Richmond, Kagoda na wizi wa EPA. Hata hivyo, Chenge jana alipoulizwa na gazeti hili kuhusu kutajwa kwake kuwa mmoja wa wanachama wanaotakiwa kupima uzito wa tuhuma zinazowakabili na kujiondoa wenyewe ikiwa ni hatua ya chama hicho kujisafisha kwa kujivua gamba, alisema: "Sijui hicho kitu. Naheshimu vikao na taratibu za chama hilo ni jambo la chama si la vyombo vya habari." Alisema chama kina taratibu zake za kiutendaji na kuongeza: "Siwezi kuanza kuzungumza na vyombo vya habari kuhusu mambo ambayo yana taratibu zake ndani ya chama." Alisema kamwe hatakiuka taratibu za chama na kwamba uamuzi wote utakaofanyika au kutolewa huwa unafuata vikao vya chama.Alipoulizwa juu ya kusubiri kwake taratibu za chama wakati tayari jambo hilo linafahamika kwa umma alijibu: "Kwa ‘public’ ipi wewe? Mimi sijui hilo jambo, nasubiri taratibu za chama na siwezi kuzungumza zaidi nje ya chama." Akizungumzia utekelezaji wa maazimio ya Halmashauri Kuu ya chama hicho (NEC-CCM), Nnauye alisema taratibu zimekuwa zikiendelea na kuwataka wananchi kuwa na subira.Juzi, Nnauye alikaririwa akisema kwamba taratibu hizo zingefanyika baada ya Sikukuu ya Pasaka na kusisitiza: "Ambacho nimekuwa nikikisema kiko palepale." Mapema mwezi huu, NEC-CCM ilitoa muda wa siku 90 kwa watuhumiwa wote wa kashfa mbalimbali ndani ya chama hicho kujipima wenyewe na kujiondoa kwenye nafasi hizo vinginevyo, chama kingewang'oa kwa nguvu. Azimio hilo limekuwa likitangazwa kwa nguvu katika mikutano mbalimbali ya hadhara ikiwa ni mkakati wa chama hicho kurejesha imani chama kwa wananchi ambayo imeanza kupotea kutokana na tuhuma za ufisadi. Juzi, Nnauye akizungumza na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC Taifa), alisema chama hicho hakitishiki na uwezekano wa makada hao kuhamia upinzani. Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, akihutubia sherehe za kuzaliwa chama hicho Februari 5, mwaka huu alitangaza mkakati huo wa chama kujivua gamba na kurejea katika misingi ya maadili ya uongozi iliyorithi kutoka Tanu na CCM ya nyuma. Sekretarieti ya CCM kukutana kesho Katika hatua nyingine Sekretarieti ya CCM inatarajiwa kukutana kesho kujadili pamoja na mambo mengine, utekelezaji wa maazimio ya Nec-CCM. Kwa mujibu wa duru za kisiasa kutoka CCM, mkutano huo utajadili ajenda hiyo kwa kufanya tathmini ya azimio hilo na namna ya utekelezaji wake.Alipoulizwa jana, Nnauye alithibitisha kufanyika kwa mkutano huo lakini alisema ni kikao cha utendaji cha kawaida.Kwa mujibu wa Nnauye, kikao kama hicho kiliwahi kufanyika Mjini Dodoma baada ya kuundwa kwa sekretarieti hiyo na pia tayari ilikwishakutana Dar es Salaam. Alisema kikao hicho si maalumu wala cha dharura na kwamba hufanyika mara moja kwa wiki. "Siyo kikao cha dharura wala kikao maalumu, ni sehemu tu ya utendaji wa sekretarieti. Tunafanya vikao kama hivi mara moja kwa wiki, kwa hiyo hakuna kikao maalumu," alisema.
Chanzo Mwananchi

Wednesday, April 27, 2011

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Clement Senzota Mwete Mshana kuwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar es Salaam, leo, Jumatano, Aprili 27, 2011, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana George Yambesi inasema kuwa uteuzi huo unaanzia Alhamisi iliyopita, Aprili 21, mwaka huu, 2011.
Kabla ya uteuzi huo, Bwana Clement Senzota Mwete Mshana alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo).
Bwana Mshana anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bwana Dunstun Tido Mhando ambaye amemaliza muda wake wa utumishi kwa mujibu wa mkataba wake.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
27 Aprili, 2011

IRANI YATOA DOLA MILIONI 1.2 KUSAIDIA KILIMO KWANZA

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu (Kulia) akizungumza na Naibu Balozi wa Irani hapa nchini Bw Bahman Ahmadi(Kushoto) alipomtembelea Ofisini kwake leo. Mwingine ni Mshauri wa kibiashara katika Ubalozi wa Iran hapa nchini Bw Mobasher.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Lazaro Nyalandu (Kulia) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Naibu Balozi wa Irani hapa nchini Bw Bahman Ahmadi (Kushoto) alipomtembelea Ofisini kwake leo.Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Lazaro Nyalandu (Kushoto) katika picha ya pamoja na wageni wake Naibu Balozi wa Irani hapa nchini Bw. Bahman Ahmadi(Katikati) na Mshauri wa kibiashara katika Ubalozi wa Iran hapa nchini Bw. Mobasher (Kulia).
******************************
Na.Mwandishi wetu
Katika kusaidia kutekeleza kwa vitendo kampeni ya Kilimo Kwanza, Serikali ya Irani itaisadia Tanzania Dola za kimarekani Milioni moja pointi mbili (1.2Mill USDs) kwa ajili ya kampeni hiyo.
Taarifa hiyo njema imetolewa Jijini Dar es salaam leo, wakati Balozi Msaidizi wa Iran hapa nchini Bw Bahman Ahmadi alipotembelea Wizara ya Viwanda na Biashara na kukutana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mh. Lazaro Nyalandu.
Katika mazungumzo hayo yaliyojikita katika kuimarisha Uhusiano mwema bana ya nchi hizi mbili hasa kibiashara, Mh. Nyalandu kwa niaba ya serikali ya Tanzania, ameishukuru serikali ya Iran kwa msaada huo na kuahidi kuwa utatumika kama ulivyokusudiwa.
Aidha, Mheshimiwa Nyalandu amewakaribisha wawekezaji kutoka Iran kuja nchini na kushirikiana na wazalendo katika kutumia vyema fursa mbalimbali zilizopo hasa katika sekta ya Kilimo.
Na Mo Blog

Tuesday, April 26, 2011

UPCOMING MOVIE STAR!!!

Anaitwa Myrosh Kaida, amezaliwa 23rd October 1985, ni mwanafunzi kutoka St Augustine university of Tanzania ambapo yuko mwaka wa pili akichukua Bachelor of Education..
Ni mmoja kati ya watu ambao watashiriki filamu za Fiesta na hiki ni kipaji kipya kabisa kutoka MWANZA ambapo kuna wenzake wengine wengi ambao nitawaletea picha zao mmoja baada ya mwingine.. kwa kuanza nimeanza na huyu.
Ana malengo mengi sana lakini kubwa ni kuwa muigizaji mkubwa sana kwenye filamu na kufanikiwa katika kila atakachokifanya.
Hiki ni kipaji kipya kabisa kutoka MWANZA-TANZANIA.
Click

WATANZANIA LEO WAFANYA MAADHIMISHO YA MIAKA 47 YA MUUNGANO

Leo ni siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Pichani ni Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere akichanganya mchanga wa Tanganyika na Zanzibar katika sherehe za kuuasisi Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais Jakaya Kikwete leo amewaongoza watanzania katika kilele cha maadhimisho ya siku ya muungango wa Tanzania yaliyofanyika kitaifa visiwani Zanzibar.
Katika maadhimisho hayo rais Kikwete aliingia katika uwanja wa Amaan visiwani humo akiwa katika gari la wazi, ambalo lilizunguka uwanja huo huku rais kikwete kiwapungia mkono wananchi waliohudhuria.
Baada ya hapo rais aliwenda katika jukwaa maalum ambapo alipigiwa mizinga 21 kwa heshima yake huku wimbo wa taifa ukipigwa na bendi ya polisi.
Rais pia akagua gwaride la heshima na kisha vikosi vya jeshi la ulinzi vilipita mbele yake kwa mwendo wa pole na baadae vilipita kwa mwendo wa kasi.
Sherehe za maadhimisho hayo zimehudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Rais Mohammed Gharib Bilal na rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dakta ali Mohammed Shein pamoja mabalozi wa nchi mbali mbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania.
MATUKIO PICHANI:
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akiingia uwanja wa Amani Zanzibar(Unguja) leo hii kwenye sherehe ya maadhimisho ya miaka 47 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa kwenye jukwaa na rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mh. Dr. Mohamed Shein muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa Michezo wa Amaani mjini Unguja kuongoza sherehe za miaka 47 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Rais Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia mke wa muasisi wa muungano wa Tanganyika na Zanzibar Mama Fatma Karume mara baada ya kuwasili katika uwanja wa michezo wa Aman mjini unguja kuongoza sherehe za muungano wa Tanzania na Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete na Amiri Jeshi Mkuu akiukagua gwaride lilioandaliwa namajeshi ya ulinzi katika uwanja wa michezo wa Amani wakati wa shrehe za miaka 47 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Wakuu wakiwa jukwaa kuu
Sehemu ya umati wa wananchi
Umati wa wananchi
Viongozi na mabalozi wa nchi mbalimbali
Halaiki na Paredi.
Picha na Freddy Maro

Monday, April 25, 2011

MY STORY:AHMED ABDULRAHMAN SHEIKH…!!!

Ahmed Albaity.
Ahmed at the Hospital.
On 6th July 2007 was a wonderful and joyious day for me. My mother was flying to Abu dhabi.so she asked me to accompany her to Dar es salaam airport .on 7th July, My mother left.
On Sunday 8th July,early in the morning i left Dar and by noon, was already in Tanga. Here in Tanga we had this group known as combat riders so i had to let my friends knew that i was in Tanga.
In knowing that i was around,my friends immediately organized a walk to the shores of the Indian ocean where we normally used to go for physical exercise mostly karate. So i got myself ready n straight to my friends and at exactly 5pm we were already at the beach. we went straight to Raskazone Swimming Club ready for a warm up swim.
From nowhere i had this feeling of not having a swim, and besides i was a bit tired following a long safari i had hours ago.but as u know friends always so insisting,i decided to join them and couldn’t bring myself to let them down.As they say cold water can bring back unconcious to concious.and really,water made me a whole new self again. Sometimes later we decided to dive.
Since there wasn’t a bar up high from which we can dive towards the water,so we thought that one should climb over one’s shoulders and take a dive from there.so i went first. I did great and so our karate teacher asked me to go for the second time so that the others would learn from me.This time i did go faster n harder than before.
Accidentally i badly hit my head to the ocean floor since we were diving into shallow water. Abruptly i felt my whole body being electrified.while still in the water and concious i tried to swim off the water but my hands couldn’t move,not knowing what to do,i again tried to move myself but my whole body including my legs failed me.that was when i realized that i was badly hurt and couldn’t save myself.
So i was lying on water face down like a floating thing seeing me still floating, a friend of mine whose shoulders i used for diving, thought i was teasing
them so he came pulling me by the arm while telling others to get ready for their turn seeing me not responding, one of my friend realized that i wasn’t joking at all, then he came and tried to stood me up but was slippery as a fish on him.
The whole body was as if saying to him “we are being disconnected from the mind”. Seeing me at that condition, he was to some extent sent aback and scared too because he knew that i was really hurt. When he turned me up ( facing him) ,voicelessly told him that i was badly hurt. From the tone of my voice, was clear that i wasn’t okay.
From there, the rest of my friends n other people carried me out of water and hurriedly took me to Bombo hospital, one and only regional hospital here in Tanga.
On the way to the hospital i asked my friends not to mention a thing to my mother,
mostly i feared that she might not take it or being heart attacked.
At Bombo hospital, they examined me and realized that the situation was critical and therefore i had to be transfered to Muhimbili hospital(National hospital ) in Dar es salaam. On Monday afternoon i was on ma way to Dar.
It should be remembered that,at that moment, couldn’t feel my body n couldn’t move even a finger. In around 11 pm we were already in Muhimbili.The doctors started doing traction procedures right away.i was holed on the left n right side Of my head with heavy objects of 14 kg purposely for pulling out my neck. I stayed with those 14 kg for two weeks.
Then they removed them. I didn’t expect to be hurt this bad.i had thought that ones the traction procedure had been conducted i would walk again but no. All this time mum had not been informed. When she called that is when i decided to tell her what really happened n that the whole of my body was off.( quadriplegia) my mother was really shocked and cried a lot and so my other relatives. I stayed in Muhimbili for two months without any minor recovery.
Since my family was financially weak and couldn’t afford the costs ,i had to be returned to Tanga. After one month, my family got some sponsors who willingly flew me to India. The date was 1.01.2008. When i got there the doctors did neck surgery and that is when my voice came loudly as before. This really gave me hope that somehow i will be okay.but couldn’t give it a hundred percent. They also succeeded to treat the bed sores that were as a result of sleeping for a long time without moving.But the rest of my body was function less.
In India i was admitted in SAIFEE hospital in Mumbai where i stayed for 24 days. From there i was, returned back to Tanzania to proceed with treatment and physical exercise(Physiotherapy), i was told to return to India after six months time but like i said before, money wise my family isn’t good, so i didn’t go as suggested by doctors.
As for my sponsors,they refused as they noticed that there was no any positive development on my body, others even dared to say “why should we waste our money on someone who will never be wholly again?” Back here in Tanga i got serious sick. That is when i was taken to Kilimanjaro Christian Medical Centre(KCMC) in Moshi. Dr. Maya who is in the Orthopedic department was the one attended me, the date was 26th August 2008. I stayed there receiving
treatment mostly on malaria and bed sores. While i was there, Dr. Maya said that there is a possibility for me to be treated and so he told me to contact Dr. Chefarzt Dogmaskopp who is in Berlin Germany in VIVANTES KLINIKUM IN FRIEDRICHSHAIN.
According to that doctor, the cost for treatment in Germany is extremely high.
As i said before, personally can’t afford, so right now i have lost hope unless good Samaritans volunteer to help me get the treatment required, and Insha’allah God ,the almighty will bless them in whatever they touch.
All i can say to whoever reads this, i am a helpless person in everything: eating, bathing, tending myself and other physical activities.
So i hope there are good caring and loving people who would love to see or hear that i have recovered completely. Your prayers are also important.
Whoever would like to help in anyway, would contact me through the email address:
ahmedalbaiy84@hotmail.com
THANK YOU AND GOD BLESS YOU ALL.
Click

JUMUIYA YA WATANZANIA (TANZ-UK) IKISHIRIKIANA NA UBALOZI UK YATANGAZA DIASPORA III

Do you want to find out the outcome of the last conference (Diaspora II)? Are you concerned about the role Diaspora plays in your life abroad?
Do you have questions about jobs or investments opportunities at home?Do you have suggestions on Diaspora Matters? Have you been waiting to meet key stakeholders to raise your concerns?
The time has never been so right!! You now have a good opportunity to meet and speak to various individuals one-to-one who may have answers to your questions? Key players from various sectors are expected to attend this year’s conference. Come along. Tell your fellow Tanzanians. You cannot afford to miss out on the Diaspora III 2011 Conference at Wimbley in London.
For more info visit:
http://tanzaniahighcommission.co.uk/
or
www.watanzaniauk.com/news
REGISTER NOW FOR THE EVENT AT:
http://tanzaniahighcommission.co.uk/
Organized by Tanzania High Commission-UK)
By the Communications Office – TANZ-UK
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
KUSOMA HABARI ZILIZOPITA BOFYA NENO OLDER POSTS HAPO JUU ASANTE SANA KWA KUTEMBELEA NA KARIBU TENA