Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu (Kulia) akizungumza na Naibu Balozi wa Irani hapa nchini Bw Bahman Ahmadi(Kushoto) alipomtembelea Ofisini kwake leo. Mwingine ni Mshauri wa kibiashara katika Ubalozi wa Iran hapa nchini Bw Mobasher.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Lazaro Nyalandu (Kulia) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Naibu Balozi wa Irani hapa nchini Bw Bahman Ahmadi (Kushoto) alipomtembelea Ofisini kwake leo.Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Lazaro Nyalandu (Kushoto) katika picha ya pamoja na wageni wake Naibu Balozi wa Irani hapa nchini Bw. Bahman Ahmadi(Katikati) na Mshauri wa kibiashara katika Ubalozi wa Iran hapa nchini Bw. Mobasher (Kulia).
******************************
Na.Mwandishi wetu
Katika kusaidia kutekeleza kwa vitendo kampeni ya Kilimo Kwanza, Serikali ya Irani itaisadia Tanzania Dola za kimarekani Milioni moja pointi mbili (1.2Mill USDs) kwa ajili ya kampeni hiyo.
Taarifa hiyo njema imetolewa Jijini Dar es salaam leo, wakati Balozi Msaidizi wa Iran hapa nchini Bw Bahman Ahmadi alipotembelea Wizara ya Viwanda na Biashara na kukutana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mh. Lazaro Nyalandu.
Katika mazungumzo hayo yaliyojikita katika kuimarisha Uhusiano mwema bana ya nchi hizi mbili hasa kibiashara, Mh. Nyalandu kwa niaba ya serikali ya Tanzania, ameishukuru serikali ya Iran kwa msaada huo na kuahidi kuwa utatumika kama ulivyokusudiwa.
Aidha, Mheshimiwa Nyalandu amewakaribisha wawekezaji kutoka Iran kuja nchini na kushirikiana na wazalendo katika kutumia vyema fursa mbalimbali zilizopo hasa katika sekta ya Kilimo.
Na Mo Blog

0 comments:
Post a Comment