ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A LOWEST COST AND ALSO SEND TO US NEWS, EVENTS FOR MORE INFORMATION CONTACT US TELEPHONE: +919160901191 E-mail: ally.shaaban@yahoo.com | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU NA PIA TUTUMIE HABARI, MATUKIO KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI KWA SIMU: +919160901191 Barua Pepe: ally.shaaban@yahoo.com | DO YOU NEED TO CREATE BLOG CONTACT US HERE | UNAHITAJI KUFUNGUA BLOG WASILIANA NASI HAPA

Monday, February 28, 2011

Nayo Harambee YA Kuchangia Gongo la Mboto Mjini London Yafana!


 MDAU FREDDY MACHA ALKUWA MSTARI WA MBELE KATIKA KUCHANGIA
 MDAU ABUU FARAJI AKIPEWA MKONO WA ASANTE
MR & MRS KAMWANO SABUNI WAKIKABDHI MCHANGO WAO
 MISS FB LYIMO NA MDAU CIDI HAWAKUBAKI NYUMA.
 WAKURUGENZI WA SERENGETI FREIGHT WAKITOA MCHANGO WAO
 WADAU KUTOKA PANDE ZOTE ZA LONDON WAKIWA KATIKA HARAMBEE
 MDAU ALI HAMISI NA RAFIKI YAKE WAKIKABIDHI MCHANGO WAO
DADA LEMNA NA WATOTO WAKE WALIKUWA MSTARI WA MBELE KATIKA KUCHANGIA
---------------------
Salaam
Tunapenda kutoa shukrani zetu za Dhati kwa watanzania wote  waishio LONDON UK walioweza kufika jana jioni AFRICAN VILLAGE BAR & RESTAURANT kuchangia waathirika wa Gongo la Mboto Tanzania. Kwa mda wa masaa mawili  
 
tumeweza kukusanya Jumla ya  pesa taslim Pounds £600, pia tumekusanya Nguo nyingi kutoka kwa watu mbalimbali na vifaa vingine mbali mbali. 

Ningependa kutoa shukrani za dhati kutoka URBAN PULSE,MISS JESTINA BLOG,AIL TV, LOCUS IMPEX SHIPPING CO, SHILLA FRISCH, NA Utawala wa AFRICAN VILLAGE BAR & RESTAURANT LONDON kwa kusaidia na kuwezesha kufanikiwa kwa zoezi la jana.

Mungu Ibariki Africa, Mungu Ibariki Tanzania
Asanteni
***HAPPY BIRTHDAY *** 
FARIDA MOHAMED
LEO NI SIKU YA KUZALIWA KWA MWANADADA NA MDAU WA BLOG HII FARIDA MOHAMED WA DAR ES SALAAM TANZANIA.
BLOG HII INAUNGANA NA FAMILIA,NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI KUKUTAKIA KILA LA HERI KATIKA SIKU YAKO HII YA KUZALIWA.
ALLAH AKUJAALIE AFYA NJEMA NA MAISHA MAREFU,BUSARA NA HEKIMA  KATIKA MAISHA YAKO.
HAPPY BIRTHDAY TO YOU.
************

Mawaziri wa Nje kuijadili Libya
Mawaziri wa mambo ya nje kutoka duniani kote wanakutana mjini Geneva Uswisi, kujadili hatua za kuchukua kukabiliana na janga la kibinaadam linalozidi kukua nchini Libya.
Waandamanaji Libya karibu na picha ya Gaddafi
Maelfu ya wahamiaji, wengi kutoka Misri, wamekwama katika mpaka wa Libya na Tunisia, huku maelfu wakiwasili kila saa, kwa mujibu wa maafisa wa Umoja wa Mataifa.
Waandishi wa habari wanasema kuna hali ya wasiwasi, huku kiongozi Muammar Gaddafi akiendelea kuidhibiti Tripoli.
Wakimbizi kutoka Libya
Marekani imeunga mkono wazi wazi makundi yanayompinga Gaddafi mashariki mwa Libya.
Akifungua mkutano mjini Geneva, Kamishna wa haki za binaadam wa Umoja wa Mataifa Navi Pallay, amezionya mamlaka za Libya kuwa ushambuliaji wa raia unaotapakaa, unaweza kufikia kuwa makosa ya jinai katika sheria za kimataifa.
"Ni suala la masikitiko makubwa kwamba damu imemwagika katika kukaribisha mabadiliko".
Umoja wa Mataifa kuweka vikwazo kwa Gaddafi
Akizungumza akiwa njiani kuelekea kwenye mkutano huo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton amesema Marekani "inaungana na wananchi wengi wa Libya wa upande wa mashariki".
Bi Clinton amesema atajadili masuala ya kibinaadam na kisiasa na mawaziri wengine kutoka Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika kaskazini katika mkutano wa baraza la haki za binaadam, mjini Geneva.
Watu wasiopungua 1,000 wanadhaniwa kuawa katika wiki mbili za ghasia, ambapo miji ya mashariki imedhibitiwa na majeshi yanayopinga serikali.

Tuesday, February 22, 2011

Ambwene Yesaya (aka AY) in Hyderabad-India!!!

KANUMBA: TUSILAUMIWE KUPOROMOKA KWA MAADILI.
 
 Muigizaji maarufu wa filamu nchini Steven Charles Kanumba ameibuka na kusema kwamba, wasanii si chanzo cha kuporomoka kwa maadili katika jamii bali tatizo hilo linasababishwa kwa kiasi kikubwa na utandawazi unaombatana na mabadiliko ya teknolojia duniani. Akiwasilisha mada kuhusu Harakati za kuivusha tasnia ya filamu katika ngazi za kimataifa kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila Jumatatu kwenye Ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Kanumba alipuuza malalamiko kwamba, wasanii wa filamu wamekuwa chanzo cha kuipotosha jamii kupitia yale wanayoyaigiza na kusema kwamba,malezi na utandawazi ni tatizo kubwa kwa sasa katika taifa na wazazi hawana budi kudhibiti watoto wao ili kuwaepusha na wimbi hili. “Maadili hayako katika filamu tu,tunapozungumzia maadili ni katika nyanja nyingi.Leo mtoto mwenye miaka tisa anamiliki simu tena yenye internet,humo anaangalia facebook na picha za ajabu halafu mtoto huyu akiharibika watu wanasema ni filamu,hii si kweli” alisisitiza Kanumba ambaye amecheza zaidi ya filamu 40 hadi sasa. Aliongeza kwamba,kwa kawaida wanapoandaa filamu wamekuwa wakiandika umri wa watazamaji wake lakini wazazi wengi wamekuwa wakipuuza na kuwaacha watoto kuangalia filamu ambazo hawapaswi kuangalia.Alitaja filamu kama ya This Is It ambayo anasema kuna watoto hawaruhusiwi kuiangalia lakini wazazi na walezi wengi wanapuuza hilo. “Filamu zetu tunazotengeneza zinakuwa na ujumbe kwa jamii,zinabeba masuala yaliyomo ndani ya jamii.Suala la nani aangalie kilichomo tumekuwa tukiziwekea umri wa watazamaji.Naomba mniambie jamani hayo tunayoyaonyesha katika filamu yetu hayapo katika jamii?Na kwa nini sasa tulaumiwe kwa mambo ambayo yako ndani ya jamii zetu” alihoji Kanumba. Akizungumzia suala la wao kuwa waongozaji,waandishi wa simulizi (script writers) na watafutaji mandhari (location) katika filamu moja,Kanumba alisema kwamba,ni suala la kawaida na limekuwa likifanyika katika nchi mbalimbali duniani na mara nyingi hufanywa ili kukwepa mlolongo mrefu na pia kubana matumizi. Juu ya wizi katika kazi zao,Kanumba alisema kwamba,Chama cha hakimiliki (Cosota) kimekuwa kikijtahidi lakini tatizo limekuwa kwenye nguvukazi ya mamlaka hiyo lakini pia sheria ambazo zinaonekana hazikidhi matakwa. Hata hivyo,akizungumzia hilo kwa niaba ya Cosota,Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego alisema kwamba,sheria mpya za hakimiliki ziko katika kiwango cha kupelekwa bungeni kwa ajili ya kupitishwa na uwezekano mkubwa ni kwenye bunge lijalo la mwezi wa nne.
TANZANIAN STUDENTS ASSOCIATION OF HYDERABAD (TSAH)
Ndugu Watanzania, tarehe 27 February 2011, jumapili, kutakua na mkutano wa wana-TSAH, utakaofanyika nyumbani kwa Dany Msemo, Yaprar,Sainkpur, kuanzia saa tisa na nusu alasiri.
Tunaombwa kufika bila kukosa kwa ajili ya ufafanuzi wa mambo kadhaa yaliyojitokeza.
Pia, kikao hicho kitajadili mambo mbalimbali yanayohusu jumuiya yetu.
Mbali na hayo, ijulikane wazi kuwa, Katibu mkuu wa TSAH amepokea barua ya kujiuzulu kwa Mwenyekiti wa TSAH, na Makamu wake.
Mamlaka husika ndio inaweza kukubali wajiuzulu au kukataa kujiuzulu kwao baada ya kujiridhisha na maombi hayo.
Tunaombwa kufika wote bila kukosa.
Uwepo wako ni mhimu sana katika uimarishaji wa jumuiya yetu TSAH.
Katibu Mkuu TSAH
John Gagah
+91 950 26 96 870
jonbalele@gmail.com

Sunday, February 20, 2011

***HAPPY BIRTHDAY *** 
HUSSEIN MSILIMIWA
LEO NI SIKU YA KUZALIWA KWA MWANAKAKA NA MDAU WA BLOG HII HUSSEIN MSILIMIWA HYDERABAD (SINKPUR) INDIA.
BLOG HII INAUNGANA NA FAMILIA,NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI KUKUTAKIA KILA LA HERI KATIKA SIKU YAKO HII YA KUZALIWA.
ALLAH AKUJAALIE AFYA NJEMA NA MAISHA MAREFU,BUSARA NA HEKIMA  KATIKA MAISHA YAKO.
HAPPY BIRTHDAY TO YOU.
************

Sunday, February 13, 2011

MSIBA HYDERABAD-INDIA

 
NICKSON MEMBI (R.I.P)
TANZANIA STUDENT ASSOCIATION HYDERABAD(TSAH)
Jumuiya ya wanafunzi wa Kitanzania Hyderabad India kwa masikitiko  makubwa mno inatangaza kifo cha mwanafunzi NICKSON MEMBI kilichotokea India.Habari ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu popote walipo.Taratibu  za mazishi zinapangwa.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
KUSOMA HABARI ZILIZOPITA BOFYA NENO OLDER POSTS HAPO JUU ASANTE SANA KWA KUTEMBELEA NA KARIBU TENA