SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, November 4, 2011

UNDP YAZINDUA RIPOTI YA MAENDELEO YA DUNIA 2011

Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Tanzania Bw. Alberic Kacou akitoa hotuba kwenye hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo Duniani ya Mwaka 2011, ambapo amesema ripoti hiyo inaonyesha jinsi ambavyo uharibifu wa mazingira unavyochochea kuwepo kwa matabaka ya watu kutokana na kuongeza athari kwa watu ambao tayari hawana unafuu wa kimaisha. Ameelezea jinsi ambavyo matabaka yanayohusiana na hali ya maendeleo miongoni mwa wanadamu yanavyozidisha uharibifu wa mazingira.
Mshauri wa Masuala ya Kiuchumi wa UNDP Bw. Amarakoon Bandara (katikati) akiwasilisha ripoti hiyo kwa wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa ripoti hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa ESRF Dk. Hoseana Lunogelo.
 
Dk. Hoseana Lunogelo akitoa tathmini yake kuhusiana na ripoti hiyo wakati wa kipindi cha majadiliano.
 
Wadau wa Umoja wa Mataifa na wageni waalikwa wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi katika hafla hiyo.
 
Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Peniel Lyimo, akitoa hotuba ya uzinduzi huo ambapo ameelezea umuhimu wa kuwa na ripoti kama hizo kwa kuwa zinatoa muelekeo halisi wa maendeleo ya dunia katika nyanja mbalimbali. Kutoka kushoto ni Dk. Hoseana Lunogelo, Amarakoon Bandara  na Alberic Kacou.
 
Peniel Lyimo, akikata utepe kuashiria uzinduzi huo akisaidiwa na  Alberic Kacou. Uzinduzi ukifanywa rasmi.
 
Wawakilishi wa ofisi mbalimbali za ubalozi, Umoja wa Mataifa na viongozi wa serikali katika uzinduzi huo.

0 comments:

Post a Comment