SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, November 13, 2011

Mbunge Wa Mbeya Mjini(CHADEMA)Joseph Mbilinyi Alivyotuliza Fujo Za Wamachinga Mkoani Mbeya Zilizodumu Kwa Siku Mbili

Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mheshimiwa Evans Balama mwenye shati la miraba ya samawati(Katikati) katika picha ya pamoja kabla ya Mheshimiwa Mbunge Joseph Mbilinyi  Kuhutubia. 
Mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Bwana Joseph Mbilinyi akiwasihi wananchi kuwa watulivu na kwamba mgogoro umekwisha na utatuliwe kisayansi badala ya kisiasa na pia amewapongeza machinga kwa utulivu waliouonyesha bila kupora bidhaa madukani.
Halaiki ya wananchi waliofika kuusikiliza mustakabali wa wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama machinga kuendelea na biashara zao katika maeneo yao ya awali, wakati utaratibu wa maeneo ya kufanyia biashara ukiandaliwa na halmashauri ya jiji la Mbeya.
Maelfu ya wananchi waliofika kuusikiliza mustakabali wa wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama machinga kuendelea na biashara zao katika maeneo yao ya awali, wakati utaratibu ukiandaliwa na halmashauri ya jiji la Mbeya.
Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), likiwasaidia Jeshi la Polisi kuweka hali ya amani na utulivu mara baada ya kuisha kwa mkutano uliofanyika katika kituo cha mabasi madogo ya abiria (daladala) eneo la Kabwe Mwanjelwa jijini Mbeya.
Wananchi wakirudi makwao kwa furaha baada ya mgogoro uliodumu kwa siku mbili kumalizika, baada ya hotuba ya Mheshimiwa mbunge wa jimbo la Mbeya(Chadema) mjini Bwana Joseph Mbilinyi.
Credit To H@ki Ngowi

0 comments:

Post a Comment