Naibu
Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara
akimpatia kitabu cha taarifa ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara kwa
Wizara hiyo leo nyumbani kwa Mjane wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu
Julius Nyerere, Mama Maria Nyerere mara baada ya kumtembelea nyumbani
kwake Butiama, mkoani Mara.
Mjane
wa Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, Mama Maria Nyerere
akizungumza na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Dk. Fenella Mukangara wakati alipombelea nyumbani kwake
kijijini Butiama, mkoani Mara leo (jana). Kulia kwa Naibu Waziri ni
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi Sihaba Nkinga pamoja na Viongozi
waandamizi wa Wizara hiyo.
Mtoto
wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Makongoro Nyerere
akitoa historia ya makaburi ya wazazi wa mwalimu Julius Nyerere
yaliyopo mwitongo, Butiama kwa Viongozi waandimizi wa Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo waliokwenda kumjulia hali Mama Maria
Nyerere.
Mkuu
wa Mkoa wa Mara (kulia) John Tupa akipata maelezo juu ya majukumu ya
Idara ya Habari (Maelezo) kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya
Habari (Maelezo) Ndg. Raphael Hokororo mara baada ya kutembelea banda
la Idara hiyo katika maonyesho ya maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa
Tanzania Bara kwa Wizara hiyo yanayoendelea katika uwanja wa kumbukumbu
ya Joseph Kazurira Nyerere, huko Butiama mkoani Mara.
Mkuu
wa mkoa wa Mara John Tupa(katikati) akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani) katika banda la Idara ya Habari kuhusiana na
maandalizi ya mbio za mwenge wa uhuru unaotarajia kuwashwa mkoani humo.
Wa pili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Bi. Sihaba Nkinga na kwanza na kwanza kushoto ni
kaimu Afisa Utamaduni na Michezo, Shekheadi Saidi. Wengine wa
pili kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa huo, Clement Lujaji na wa kwanza
kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Karaine Kimaati.
Naibu
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fenella Mukangara mara
baada ya kumtembelea Mjane wa Mwalimu Nyerere, Mama Maria Nyerere
kijijini kwake Butiama, mkoani Mara leo. Wengine katika picha ni
Viongozi waandamizi wa Wizara hiyo, kulia hiyo ni mtoto wa Hayati Baba
wa Taifa, Madaraka Nyerere.
Picha Zote na Anna itenda-MAELEZO
0 comments:
Post a Comment