SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, October 18, 2011

Mama Salma Kikwete Atoa Heshima Za Mwisho Kwa Mwili wa Marehemu Mama Han Bing Aliyeuwawa na Majambazi

Mmoja wa Wanafamilia akimbembeleza mtoto wa marehemu, lady Han Bing
Picha ya Marehemu Mama Han Bing mke wa Mwenyekiti wa jumuiya ya wafanya biashara wa kichina nchini Tanzania
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA ,akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu Mama Han Bing mke wa Mwenyekiti wa jumuiya ya wafanya biashara wa kichina nchini Tanzania aliefariki oktoba 11,2011 jijini Dar es Salaam kwa kuuwawa na majambazi wasiojulikana
 Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete akimpa pole mume wa marehemu.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimfariji mtoto wa marehemu Han Bing wakati wa ibada ya kumuaga iliyofanyika Dar es Salaam. Oktoba 11, majambazi yalimuua Han kwa risasi na kumpora sh milioni 30 alizokuwanazo kwenye gari.
Mama Salma Kikwete akiwa katika misa pamoja  na viongozi mbalimbali.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh. Bernard Membe akitoa salamu za pole wa wafiwa na wanajumuiya ya kichina katika msiba huo.
Ndugu, Jamaa na marafiki wakiomboleza katika msiba huo.
Ndugu wa Marehemu wakiwa katika maombolezo ya msiba huo
Wanafamilia katika Misa ya buriani
Kamanda wa kanda maaluum ya kipolisi Suleiman Kova akiwapa pole wmna jumuiya ya wachina waishio Tanzania jijijinDra es salaam wakati walipokwenda kuaga mwili wa Mama Han Bing alieuwawa na majambazi oktoba 11.2011.
Picha na Zote na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO

1 comments:

Anonymous said...

MBONA MTANZANIA AKIUAWA HAMANGAIKI HIVI??????
NI WATANZANIA WANGAPI WANAUAWA LAKINI SERIKALI INAKAA KIMYA????????

Post a Comment