SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, October 18, 2011

Abiria 30 wanusurika Kifo katika ajali mbaya iliyotokea eneo la Mbalizi Mkoani Mbeya

Pichani ni gari hilo lililopinduka.
AJALI ya gari ambayo hufanya ruti ya kusafirisha abiria kutoka Mwanjelwa jijini Mbeya mpaka mji mdogo wa Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini,  ambayo imetokea kwenye mteremko wa Mbalizi ambapo zaidi ya abiria thelathini wamenusurika kifo, baada ya gari kushindwa kupandisha mlima hali iliyopelekea kupinduka.
Tukio hili limetokea siku ya Jumapili. Baada ya kupinduka kwa gari hiyo ambayo hufanya ruti ya kusafirisha abiria kutoka Mwanjelwa jijini Mbeya hadi mji mdogo wa Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini hatimaye lilinusurika kutumbukia bonde la mtoni Mbalizi tukio lililotokea siku ya Jumapili.
Jeshi la polisi Usalama barabarani Mbeya linanapaswa kufanya uchunguzi wa kina ili kuweza kubaini magari yenye kasoro kwa lengo la kuepukana na ajali zisizokuwa za lazima.
PICHA KWA HISANI YA MBEYA YETU BLOG.

0 comments:

Post a Comment