SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, October 31, 2011

Alichokisema Mbunge wa Arusha Mjini(CHADEMA)Mheshimiwa Godless Lema Kwa Waandishi Wa Habari

Mbunge wa Arusha mjini(CHADEMA)Mheshimiwa Godless Lema 
********
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Nawasalimu nyote.
Nimewaita kutoa taarifa juu ya kilichotokea juzi tarehe 28/10 /2011 baada ya kuhairishwa shauri la kesi ya uchaguzi iliyoko mahakamani dhidi yangu .Tarehe 27/10/2011 kesi hii ilihahirishwa na Judge A . Mujuluzi kwani usikilizaji wake usingewezekana kwa kuangalia idadi ya watu walivyokuwa wamejaa pale mahakamani ,maagizo yalitoka kwamba shauri litakalofuata mahakama iwe imetayarisha vipaza sauti kwa ajili ya usikilizwaji wa kesi hiyo.

Lakini kwa bahati mbaya jambo hilo halikuwezekana kabisa kwa sababu ambazo baadaye Mh. Judge alizitolea ufafanuzi mzuri na mawakil wa pande zote wakakubaliana kuendelea na shauri hilo bila vipaza sauti lakini kwa ahadi kuwa mpango huo unatekelezwa haraka na wakati mwingine wa kesi itakapokuja mahakami utaratibu huo utakuwa umekamilika.
Jambo la kushangaza siku hiyo wakati nafika mahakamani nilikuta polisi wengi sana na wamevaa nguo zinazoashiria tayari wako kwa mapambano na watu wakizuiwa kabisa kuingia mahakamani kuanzia geti kubwa na polisi walikuwa wanajaribu kuhoji kila mtu kuwa anakwenda kusikiliza shauri gani na kama mtu angejibu ni shauri la kesi ya uchaguzi basi halikuwa haruhusiwi kuingia mahakamani kuanzia geti la mwanzo wa mahakama.
Nilikata dhambi hii na uonevu huu kwa wapiga kura wangu nilimfuata OCD Bwana Zuberi Mwombeji kuongea naye juu ya jambo hili la kuzuia watu na alikataa kabisa na kusema “ hao watu wanaenda wapi kwani kesi inawahusu ? na yeyote atakaye vuka hawa polisi hapa hatakuwa chambo na kuniambia kuwa hata watu wakija maelfu na maelfu mahakamani lazima kesi hii initie kidole “ ( Zuberi) , tulibishana huku nikijaribu kutetea utu wangu na mamlaka yangu kama Mbunge , ikawa zogo mahakamani muda mrefu bila mafanikio mpaka nilipomuomba wakili wangu aingilie kati kisheria ndipo watu waliporuhusiwa kwenda kusikiliza kesi .

Baadaye baada ya kesi nilikuta wananchi waliokuwa nje ya chumba cha mahakama wakiwa na hasira huku wakilalamika na kwani kwa mara nyingine tena OCD Zuberi alikuwa amewaita tena wananchi PANYA na akiamuru polisi wa ngazi ya chini kwa kusema “sogezeni hao PANYA nyuma”Lugha hii ni mbaya haikubaliki hata kidogo, niliongea na wanachi na na kukemea lugha hii kwa hasira baadaye nilielekea ofisini kwangu kwa miguu huku nikisindikizwa na polisi na watu wengi waliokuwa mahakamani na baadhi ya watu niliomba tukutane nao ofisini kwangu wengi wakiwa ni viongozi wa matawi na vijana naotarajia kuwa mashaidi katika kesi ya uchaguzi,niliongea nao ofisini kwangu nikawaaga nikaondoka na wachache niliwaacha ofisini kwangu na Katibu wangu na baadhi ya wageni wengine,baada ya muda nilipigiwa simu kuwapolisi wameingia ofisini kwangu na kukamata watu wote , nilimpigia simu Kaimu RPC kumueleza suala hili nayeye alisema ni bora nifike ofisini kwake tuongee jambo hili ,nilipofika nilimueleza jinsi OCD anavyoendelea kufanya kazi kibabe, kwa shuruti za siasa na bila busara na kuhumiza watu bila sababu , alinisikiliza kwa muda usiopungua saa nzima na baadae nikifikiri nimeeleweka ghafla niliwekwa chini ya ulizi na kuambiwa nitoe maelezo na kushitakiwa kwa kosa la kuongea watu nje kabisa ya viwanja vya Mahakamani na ofisini kwangu .

Ninafahamu mipango yote ya siri na wazi iliyokusudiwa kwangu na wafuasi wangu , ndio maana sishangai kwamba vyama vingine vinaweza kufanya mikutano na maandamano bila kibali na kuchungwa na polisi na yeye OCDna polisi walipohojiwa na waandishi wa habari juu ya jambo hilo UVCCM kufanya mkutano na maandamano bila kibali,, Polisi walisema wanataarifa na wametoa onyo kwa viongozi waliohusika.
Habari zaidi

Birthday Ya 8020 FashionsYafana Sana Leo(Jana)

 Mgeni Rasmi katika hafla ya kutimiza miaka 5 ya 8020 Fashions Blog, Mbunge wa Viti Maalum wa CCM,Mh. Angelah Kairuki akisoma hotuba fupi ya ufunguzi wa hafla hiyo iliyofanyika mchana wa leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee V.I.P Hall jijini Dar es Salaam.
 Mwanzilishi na Mmiliki wa Blog ya 8020 Fashions,Shamim Mwasha a.k.a Zeze akizungumza wakati wa hafla hiyo ambayo ilihudhuliwa na wadau mbali mbali na kufana sana.
 Mgeni Rasmi katika hafla hiyo ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum wa CCM,Mh. Angelah Kairuki akiwa na Da' Shamim Zeze na wadau kwenye Red Kapet.
 Mc wa Shughuli hiyo,Dina Marios (kulia) akizungumza na Da' Shamim Mwasha wakati wa hafla hiyo iliyofana sana na kupendeza.
 Wadau Mbali Mbali walijitokeza kumpa tafu Da' Shamim Mwasha katika hafla ya Besdei ya kuzaliwa kw Libeneke lake la 8020 Fashions Blog kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee V.I.P Hall,jijini Dar 
  Mgeni Rasmi katika hafla hiyo,Mbunge wa Viti Maalum wa CCM,Mh. Angelah Kairuki akimlisha kipande cha keki Da' Shamim Mwasha.
 Mrs. Ankal (kulia) akimlisha kipande cha keki Da' Shamim,huku Mh. Angelah Kairuki akishuhudia.Keki hiyo ni zawadi maalum kutoka kwa Ankal Michuzi a.k.a Mzee wa Libeneke. 
Dina,Joyce na Sophia ni full kitenge.
Da' Mwamvita Makamba (pili shoto),Da' Mwammy Mlangwa (pili kulia) wakiwa na wadau wengune wa Vodacom Tanzania.
 Mrs Ankal akikabidhiwa Nondozz ya Ankal ikiwa ni sehemu ya Shukrani kwake kwa mchango mkubwa katika libeneke la Kublogu.

Leo Vodacom Foundation imekamilisha Kutoa Madawati 225 Kwa Shule 5 Za Wilaya Ilala na Kinondoni

Afisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akimkabidhi msaada wa madawati Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwongozo  Elly Shuma  kwa niaba ya walimu wenzake wa shule tano zilizonufaika na msaada huo wa madawati  225 yenye thamani ya  zaidi ya shilingi Milioni shirini na ishirini na tano elf(20,25,000)kwa shule tano za wilaya ya Kinondoni na Ilala,Jumla ya  madawati Elf moja  yenye thamani ya Milion 90 yametolewa msaada kwa shule 20 za Mkoa wa Dares Salaam  mwaka huu.
Afisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akiongea na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwongozo iliyopo Wilaya ya Kinondoni Jijini Dares Salaam mara baada ya kukabidhi msaada wa madawati  225 yenye thamani ya  zaidi ya shilingi Milioni 20,25,000,kwa shule tano za wilaya ya Kinondoni na Ilala,Jumla ya  madawati Elf moja  yenye thamani ya Milion 90 yametolewa msaada kwa shule 20 za Mkoa wa Dares Salaam  mwaka huu.
Afisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akiongea na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwongozo iliyopo Wilaya ya Kinondoni Jijini Dares Salaam mara baada ya kukabidhi msaada wa madawati  225 yenye thamani ya  zaidi ya shilingi Milioni 20,25,000,kwa shule tano za wilaya ya Kinondoni na Ilala,Jumla ya  madawati Elf moja  yenye thamani ya Milion 90 yametolewa msaada kwa shule 20 za Mkoa wa Dares Salaam  mwaka huu. 
Afisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akiongea na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwongozo iliyopo Wilaya ya Kinondoni Jijini Dares Salaam mara baada ya kukabidhi msaada wa madawati  225 yenye thamani ya  zaidi ya shilingi Milioni 20,25,000,kwa shule tano za wilaya ya Kinondoni na Ilala,Jumla ya  madawati Elf moja  yenye thamani ya Milion 90 yametolewa msaada kwa shule 20 za Mkoa wa Dares Salaam  mwaka huu.

NHC yatiliana saini ya makubaliano ya mikopo ya nyumba na benki saba za hapa nchini

 Waziri wa Ardhi,Mh. Prof. Anna Tibaijuka akihutubia wakati wa hafla ya kutiliana saini ya makubaliano baina ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Mabenki  ili kuwezesha kutoa mikopo ya Nyumba kwa wananchi hapa nchini .hafla hii imefanyika leo kwenye hoteli ya Hyatt Kilimanjaro,jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Nyumba Tanzania,Eng. Kesogukewele Msita akihutubia katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba nchini,Nehemiah Mchechu akitioa hotuba yake wakati wa hafla ya kutiliana saini ya makubaliano baina ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Mabenki  ili kuwezesha kutoa mikopo ya Nyumba kwa wananchi hapa nchini .hafla hii imefanyika leo kwenye hoteli ya Hyatt Kilimanjaro,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Lawrence Mafuru akisoma hotuba yake fupi kwa niaba ya Mabenki ya hapa nchini wakati wa hafla ya kutiliana saini ya makubaliano baina ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Mabenki  ili kuwezesha kutoa mikopo ya Nyumba kwa wananchi hapa nchini .hafla hii imefanyika leo kwenye hoteli ya Hyatt Kilimanjaro,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba Tanzania,Nehemiah Mchechu akipena mkono wa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC,Laurance Mafuru mara baada ya kutiliana saini ya makubaliano baina ya Shirika hilo na Benki ya NBC ili kuwezesha kutoa mikopo ya Nyumba kwa wananchi hapa nchini .Wanaoshuhudia tukio hilo ni Waziri wa Ardhi,Mh. Prof. Anna Tibaijuka na Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Nyumba Tanzania,Eng. Kesogukewele Msita.hafla hii imefanyika leo kwenye hoteli ya Hyatt Kilimanjaro,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba Tanzania,Nehemiah Mchechu pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC,Laurance Mafuru wakitiliana saini ya makubaliano kuwezesha kutoa mikopo ya Nyumba kwa wananchi hapa nchini .Waliosimama wakishuhudia tukio hilo ni Waziri wa Ardhi,Mh. Prof. Anna Tibaijuka na Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Nyumba Tanzania,Eng. Kesogukewele Msita.hafla hii imefanyika leo kwenye hoteli ya Hyatt Kilimanjaro,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba Tanzania,Nehemiah Mchechu pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB,Mark Wiessing wakitiliana saini ya makubaliano kuwezesha kutoa mikopo ya Nyumba kwa wananchi hapa nchini .Waliosimama wakishuhudia tukio hilo ni Waziri wa Ardhi,Mh. Prof. Anna Tibaijuka na Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Nyumba Tanzania,Eng. Kesogukewele Msita.hafla hii imefanyika leo kwenye hoteli ya Hyatt Kilimanjaro,jijini Dar es Salaam. 
Picha na Habari Zaidi

Sunday, October 30, 2011

KILA LA HERI KAKA NAKUTAKIA SAFARI NJEMA MOLA AKUFIKISHE SALAMA NYUMBANI

 SADDALAH MBEYU 
NAKUTAKIA MAFANIKIO KATIKA MAISHA YAKO MAPYA UNAYOENDA KUYAANZA NYUMBANI. 
TUPO PAMOJA KAKA.
"USE YOUR TALENT WELL AND BE THE BEST YOU CAN BE,
THE BRIGHT FUTURE IS IN YOUR HAND IF YOU CAN SEE,
I WRITE THIS TO YOU TO SHOW YOU THAT I CARE,
AND ALSO AM GLAD THAT YOU WILL ALWAYS BE THERE," 
From Ally S. Mgido's CEO 24 SEVEN 365 (http://allyshams.blogspot.com).

NBC Yapiga Jeki Ujenzi Wa Jengo La Maabara La DUCE

Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, Robi Matiko-Simba (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya shs milioni 10 kwa Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Prof.  Salome Misana zilizotolewa na benki hiyo kusaidia ujenzi wa jengo la maabara la Shule ya Sekondari Chang’ombe inayomilikiwa na DUCE. Hafla ya makabidhiano ilifanyika chuoni hapo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katikati ni Mshauri wa Mambo ya Habari wa NBC, Redemptus Masanja (wa pili kushoto) na Naibu Mkuu wa Chuo Utawala, Prof. Bavo Nyichomba.
Mshauri wa Mambo ya Habari wa NBC, Redemptus Masanja (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya shs milioni 10 kwa Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Prof.  Salome Misana zilizotolewa na benki hiyo kusaidia ujenzi wa jengo la maabara la Shule ya Sekondari Chang’ombe inayomilikiwa na DUCE. Hafla ya makabidhiano ilifanyika chuoni hapo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katikati ni Meneja Mahusiano wa NBC, Robi Matiko-Simba (wa pili kushoto)  na Naibu Mkuu wa Chuo Utawala, Prof. Bavo Nyichomba.

  
Mshauri wa Mambo ya Habari wa NBC, Redemptus Masanja (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya shs milioni 10 kwa Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Prof. Bavo Nyichomba zilizotolewa na benki hiyo kusaidia ujenzi wa jengo la maabara la Shule ya Sekondari Chang’ombe inayomilikiwa na DUCE. Hafla ya makabidhiano ilifanyika chuoni hapo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katikati ni Meneja Mahusiano wa NBC, Robi Matiko-Simba (wa pili kushoto)  na Mkuu wa chuo hicho, Prof. Salome Misana.
 

Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, Robi Matiko-Simba (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya shs milioni 10 kwa Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Prof.  Salome Misana zilizotolewa na benki hiyo kusaidia ujenzi wa jengo la maabara la Shule ya Sekondari Chang’ombe inayomilikiwa na DUCE. Hafla ya makabidhiano ilifanyika chuoni hapo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.  
Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, Robi Matiko-Simba (wa pili kushoto waliokaa), Mshauri wa Mambo ya Habari wa NBC, Redemptus Masanja (kushoto waliokaa) Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Prof.  Salome Misana (kushoto kwa Robi) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu wa chuo hicho katika hafla ambayo NBC ilikabidhi hundi ya shs milioni 10 kusaidia ujenzi wa jengo la maabara la Shule ya Sekondari Chang’ombe inayomilikiwa na DUCE. Hafla ya makabidhiano ilifanyika chuoni hapo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

NA MWANDISHI WA NBC
BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC), imekabidhi hundi ya shs milioni 10 kuchangia ujenzi wa jengo la maabara ya Shule ya Sekondari Chango’ombe inayomilikiwa na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE).

Akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa chuo hicho, Prof. Salome Misana, Meneja Mahusiano wa NBC, Robi Matiko-Simba alisema msaada huo ni sehemu ya majukumu ya benki hiyo ndani ya mfuko wake wa kuisaidia jamii (CSR)

“ Kama NBC suala la elimu ni muhimu mno hususani kusaidia chuo kama DUCE kwani ubora wa elimu atakayopata mwalimu kwa sasa, mchango wake ni mkubwa sana katika ubora wa elimu watakayopata watoto watakaofundishwa na walimu hao,” alisema Bi. Robi.

Alisema ni kwa kuzingatia hilo hadi sasa Benki yas NBC imeshatumia zaidi ya shs bilioni 1.5 katika masuala ya elimu ikisaidia katiukia maeneo mbalimbali kama vile ujenzi wa madarasa, ununuaji wa madawati, vitabu, madaftari na vifaa vingine vya kufundishia.

Akipokea msaada huo Mkuu huyo wa DUCE, Prof. Salome Misana aliishukuru Benki ya NBC kwa kuunga mkono juhudi za chuo hicho katika kuboresha miundo mbinu ya chuo hicho katika jitihada zake za kuboresha masomo ya sayansi katika chuo hicho kilichoanzishwa mwaka 2005 ikiwa ni juhudi za serikali katika kupambana na tatizo la uhaba wa walimu na wataalamu wengine katika sekta ya elimu.

Alisema katika kuadhimisha miaka 50 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sambamba na miaka 50 ya Uhuru, DUCE pamoja na mambo mengine kiliazimia kuanzisha mchakato wa ujenzi wa jengo la maabara ya Shule yao ya Sekondari Chang’ombe wakiwa na kauli mbiu ya ‘Tuinue Sayansi na Teknolojia Mashuleni na Vyuoni kaka Chachu ya Maendeleo ya Kiuchumi Tanzania’.

Mkuu huyo wa DUCE alisema mchakato huo ulizinduliwa na rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal Septemba 13 huku makadirio ya ujenzi huo ukitegemewa kugharimu wastani wa shs bilioni 2.

Naye Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Bavo Nyichoma alisema mchango wa NBC ni muhimu sana katika jitihada zao za kuhakikisha ujenzi wa maabara ya shule hiyo zinafanikiwa kwani sanyansi ndio gurudumu la maendeleo.

“Nchi zote zilizoendelea ni kutokana na matunda ya wanasayansi wake na hata sisi ili tuweze kupata wanafunzi wazuri ni lazima tuwekeze kwa vitendo katika elimu ya sayansi,” alisema.

Chuo Kikuu cha DUCE kikiwa na wanafunzi 616 kati yao 382 wakichukua masomno ya sayansi hutumia Shule ya Sekondari Chang’ombe kama sehemu ya kufanya mazoezi ya ufundishaji kwa vitendo.
Na globalpublishers

HAPPY BIRTHDAY ALLY CHUNDA

Siku kama ya leo alizaliwa Mdau wa blog hii anaitwa ALLY M. CHUNDA JR., wa OSMANIA UNIVERSITY HYDERAD(SAINKPUR), Nchini INDIA.

Blogu hii inaungana na Familia yake, Ndugu, Jamaa na Marafiki wote katika kukutakia siku njema iliyo na Furaha, Amani na Upendo, na pia Mafanikio katika maisha yako.

Mwenyezi Mungu akujaalie Afya Njema,Maisha Marefu, Mafanikio, Busara na Hekima katika siku zote za maisha yako.
HAPPY BIRTHDAY ALLY CHUNDA!!

Saturday, October 29, 2011

Saif Gaddafi Asema Hana Hatia

Saif Gaddafi
Mkuu wa mashtaka wa Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa, ICC, anasema mtoto wa kiume wa Kanali Gaddafi, Saif al Islam, anajitetea kuwa hana makosa.
Saif Gaddafi amejificha, baada ya serikali ya baba yake kutolewa madarakani.
Luis Moreno-Ocampo anasema Saif, kwa kupitia wajumbe, amemwambia kuwa anataka kufutiwa mashtaka.
Luis Moreno-Ocampo anasema Saif Gaddafi amekuwa na hamu ya kutaka kujua hatima yake, endapo ICC itamkuta hana makosa.
Yeye anakanusha kuwa aliamrisha mashambulio ya mabomu na risasi dhidi ya waandamanaji mwezi wa Februari, wakati maandamano yalipoanza nchini Libya; na anasema anaweza kutoa ushahidi kuonesha kuwa hana hatia.
Mahakama ya ICC yamemshtaki Saif Gaddafi, hayati baba yake, Kanali Gaddafi, na mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi Abdullah al-Senussi, na uhalifu wa kivita.
Bwana Moreno-Ocampo anataka kumfikisha The Hague mtoto wa Kanali Gaddafi, ili kuanza kesi.
Anajua kuwa Saif anajaribu kuchunguza yanayomkabili, pamoja na kuzungumza na nchi chache ambazo zinaweza kumpa hifadhi na askari mamluki wanaoweza kumpeleka huko.
Chanzo BBC SWAHILI

Familia ya Bw Alhaj Abdul Risasi wa Kawe jijini Dar es Salaam inatangaza kupotelewa na mtoto wao Hussein Risasi (15)

Mtoto wao Hussein Risasi (15) 
---
Familia ya Bw Alhaj Abdul Risasi wa Kawe jijini Dar es Salaam inatangaza kupotelewa na mtoto wao Hussein Risasi (15) anayesoma shule ya Msingi Olympio iliyopo Upanga Jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Alhaj Risasi ni kwamba Hussein alitoweka nyumbani kwao Kawe jijini Dar es Salaam Ocktoba 25 mwaka huu mara baada ya kurejea akitokea shuleni.
Kabla ya tukio hilo Hussein alianza utoro wa kwenda shule kwa madai kwamba amekuwa haelewi anachofundishwa na walimu wake na kwamba wanafunzi wenzake wamekuwa wakimcheka  kitendo ambacho hakukipenda.
Akifafanua  zaidi Alhaj Risasi amesema kuwa, kutokana na tabia hiyo ya utoro aliyoianza Hussein ambaye ni pacha na Hassan Risasi anayesoma Nairobi, alimwita na kumkanya kutokana na vitendo hivyo.
Hussein amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya athma tangu utoto wake jambo linaloathiri pia afya yake mara kwa mara.
Kwa yeyote atakayemuona anaombwa kutoa taarifa kituo chochote cha Polisi nchini au kupitia namba za simu 
  0715  611 277, 
    0713  314  442   
0787 377 822.

Twiga Bank yashiriki kikamilifu maonesho ya Wizara ya Fedha

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Twiga, Hussein Mbululo akiwaonesha waandishi wa Habari Nishani ya Ulezi Bora wa Vikoba  iliyotunukiwa Benki ya Twiga kwa kuwawezesha wajasiriamali wadogo nchini. Mbululo alikuwa akiionesha wakati Benki hiyo wakati wa 
Maonesho ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na kushirikisha taasisi zake zote. Maonesho hayo yanafanyika katika viwanja vya Manazi Mmoja jijini Dar es Salaam
Ofisa Masoko wa Twiga Bank, Adelbert Archard  akitoa akiwagawia wanafunzi vipeperushi na kuwapa maelezo juu ya Akaunti maalum ya Akiba kwa watoto , walipotembelea banda la Benki hiyo wakati wa Maonesho ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru yaliyoandaliwa na Wizara yaFedha na kushirikisha taasisi zake zote. Maonesho hayo yanafanyika katika viwanja vya Manazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Twiga, Hussein Mbululo (kulia) akismsikiliza  na Naibu Waziri wa Fedha, Pereira Silima wakati alipotembelea banda la benki ya Twiga wakati wa Maonesho ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na kushirikisha 
taasisi zake zote. Maonesho hayo yanafanyika katika viwanja vya Manazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Laston Msongole na Wapili kulia ni Ofisa Habari wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Twiga, Hussein Mbululo  akizungumza na waandishi wa Habari juu ya huduma zitolewazo na Benki hiyo wakati wa Maonesho ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na kushirikisha taasisi zake zote. Maonesho hayo yanafanyika katika viwanja vya Manazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Na Father Kidevu.

Friday, October 28, 2011

AMAZING FACTS ABOUT GADDAFI

Muammar Abu Minyar al-Gaddafi.
1. There is *no electricity bill* in Libya; electricity is free for all its citizens.
2. There is *no interest on loans*, banks in Libya are state-owned and loans given to all its citizens at 0% interest by law.
3. *Home* considered a human right in Libya – Gaddafi vowed that his parents would not get a house until everyone in Libya had a home. Gaddafi’s father has died while him, his wife and his mother are still living in a tent.
4. All newlyweds in Libya receive *$60,000 Dinar* (US$50,000) by the government to buy their first apartment so to help start up the family.
5. Education and medical treatments are free in Libya. Before Gaddafi only 25% of Libyans are literate. Today the figure is 83%.
6. Should Libyans want to take up *farming* career, they would receive farming land, a farming house, equipments, seeds and livestock to kick-start their farms – all for free.
7. If Libyans cannot find the education or medical facilities they need in Libya, the government funds them to *go abroad* for it – not only free but they get US$2,300/mth accommodation and carallowance.
8. In Libyan, if a Libyan buys a *car*, the government subsidized 50% of the price.
9. The price of *petrol* in Libya is $0.14 per liter.
10. Libya has *no external debt* and its reserves amount to $150 billion – now frozen globally.
11. If a Libyan is unable to get *employment* after graduation the state would pay the average salary of the profession as if he or she is employed until employment is found.
12. A portion of Libyan *oil sale* is, credited directly to the bank accounts of all Libyan citizens.
13. A mother who *gave birth* to a child receive US$5,000
14. 40 loaves of *bread* in Libya costs $ 0.15
15. 25% of Libyans have a *university degree*
16. Gaddafi carried out the world’s largest *irrigation* project, known as the Great Man-Made River project, to make water readily available throughout the desert country.

Ibada ya Maziko ya Mabaki ya Miili 12 iliyoteketea Kwa Moto Katika Ajali ya Basi la Deluxe

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza akizungumza wakati wa ibada ya maziko ya mabaki ya miili 12 iliyoteketea kwa moto katika ajali ya basi la Deluxe iliyotokea Kibaha mkoani humo wiki hii.Picha na Yusuph Badi

KONGAMANO LA WAHAHABARI LA BIMA YA AFYA LAFANYIKA MKOANI MOROGORO

Mwandishi wa Habari, Joshua Joel akifafanua jambo alipokuwa akitoa katika kongamano hilo taarifa ya utafiti wa upatikanaji wa huduma za afya zitolewazo na NHIF, katika mikoa ya Rukwa na Katavi.
Mwandishi wa habari mwandamizi wa gazeti la Jambo Leo, Grace Michael akitoa taarifa ya utafiti wa huduma za afya zilitolewazo na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), katika Mkoa wa Kigoma.
Beda Msimbe wa magazeti ya Serikali ya Daily News na Habari Leo, akitoa taarifa ya utafiti wa huduma zitolewazo na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), katika Mkoa wa Ruvuma.
Said Mmanga kutoka gazeti la Changamoto, akitoa taari ya utafiti kuhusu upatikanaji wa huduma za afya vijijini walioufanya na Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV, George Marato katika Mkoa wa Mara.
Baadhi ya wahariri wa habari na waandishi waandamizi  wakiwa katika kongamano la saba la mwaka la kujadili taarifa za utafiti wa huduma za NHIF nchini, lililoanza jana mjini Morogoro.
Wachora vibonzo Nathan Mpangala (kulia) na King Kinya wakisikiliza kwa makini wakati wa kongamano likiendelea.
 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (kulia) akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Emmanuel Humba (kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya mfuko huo, Ally Kiwenge (wa pili kushoto) baada ya kufungua kongamano la saba la mwaka la wahariri wa habari na waandishi waandamizi la kujadili taarifa za  utafiti wa huduma za NHIF nchini. Kongamano hilo la siku mbili lilianza jana mjini Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (kulia), akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari,baada  ya kufungua kongamano la saba la mwaka la wahariri wa habari na waandishi waandamizi la kujadili  taarifa za utafiti wa huduma za NHIF nchini. Kongamano hilo la siku mbili lilianza jana mjini Morogoro.