SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, October 28, 2011

KONGAMANO LA WAHAHABARI LA BIMA YA AFYA LAFANYIKA MKOANI MOROGORO

Mwandishi wa Habari, Joshua Joel akifafanua jambo alipokuwa akitoa katika kongamano hilo taarifa ya utafiti wa upatikanaji wa huduma za afya zitolewazo na NHIF, katika mikoa ya Rukwa na Katavi.
Mwandishi wa habari mwandamizi wa gazeti la Jambo Leo, Grace Michael akitoa taarifa ya utafiti wa huduma za afya zilitolewazo na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), katika Mkoa wa Kigoma.
Beda Msimbe wa magazeti ya Serikali ya Daily News na Habari Leo, akitoa taarifa ya utafiti wa huduma zitolewazo na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), katika Mkoa wa Ruvuma.
Said Mmanga kutoka gazeti la Changamoto, akitoa taari ya utafiti kuhusu upatikanaji wa huduma za afya vijijini walioufanya na Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV, George Marato katika Mkoa wa Mara.
Baadhi ya wahariri wa habari na waandishi waandamizi  wakiwa katika kongamano la saba la mwaka la kujadili taarifa za utafiti wa huduma za NHIF nchini, lililoanza jana mjini Morogoro.
Wachora vibonzo Nathan Mpangala (kulia) na King Kinya wakisikiliza kwa makini wakati wa kongamano likiendelea.
 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (kulia) akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Emmanuel Humba (kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya mfuko huo, Ally Kiwenge (wa pili kushoto) baada ya kufungua kongamano la saba la mwaka la wahariri wa habari na waandishi waandamizi la kujadili taarifa za  utafiti wa huduma za NHIF nchini. Kongamano hilo la siku mbili lilianza jana mjini Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (kulia), akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari,baada  ya kufungua kongamano la saba la mwaka la wahariri wa habari na waandishi waandamizi la kujadili  taarifa za utafiti wa huduma za NHIF nchini. Kongamano hilo la siku mbili lilianza jana mjini Morogoro.

0 comments:

Post a Comment