Mkutano Wa Siku Tatu Wa Uwazi Na Uwajibikaji Katika Bajeti Kwa
Nchi Za Afrika Mashariki
Mdhibiti
na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali Ludovick Utouh akizungumza na
waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa ukaguzi wa
mahesabu katika mashirika ya umma na umuhimu wa uawajibikazi kwa
wananchi na ushirikishwaji wa taasisi mbali mbali katika kuandaa
bajeti. Utouh alisema kuwa anaridhishwa na jinsi serikali
inavyoshughulikia mapendekezo yake juu ya masuala mbali mbali
yanayohusiana na uthibiti na ukaguzi wa hesabu.
Waziri
wa Afrika Mashariki Samweli Sitta akifafanua jambo kwa waandishi wa
habari katika ukumbi wa Ubungo Plazza kuhusu umuhimu wa Serikali za
Afrika Mahariki kuwa wazi kwa wanachi kuhusu bajeti zake na mipango
endelevu ya bajeti hizo katika kupigana na umaskini wa kipato.Sita
alisema kuwa Tanzania ni nchi inayofanya vizuri miongoni mwa nchi za
Afrika Mshariki katika uwazi na uwajibikaji wa mahesabu ya Serikali kwa
wananchi wake.
Mbunge wa Bariadi Magharibi Andrew Chenge akiwa katika mkutano huo.
Mwenyekiti
wa kamati ya Bunge ya Fedha na uchumi Abdal Kigoda akitoa mada juu
umuhimu wa uwazi na uwajibika katika bajeti za serikali.
Baadhi
ya washiriki wa mkutano wa Uwazi na uwajibikaji wa mahesabu ya
Serikali za nchi za Afrika Mashariki. Mkutano huo ni wa siku tatu,
unatarajiwa kufungwa mei 25 na umewajumuisha wawakilishi kutoka tasisi
mabali mbali wakiwemo Wabunge, Wenyeviti na wajumbe wa kamati za Fedha
za Bunge, wawakilishi kutoka Benki ya Dunia, wadau wa mashirika ya
Maendeleo, Wahisani na Waandishi wa habari.
Mgeni
rasmi katika mkutano wa siku 3 wa kujadili uwazi na uwajibikaji katika
bajeti kwa nchi za Afrika Mashariki ambae pia ni Waziri wa Afrika
Mashariki Samweli Sitta wa tatu kulia akijadili jambo na Mdhibiti na
mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali Ludovick Utouh. Wengine ni
Mwenyeketi wa kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi Abdalah Kigoda wa
kwanza kulia, Mbunge wa Bariadi na mwenyeketi wa kamati ya Bunge ya
Hesabu Za Serikali John Cheyo wa pili kulia wakiwa katika mkutano wa
siku tatu wa kujadili uwazi na uwajibikaji katika bajeti za nchi za
Afrika Mashariki juzi asubuhi katika ukumbi wa Ubungo Plazza.
0 comments:
Post a Comment