SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, May 20, 2011

BREAKING NEWS….. SHEIKH YAHYA HUSSEIN AMEFARIKI DUNIA!!!

Sheikhe Yahya Hussein 
Mtabiri maarufu wa mambo ya Nyota afrika mashariki na Kati Sheikhe Yahya Hussein Amefariki dunia Leo baada ya kuugua kwa muda mrefu.  
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospital ya Lugalo. kwa taarifa zaidi kuhusiana na Msiba wake.
 Mtabiri maarufu ndani na nje ya Tanzania, Sheikh Yahya Hussein leo asubuhi amefariki kutokana na tatizo la ugonjwa wa moyo baada ya  kukimbizwa Hospitali ya Ukombozi, Kinondoni, jijini 
Dar es Salaam leo asubuhi na  ilipotimu saa tatu asubuhi alikataka roho akiwa hospitalini hapo.
Kwa mujibu wa mtoto mkubwa wa marehemu aitwaye Hassan, alisema kuwa kesho mwili wa baba yake utaswaliwa katika msikiti wa Tambaza, na atazikwa saa saba mchana kwenye makaburi ya Tambaza jijini Dar es Salaam.
Sheikh Yahya Hussein alizaliwa mwaka 1932 wilayani Bagamoyo na kupata elimu yake ya awali katika shule ya Al-Hassanain Muslim ya Dar es Salaam na baada ya hapo alijiunga na Chuo cha Muslim Academy kilichopo Zanzibar.
Baada ya hapo Sheikh Yahya Hussein alikwenda nchini Misri na kujiunga na Chuo Kikuu cha Al-Azhar kilichopo Cairo na kuendelea na masomo ya dini, na alirejea Tanzania mapema miaka ya 60 na kuanza kazi ya utabiri wa nyota.
Blog hii inatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki, wananchi wote wa Tanzania kutokana na msiba huu mkubwa.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu awape nguvu na ujasiri wanafamilia yake katika kipindi hiki kugumu cha kuomboleza hadi kuzikwa kwa mwenzetu Sheikhe Yahya Hussein.
Na habari zaidi tutawaletea hapa hapa endelea kuwa nasi na utafahamu zaidi.
INNAH LILAHI WAINNA ILAHI RAJ UN, 
(SISI SOTE NI WAJA WA MWENYEZI MUNGU NA KWAKE TUTAREJEA).
MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI- AMEN.   

1 comments:

Anonymous said...

INNAH LILAHI WAINNA ILAHI RAJ UN (SISI SOTE NI WAJA WA MWENYEZI MUNGU NA KWAKE TUTAREJEA)

Nimepokea kwa mshituko taarifa ya Kifo cha Sheikhe Yahya Hussein. Namwomba Mwenyeezi Mungu amlaze mahala pema peponi. na kuwaombea wafiwa ALLAH AWAPE SUBIRA NA NGUVU KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU CHA MAOMBOLEZO. AMINA!

BI. SAUDA

Post a Comment