Wanachuo wa Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda wamefanya maandamano kupinga pendekezo la kuongezeka kwa ada ya chuo kutoka shilingi milioni 3 hadi shilingi milioni 6 kwa mwanachuo mmoja kwa mwaka.
Mgomo huo umekuja saa chache baada ya utawala wa chuo hicho kutangaza kuwa pendekezo hilo liko tayari likisubiri hatua za mwisho za majadiliano.
Polisi walilazimika kufyatua mabomu ya machozi kutawanya wanachuo hao walikuwa wakichoma moto vibanda vya simu katika maeneo ya maktaba kuu ya chuo hicho, kitivo cha sayansi, jingo ya seneti na maeneo mengineyo.
Polisi pia ilibidi kuwazuia wanachuo hao kutoenda kufanya maandamano hayo nje ya eneo la chuo ambako wangeharibu mali nyingi zaidi.
Baadhi ya wanafunzi waliokuwa wakinywa pombe waliwashambulia polisi kwa kuwarushia mawe na fimbo huku wakiimba, wakati wengine walibeba matawi ya miti na kuweka vizuizi katika barabara za chuoni hapo, kuvunja vioski na kupora bidhaa zilizokuwemo.
Wanachuo hao pia waliteka gari la kubebea wagonjwa la Chama cha Msalaba Mwekundu na kuliendesha kuzunguka maeneo ya chuo, huku wengine wakivamia chumba cha maonyesho cha kitivo cha teknolojia na sayansi ya chakula na kupora vyakula na vinywaji vilivyokuwepo kwa ajili ya maonesho.
Na.MO BLOG TEAM.

0 comments:
Post a Comment