SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, April 16, 2011

Ubalozi wa Marekani Watangaza Utaratibu Mpya Wa Kuomba Viza


Ubalozi wa Marekani nchini, umetangaza kuanzisha utaratibu mpya utakaorahisisha na kuongeza ufanisi katika kushughulikia maombi ya viza za kwenda nchini humo, kuanzia leo.
Kwa mujibu wa utaratibu huo, waombaji wataweza kuchagua miadi kwa ajili ya viza za muda mfupi kupitia tovuti mpya ya http://tanzania.usvisa-info.com.

Au kwa kupitia msaada kwa kupiga namba ya kituo cha huduma za wateja +255-22-2194300 begin_of_the_skype_highlighting +255-22-2194300 end_of_the_skype_highlighting begin_of_the_skype_highlighting +255-22-2194300 end_of_the_skype_highlighting ( kwa Tanzania), au +1-703-439-2304 begin_of_the_skype_highlighting +1-703-439-2304 end_of_the_skype_highlighting begin_of_the_skype_highlighting +1-703-439-2304 end_of_the_skype_highlighting (kwa Marekani), au kwa kupitia huduma ya Skype ID: usvisatanzania.
“Waombaji watalazimika kufanya malipo ya visa kupitia huduma ya Airtel Money (ZAP) au Citibank Tanzania Limited iliyopo Peugeot House, 36 Upanga Road, Dar es Salaam) kabla ya kufanya miadi (Appointment),” ilieleza sehemu ya taarifa ya Ubalozi huo iliyotumwa kwa vyombo vya habari kupitia mtandao wa kompyuta jana.
Mchakato huo mpya unasimamiwa na CSC visa information Services, unategemewa kuleta ufanisi na kurahisisha hatua za uombaji wa viza.
Kupitia mchakato huo, wasafiri watalazimika kuuliza habari zote zinazohusu aina zote za viza, mahitaji na hatua zake muda wowote kupitia tovuti: http://tanzania.usvisa-info.com.
Au kwa kupiga simu muda wa saa 2.00 asubuhi-saa 12.00 jioni, kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa kupitia namba +255-22-2194300 begin_of_the_skype_highlighting +255-22-2194300 end_of_the_skype_highlighting begin_of_the_skype_highlighting +255-22-2194300 end_of_the_skype_highlighting ( kwa Tanzania), au +1-703-439-2304 begin_of_the_skype_highlighting +1-703-439-2304 end_of_the_skype_highlighting begin_of_the_skype_highlighting +1-703-439-2304 end_of_the_skype_highlighting (kwa Marekani), au kupitia Skype ID: usvisatanzania. Huduma zote zitapatikana na kutolewa kwa lugha ya Kingereza tu.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

Post a Comment