Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ujumbe maalum wa Rais wa Somalia ulioletwa Ikulu jijini Dar es Salaam na Mjumbe maalum wa Rais huyo Bwana Mursal Saney ambaye pia ni Mkuu wa Itifaki wa Somalia. Baadaye mjumbe huyo alifanya mazungumzo mafupi na Rais Kikwete.
(Picha na Freddy Maro)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatano, Aprili 6, 2011, amepokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Somalia, Mheshimiwa Sheikh Sharif Sheikh Ahmed.
Ujumbe huo maalum wa Kiongozi wa Somalia umewasilishwa kwa Rais Kikwete na Bwana Musal Saney ambaye ni Mkuu wa Itifaki wa Somalia na Mjumbe Maalum wa Rais wa Somalia.
Mara baada ya kuwa amewasilisha ujumbe huo maalum, viongozi hao wawili wamefanya mazungumzo kuhusu hali ya Somalia na hali ya uhusiano kati ya nchi hiyo na Tanzania.
Mwisho.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
06 Aprili, 2011
Na Mo Blog.

0 comments:
Post a Comment