Ambilikile Mwaisapile(Maarufu BABU)
Na Mwandishi Wetu,
Loliondo Tiba ya kikombe inayotolewa na Mchungaji Mstaafu wa KKKT, Ambilikile Masapile ‘Babu’ imeendelea kubeba maajabu kila kukicha. Risasi Jumamosi kupitia uchunguzi wake, limebaini matukio 10 ya miujiza ambayo yametokea Loliondo tangu Babu alivyoanza kutoa tiba hiyo.
Tathmini ya gazeti hili, inaweka matukio hayo kwa mtiririko wa namba kulingana na ukubwa wake kama ifuatavyo;
1. MGONJWA KUTAPIKA NYOKA
Tukio la mgonjwa aliyetapika nyoka, limeweka rekodi ya aina yake, hivyo kuongoza miujiza hiyo. Wiki iliyopita, gazeti hili liliripoti tukio la mgonjwa aliyefika kwa Babu kwa lengo la kutibiwa lakini akatapika nyoka baada ya kupata kikombe. Ilielezwa kuwa, nyoka huyo aliwekwa tumboni mwa mgonjwa huyo kwa njia za kishirikina.
2. KUZAA NYAMA Tukio la pili ambalo linabeba miujiza kwa Babu ni lile la mgonjwa aliyekwenda kwa matatizo ya uzazi, matokeo yake akajifungua kipande cha nyama baada ya kupata kikombe. Ilielezwa kuwa, mwanamke huyo (jina lake halikufahamika) baada ya kupata kikombe, alihisi tumbo kuvimba, baadaye kushikwa uchungu wa uzazi, akajifungua kipande hicho cha nyama chenye uzani wa kilo mbili. Taarifa iliyotolewa baadaye ni kuwa mwanamke huyo alikuwa amefungwa uzazi kwa njia za kishirikina.
3. KIZAAZAA CHA POCHI
Pochi ya Mkenya iliyoibwa Loliondo ikiwa na hati ya kusafiria na fedha za Kenya Shilingi 20,000 (zaidi ya shilingi 356,000) iliibua kizaazaa na kuwa moja kati ya maajabu 10 ya Babu. Ilielezwa kuwa, baada ya Mkenya huyo kuibiwa na taarifa kuenea, Babu alitoa agizo kwa aliyeiba kurejesha pochi hiyo, vinginevyo angechapwa na Mungu. Baada ya agizo hilo, mhusika aligoma kurudisha pochi lakini dakika kadhaa zilizofuata, kijana mmoja alianza kulalamika anachapwa fimbo na mtu asiyejulikana, huku akijitaja kwamba yeye ndiye aliyeiba.
4. WALIOUA NYOKA WAKIONA
Tukio lingine la maajabu lilitokana na mtu aliyetapika nyoka. Habari zinasema kuwa baada ya mtu huyo kutapika nyoka, Babu aliagiza ‘mdudu’ huyo asifanywe chochote mpaka aondoke mwenyewe. Hata hivyo, baadhi ya watu walikosa uvumilivu, kwa hiyo walimpiga nyoka huyo mpaka akafa. Saa chache baada ya nyoka kuuawa, wauaji walianza kuugua, huku wakilalamika kuchomwa chomwa mwilini na vitu visivyoonekana. Watu hao, baadaye walipelekwa kwa Babu ambaye aliwaombea wakapona lakini aliwapa sharti la kuzingatia anachoagiza.
5. MZIMU KWENYE DAWA
Tukio lingine la ajabu kwenye himaya ya Babu ni lile la mzimu ulioonekana kwenye foleni. Mwanamuziki zao la Bongo Star Search (BSS), Baby Madaha ambaye alikwenda Loliondo kupata kikombe alisema kuwa, aliishuhudia mzimu wakati akisubiri zamu yake. Baby alisema kuwa, awali alidhani mzimu huo ni mtu wa kawaida, lakini watu wakamwambia siyo na kufumba na kufumbua ulitoweka. Baadaye alielezwa kuwa ule ni mzimu na kufafanuliwa kwamba kwenye himaya ya Babu Ambi kuna miujiza mingi.
6. KUPONA KABLA YA KIKOMBE
Kuwepo kwa watu ambao wametoa ushuhuda wa kupona kabla ya kupata kikombe ni maajabu mengine ya Babu. Imeelezwa kuwa, watu hao ambao hutoka nyumbani kwao wakiwa wagonjwa, hupona wakiwa kwenye foleni, hivyo hunywa kikombe ili kukamilisha safari yao ya tiba. Janette Ismida wa Morogoro alilithibitishia gazeti hili wiki iliyopita kwamba, alipona kwenye foleni, alisema: “Nafikiri imani ndiyo inaponya. Mimi nilikuwa na kiharusi, mdomo wangu ulikuwa umepinda. “Nikiwa kwenye foleni nilishangaa nashikwa na baridi kali, nikaona maruweruwe. Kikafuata kigiza fulani hivi wakati ni mchana. Baada ya hapo nikapona, nikawa naweza kuongea, kwa hiyo nilikunywa kikombe kukamilisha tu.”
7. MAPEPO YALIPUKA
Tukio lingine la ajabu ni lile la wanawake mbalimbali kulipuka mapepo wakiwa hatua chache kumfikia Babu, wakiwepo walokole. Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa, huwa haipiti siku bila wanawake wasiopungua 10 kulipuka mapepo na kuzungumza vitu vya ajabu kwa lugha mbalimbali duniani.
8. VIBWEKA VYA WACHAWI
Gazeti hili lilielezwa na mmoja wa wasaidizi wa Babu kuwa, wachawi wamekuwa wakifika Loliondo kufanya vitendo vya kumjaribu mchungaji huyo lakini siku zote wameshindwa. “Wachawi wanamfikia sana Babu, lengo lao ni kuona nguvu zake lakini kwa taarifa ni kuwa hawamuwezi, ” alisema mmoja wa wasaidizi wa Babu aliyeomba hifadhi ya jina lake gazetini.
9. WANAOMUIGA WAKOSA MVUTO
Tangu Babu Ambi aibuke Loliondo, watu mbalimbali wamekuwa wakitoa ushuhuda wa kufunuliwa kwenye ndoto utabibu wa njia ya kikombe. Hata hivyo, kwa kile kinachoonekana ni nguvu ya Babu, wote waliojitangaza wamekosa mvuto, hivyo Loliondo imebaki kuwa kimbilio kuu la wagonjwa wenye maradhi sugu. Watu ambao wamejitangaza kutoa tiba hiyo mpaka sasa ni Fatma Said Sengo ‘Bibi’ wa Morogoro, Margaret Mutalemwa ‘Dada’ wa TaboLinkra wakati Mbeya kuna kijana, Jafar Welino ‘Kaka’.
10. KICHAA CHA BIBI KIZEE
Tukio la 10 la ajabu ambalo lilichukua nafasi Loliondo ni la bibi kizee (jina tunalo) ambaye alipelekwa kupata tiba ya kikombe. Bibi huyo baada ya kunywa dawa, alipona ghafla wakati kwa miaka mingi alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kurukwa akili. Kwa mujibu wa ndugu aliyeongozana naye, bibi huyo alirukwa akili kwa zaidi ya miaka Link30, hivyo walimpeleka kwa Babu Ambi kama kubahatisha. “Mungu mkubwa sana, hatukutegemea. Alipokunywa tu kikombe alishangaa amefikaje pale, halafu akaomba apewe maji aoge kwa sababu alikuwa mLinkchafu,” alisema ndugu huyo.
CHANZO: http://www.globalpublishers.info/

0 comments:
Post a Comment