SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, March 31, 2011

BREAKING NEWZI!!!

Bi. Fatma Senga
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu akizungumza jambo baada ya kutembelea eneo hilo la Kichangani na kuzungumza na Mama Fatma juu ya tiba yake na kumpa mwongozo wa kufanya shughjuli hiyo bila kuleta usumbufu wala madhara kwake na jamii
itakayotumia tiba hiyo.
Mwambungu aliambatana na viongozi kadha wa ofisi yake baada ya kupata taarifa ya kuwapo kwa KIKOMBE katika Wilaya yake.
Hivi ndo Vikombe, Glasi na Bilauri zinazotumika kugawa dozi ya kutibu magonjwa mbalimbali yakiwapo yale sugu yaliyoshindikana kwa dawa za kisomi.
Mkazi wa Kichangani ndani ya Manispaa ya mji Kasoro Bahari Morogoro, Fatma Senga ambaye nae amefuata nyayo za babu wa Loliondo, Kaka wa Mbeya , Dada wa Tabora na hivi sasa ni yeye Mama wa Kichangani Morogoro anayetoa dozi ya kipimo cha kikombe/Glasi.
Huyu yeye hana kipimo maalum na vikombe vyake kwa jinsi vilivyoonekana ni vile vidogo vya Chai na Bilauri za bati.
Mama huyu nadai kuoteshwa na Mungu usiku wa kuamkia Machi 30 na leo ameanza kugawa dozi hiyo kwa gharama za sh. 200 tu kwa kipimo.
Mapema leo Mkuu wa Wilaya ya ya Morogoro, Said Mwambungu pamoja na maofisa wa wilaya akiwepo Mkaganga Mkuu wa Wilaya walifika nyumbani kwa mama huyo na kumwomba daktari achukue sampuli ya dawa hiyo kwa uchunguzi kujua usalama wake.
Zaidi ya watu 200 wanasadikiwa kupata huduma hiyo kwa siku mbili zilizopita.
Aidha Mama fatma yeye alikuwa ni mtoa tiba M'badala tangu mwanzoni mwa miaka ya tisini hadi hapo alipoooteshwa na Mungu.
Haya Watanzania huenda ndo yale mambo ya unabii yanayo semwa katika vitabu vitakatifu kuwa nyakati za mwisho.

Waziri Wa Libya Ahojiwa Uingereza

Waziri wa mambo ya nje wa Libya Mousaa Koussa
Waziri wa mambo ya nje wa Libya Mousaa Koussa amekuwa akihojiwa na maafisa baada ya kuwasili Uingereza bila kutarajiwa siku ya Jumatano.
Alitokea Tunisia. Ofisi ya Uingereza ya mambo ya nje ilisema "hakuwa na nia tena" ya kufanya kazi na Kanali Gaddafi.
Hata hivyo msemaji wa Libya alikana kwamba Bw Koussa ameasi na kwamba alikuwa katika safari ya kidiplomasia.
Kuwasili kwake Uingereza kumefanyika huku waasi wa Libya wakiwa wamerudi nyuma kwenye miji iliyotekwa hivi karibuni katika pwani ya mashariki.
Kurudi nyuma kwa waasi kulitokana na mapigano makali baina ya Brega na Ajdabiya siku ya Alhamisi.
Awali waasi hao walishapoteza bandari muhimu ya mafuta ya Ras Lanuf na mji mwengine ulio karibu wa Bin Jawad.
Upande wa magharibi, mji ulioshikiliwa na waasi wa Misrata bado unaripotiwa kushambuliwa na majeshi ya wanaomtii Kanali Gaddafi.
Chanzo: BBC SWAHILI

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO SAYANSI NA TEKNOLOJIA ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA ZANTEL

Ofisa Mkuu wa Tekenorojia Kampuni ya Zantel Bw. Moncef Mettiji wa pili (kulia) akimuonesha moja ya mitambo ya mawasiliano ya Kampuni hiyo Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Bw. Charles Kitwanga alipotembelea kampuni hiyo Dar es salaam Kuliani Ofisa Mtendaji Mkuu Ali Bin Jarsh na kushoto ni Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa wa Zantel Norman Moyo.
(PICHA NA MPIGA PICHA WETU)Link

CHEKA ULINGONI NA BONDIA BORA DUNIANI

Kimbau akielezea mpambano huo, Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar es Salaam.
AFISA Uhusiano wa Kampuni ya Aurora Group Companies, Shomari Kimbau, leo ametangaza mpambano wa ngumi unaotambuliwa kimataifa na IBF kati ya bondia Francis Cheka wa hapa nchini anayeshikilia nafasi ya 134 kwa ubora duniani, na Marcus Upshaw wa Marekani ambaye anashika nafasi ya 36 kwa ubora duniani na nafasi ya 6 nchini Marekani.
Kimbau amesema mpambano huo utafanyika ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, Mei 1 mwaka huu ambapo refarii na wasimamizi wengine watatoka nchi mbalimbali. Kimbau aliongeza kwamba endapo Cheka atashinda pambano hilo linalotambulika kimataifa atapanda kutoka nafasi ya 134 duniani aliyopo sasa.
NA RICHARD BUKOS /GPL

India Beat Pakistan To Storm Into Final

MOHALI: India kept alive a billion dreams after sinking Pakistan by 29 runs in their World Cup semi-final on Wednesday to set up an all-Asian final against Sri Lanka.

MIUJIZA YA KIKOMBE CHA DADA MAGE WA TABORA INAENDELEA!!

Ndani ya uzio wanaruhusiwa kuingia watu 10 kwa mara moja.
Leo ikiwa ni takriban siku kumi tangu Dada Mage aaanze kutibu wagonjwa kwa tiba anayodai kuwa kapewa na uwezo huo na Mwenyezi Mungu, Mtaa huo wa Urban Quarter umeanza kuwa maarufu hasa baada ya wachuuzi wa vyakula vya kila aina kuanza kutoa huduma hapo. Kama uonavyo leo pana takriban watu 2000 hivi ukifananisha na jana ambapo palikuwa 500 hivi.
BOFYA HAPA

USAFIRI WA HUU DAH!!!

Hivi hapa ikitokea ajali nani alaumiwe abiria au mmiliki wa chombo!!??
Hapo vipi mnasemaje wadau?.

Wednesday, March 30, 2011

WAZIRI MKUU AFUNGUA MKUTANO WA REPOA

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti Kuhusu Kuondoa Umaskini (REPOA) Profesa Esther Mwaikambo (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA Profesa Samweli Wangwe baada ya kufungua mkutano wa Taasisi hiyo kwenye hoteli ya Whitesands jijini Dar es salaam Machi 30,2011.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

GBAGBO ATAKA MAPIGANO YASITISHWE IVORY COAST

Bw. Laurent Gbagbo
Vikosi vinavyomuunga mkono Alassane Ouatarra anayetambuliwa na Jumuiya ya Kimataifa kuwa rais halali wa Ivory Coast kwa sasa vinaidhibiti miji miengine minne muhimu. Kwa mujibu wa msemaji wa kiongozi anayeng’ang’ania madaraka nchini humo Laurent Gbagbo aliyehojiwa na kituo cha Radio ya Ufaransa cha RFI, kambi yao inatoa wito wa kusitisha mapigano kwa kuwa wanaelekea kushindwa. Hata hivyo kambi ya Outarra imesema kuwa muda umeshapita wa kutafuta suluhu ya amani au kugawana madaraka. Laurent Gbagbo amekuwa akiendelea kung’ang’ania madaraka hata baada ya Jumuiya ya Kimataifa kumtambua Alassane Ouattara kama mshindi halali wa awamu ya pili ya uchaguzi wa rais uliofanyika mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka jana.

Tuesday, March 29, 2011

Beyonce Drops Dad As Her Manager

Beyonce
Mathew Knowles
Beyonce has parted ways with her father - Mathew Knowles will no longer manage his daughter's phenomenally successful career.
The patriarch resigned from his sales job in 1995 to take care of the star's singing aspirations, helping to launch her career with hit girl-group Destiny's Child.
Knowles also managed his daughter's bandmates Kelly Rowland and Michelle Williams, but Rowland ditched him as her manager in 2009, and Williams followed suit a year later.
Now, the Crazy In Love hit-maker has also decided to end her business arrangement with her dad - but she maintains their personal relationship is still intact.
In a statement, the singer's spokesperson, Yvette Noel-Schure, reveals Beyonce has parted from her father "on a business level," while Beyonce adds that "he is my father for life and I love my dad dearly."

MTANZANIA ANAYEPIGA SOKA CHELSEA

Mchezaji wa Chelsea, Adam Nditi akiwa uwanjani na timu yake wakati wa mechi ya Kombe la FA kwa vijana kati ya Chelsea na Arsenal mchezo uliopigwa katika uwanja wa Stamford Bridge Januari 20, 2011 mjini London, England. Picha kwa hisani ya Zimbio.
Bofya Hapa

WADAU WA HYDERABAD HAPO NI WAPI???

Picha hii imetumwa na mdau mmoja toka hapa Hyderabad, unaweza tambua eneo/sehemu hii!!.

Three Held For Hacking Bank Accounts-India New Delhi

map of india
New Delhi, Three people have been arrested for hacking at least 14 bank accounts of Rs.8 lakh to pay around 150 people's electricity bills, police said Monday.
'Anil Jain, Suresh Khandelwal and Rakesh Roshan were held Sunday from Gandhi Nagar area in east Delhi,' said Deputy Commissioner of Police O.P. Mishra. Another member of the gang, Pritam Mishra, is absconding.
The three were held after HDFC Bank registered a complaint that a few people had fraudulently acquired data of customers and made some unauthorised payments of electricity bills and other payments through internet banking.
During investigations, police found that that someone had obtained the data of account holders by phishing, or fraudulently obtaining secret details through a fake website resembling the original.
During interrogation, the three accused were found to paid bills from the bank accounts they had hacked.
'Around Rs.8 lakh was withdrawn from 14 customers of the bank to deposited bills of about 150 consumers. The gang has also duped the customers of other banks by depositing the bills and other payments of recharging of mobile phones,' added Mishra.
'After verification from the details of the consumers of BSES, whose payments were made by the accused, and from the data of bank officials, Jain was first held followed by Khandelwal and Roshan,' said Mishra.
Jain has a telephone shop and Khandelwal was running a garment shop in Gandhi Nagar area.
source: http://in.news.yahoo.com/crime/

Kikombe Cha Loliondo Ni Salama

TAARIFA YA SERIKALI KUHUSU BABU HUKO SAMUNGE LOLIONDO.
TAARIFA YA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII KUPITIA TAASISI ZAKE ZA UTAFITI KUHUSU DAWA YA MCHUNGAJI MSTAAFU AMBILIKILE MASAPILA WA SAMUNGE- LOLIONDO, AMBAZO NI: MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA (TFDA), TAASISI YA UTAFITI WA DAWA ASILI YA CHUO KIKUU CHA AFYA YA SAYANSI SHIRIKISHI MUHIMBILI, (MUHAS) MKEMIA MKUU WA SERIKALI (CGC), TAASISI YA TAIFA YA UTAFITI WA MAGONJWA YA BINADAMU (NIMR).
Taarifa ziliifikia serikali kuwa, Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila, anatibu magonjwa sugu kwa kutumia dawa aliyooteshwa na Mwenyezi Mungu. Inasemekana kuwa, mchungaji alianza tiba hii tangu mwezi Agosti 2010, lakini watu wengi walianza kumiminika kwenda huko Samunge, kuanzia mwishoni mwa mwezi wa pili, mwaka huu wa 2011.
Kufuatia taarifa hii, serikali iliielekeza Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuwa, ufanyike haraka uchunguzi kuhusu dawa hii na itoe ushauri Serikalini ipasavyo. Baada ya kupokea maagizo hayo, wizara iliteua wataalamu kutoka taasisi zake tukiwemo sisi, TFDA, NIMR, Muhimbili kwa maana ya MUHAS, Mkemia Mkuu na tulijumuisha wataalamu wa hapa wizarani, ili kuifanya kazi hiyo muhimu, akiwemo Msajili wa Tiba Asili na Mbadala.
Hapo Machi 7 mwaka huu, sisi TFDA na wenzetu wanasayansi tulifanya safari kwenda Samunge kuonana na kufanya mazungumzo na Mchungaji mstaafu AmbilikileMasapila. Sisi TFDA na wataalam wenzangu wote, tunamshukuru sana mchungaji mstaafu, kwa ushirikiano na msaada mkubwa aliotupa sisi watafiti wote. kwa kuwa, tulifanya mazungumzo kwa masaa kadhaa kuhusu dawa hiyo jinsi alivyoanza, pia, alituonyesha mti unaotumika na alitupa sehemu mbali mbali za mti huo, kwa uchunguzi zaidi. Kadhalika, alituonyesha jinsi anavyotayarisha dawa hiyo na kutupatia sampuli yake iliyokwishategenezwa, tayari kwa matumizi. Sisi TFDA na wataalamu wenzetu tuliondoka nayo, kwa ajili ya uchunguzi zaidi, kwenye maabara zetu.
Baada ya kurejea kituoni Dar es Salaam, kazi ya utafiti wa dawa hiyo ilianza:
Jambo la kwanza kama watafiti, ilikuwa ni kuangalia na kuhakikisha usalama wa dawa ya Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila kwa watu. Uchunguzi uliofanyika, umetoa matokeo ambayo tumeridhika kuwa, dawa kwa kipimo anachotumia Mchungaji mstaafu AmbilikileMasapila, haina madhara yoyote yanayotambulika kwa sasa, kwa matumizi ya binaadamu.
Kazi inayofuata kwetu sisi watafiti baada ya matokeo haya, ni kuchunguza na kubaini, kama kweli dawa hii inatibu magonjwa hayo matano (5), kama anavyoeielezea yeye Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila. Uchunguzi huu utakapo kamilika, matokeo yake yatatolewa mara moja kwa wananchi wote!.
Hata hivyo, ninaomba kuwatahadharisha kuwa, hatua hii ya uchunguzi, si ya muda mfupi. Kwa mujibu wa kanuni na taratibu za kisayansi duniani, tafiti za namna hii zina mchakato unaohitaji muda wa kutosha kukamilisha hatua zake mbali mbali, na pia, kufikia viwango na vigezo vinavyokubalika Kitaifa na Kimataifa. Tunafanya hivyo kwa kuzingatia kuwa, dawa hii ni kwa ajili ya matumizi ya binadamu, na inafuatiliwa na wananchi wetu na mataifa mbalimbali.
Sambamba na utafiti katika hatua hii, pia tunafanya uchambuzi wa kisayansi, katika maabara zetu, kwa sampuli tuliyoichukua kwa Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila, kwa kuangalia mambo mengine mawili muhimu kama ifuatavyo:
1. Kwa hatua tuliyofikia na taarifa tulizo nazo za dawa hii mpaka sasa, tumeandaa na tunakamilisha taratibu, ili tuweze kufuatilia maendeleo ya kiafya ya wagonjwa 200, ambao wamekubali kwa ridhaa yao wenyewe, kushiriki katika utafiti huu, ili kuona maendeleo yao kiafya, baada ya kunywa dawa ya Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila, kwa maradhi walionayo. Hatua hii, inafuata vigezo vyote vya Kitaifa na Kimataifa.
2. Pia tumeweka utaratibu madhubuti, wa kufuatilia matumizi ya mti huu, kama “mmea tiba”, katika sehemu nyingine za nchi yetu, kwani tuna taarifa kuwa, makabila mbali mbali yamekuwa yakitumia mti huu kama tiba. Makabila hayo ni pamoja na; Wagogo, Wamasai, Wabarbaig na Wasonjo kule Samunge.
Kwa niaba ya watafiti na wataalam wenzangu, ninaomba nimalize kwa kusema kwa muhtasari kuwa;:
1. Sisi sote tumeridhishwa kuwa, dawa anayotoa Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila, haina madhara yeyote yanayotambulika kwa sasa kwa matumizi ya binadamu. jambo hili mwazoni lilitia wasiwasi Serikali, Wataalam mbalimbali na wananchi kwa ujumla.
2. Kazi hiyo ya utafiti inaendelea ili kubaini magonjwa inayotibu,
3. Katika hatua hii, ninapenda kuwashukuru wataalamu wenzangu wote wa kikosi kazi cha wataalam wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Ofisi ya mkuu wa wilaya, Ngorongoro na ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha na wananchi wote kwa kufanikisha zoezi hili mpaka sasa.
4. Pia sisi tunamshukuru sana Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila, kwa ushirikiano alioutoa, kwa timu ya watafiti waliofika kumuona, kuanzia siku ya kwanza mpaka leo hii..
Mwisho ninachukua fursa hii, kuwaomba wananchi wawe na subira katika kipindi hiki ili watupe nafasi tuweze kufanya kazi hii ya utafiti na uchambuzi zaidi, kwa utulivu na umakini wa juu kwani duniani kote, tafiti za aina hii, hazina njia ya mkato, nasi tunaahidi kwamba, tutatoa taarifa ya kina mara utafiti utakapo kamilika.
Asanteni.
Chanzo: http://www.globalpublishers.info/

MSIBA TANZANIA

ARAFA HAMISI BILAL 1962-2011
Jumuiya ya Watanzania Italy kwa masikitikiko makubwa imepokea taarifa za msiba wa Shangazi yake Dada Sophia ambaye anaishi Castel Volturno CE -Italia. Marehemu ARAFA HAMISI BILAL amefariki siku ya jumapili nchini India ambako alikuwa huko kwa matibabu.
Mipango ya mazishi inafanywa.Mazishi yatafanyika siku ya jumatano kwenye makaburi ya kisutu jijini Dar Es Salaam. Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania Italia kwa niaba ya Watanzania wote waishio Italia inaungana na wazazi,ndugu,jamaa na wafanyakazi wa Uwanja wa ndege wa kimataiafa wa MWALIMU NYERERE ambako marehemu alikuwa akifanya kazi,katika kuomboleza na kuwaombea Mwenyezi Mungu awape uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba.

Monday, March 28, 2011

NONDOZI ACHARYA INSTITUTES, BANGALORE, INDIA ACHARYA EAST AFRICAN STUDENTS OF ACHARYA








wapatao 32 wala nondiz (jumamosi 26/03/2011).

Wingi Wa Watu Wamwelemea Mchungaji Ambilikile Mwasapile "Babu"

Mchungaji Ambilikile "Babu" Mwasapile
Mchungaji mmoja wa Tanzania amewaomba watu waache kwenda kwenye eneo lake la kijijini kupata "tiba ya miujiza" baada ya maelfu ya watu kufurika kwake, na kusababisha vurumai eneo hilo.
Mchungaji Ambilikile "Babu" Mwasapile, mwenye umri wa miaka 76, alisema hataki wateja wengine wapya mpaka siku ya Ijumaa tarehe 1 Aprili, ili mkusanyiko huo wa watu upungue.
Vyombo vya habari nchini humo vimesema takriban watu 52 wamefariki dunia wakisubiri kupata tiba yake.
Mwandishi mmoja wa BBC alisema msururu wa watu umeongezeka hadi kufikia kilomita 26.
Imani za kimiujiza na kupona kwa tiba za asili zimeenea sana nchini Tanzania.
Baadhi ya waganga wa kienyeji walisema viungo vya maalbino ni bora wakati wa kutengeneza hirizi, na kusababisha mauaji ya albino wengi katika miaka ya hivi karibuni.
Dawa ya Bw Mwasapile imetengenezwa na mitishamba na maji, ambapo huiuza kwa shilingi 500 za Kitanzania.
Wataalamu wa kitabibu nchini Tanzania wanafanya uchunguzi iwapo dawa hiyo ni salama na kama ina sifa zozote za kutibu.
Alipomtembelea Bw Mwasapile nyumbani kwake eneo la Loliondo hivi karibuni, mwandishi wa BBC Caroline Karobia aliwakuta watu 6,000 wakimsubiri askofu huyo mstaafu wa kanisa la Kilutherani la Tanzania (ELCT).
Watu husubiri kwa siku kadhaa barabarani na nje ya nyumba yake katika kijiji cha Samunge, bila ya kuwa na mahala pa kulala, maji safi wala vyoo.
Huku taarifa za tiba hiyo zikiwa zimeenea kwa kipindi cha mwezi mmoja uliopita juu ya uwezo wa mchungaji huyo kutibu, imefika hatua ya baadhi ya watu kutolewa hospitali na ndugu zao ambao wanaamini kuwa watatibiwa na Bw Mwasapile.
Baadhi wamekufa kabla hata ya kuonana naye, wakati wengine wameripotiwa kufariki dunia baada ya kunywa dawa yake.
Polisi wa ziada wamesambazwa eneo hilo kudhibiti idadi kubwa ya watu waliojitokeza, baadhi wakiwa wamesafiri kutoka nchi jirani ya Kenya na kwingineko.
Bw Mwasipile aliomba mapumziko hayo kufuatia mkutano na maafisa wa eneo hilo.

Abhishek Tells Youth Keep Off Drugs

Actor Abhishek Bachchan
Actor Abhishek Bachchan has appealed to the youth to stay away from drugs. “Taking drugs is the most uncool thing to do,” he said, while flagging off an awareness run against drug abuse organised on Sunday morning by the Narcotics Control Bureau (NCB) as a part of its silver jubilee celebration.
More than 300 National Cadet Corps cadets, volunteers from non-governmental organisations and civilians participated in the run. It was followed by an interactive session on drug abuse and the rise in cases of children using drugs.
The session saw a discussion on the steep rise in the use of whiteners as drugs among children in the last two to three years. It has been reported that whiteners are largely being used by school-going children as inhalers for intoxication. Many schools in the State have reported an increase in consumption of whiteners. What has added to the woes of the agencies is that whiteners are not covered under the Narcotic Drugs and Psychotropic Substances Act.
A senior official told The Hindu that it was impossible to ban such substances. “People need to be sensitised on these issues. Especially the parents and the school authorities need to be informed about the use of whiteners.”
“A few months ago, the Pune police issued a circular to stationery shop owners about the use of whitener as drug. The appealed to them to check sudden rises in its sale,” he said.
During the interactive session, Dr. M.S. Menon, a medical consultant with experience in addiction management, said drugs impacted not only the individual but also society. “Drugs not only bring about undesirable physical changes, but they also make a person anti-social,” he said.
“Harmless-looking drugs like cough syrups, pain-killers are being abused by the people. The drugs are easily available over the counter as there are no strict rules about the delivery of prescription medicines,” he said.
Mr. Wanage said drug addiction was on the rise among the educated, urban youths who started earning at a young age. “They want to work hard and party harder. It starts with recreational drugs.” The rise in rave parties was a case in point.

Sunday, March 27, 2011

TUZO ZA KILI MUSIC AWARDS 2011

Hawa ndio ma-mc Milad Ayo na Penny katika Sherehe nzima za KILI MUSIC AWARDS 2011.
Pichani kulia ni mwanamuziki mkongwe kutoka bendi ya Msongo Ngoma Band,Mzee Mabella akionesha tuzo yake aliyoibuka nayo usiku wa kuamkia leo,tuzo hiyo ni imenyakuliwa na Mzee Mabella kuwa msanii binafsi ambaye hakuwahi kuhama bendi yako ya Msondo kwenda bendi nyingine tangu anaanza mziki (Tuzo binafsi ya Hall of Fame).
Waziri wa habari,vijana,utamaduni na michezo Dk.Emmanuel Nchimbi pichani Shoto akikabidhi tuzo ya taasisi,shirika la utangazaji la TBC kwa kuweza kuhifadhi nyimbo za wanamuziki kwa muda mrefu. (tuzo ya taasisi hall of Fame).
Mzee Yusuph akikabidhiwa tuzo yake ya wimbo bora wa taarabu uitwao Valentine kutoka Mchezaji wa mpira,Juma Kasseja.
Mapacha 3 nao waliibuka na tuzo yao wimbo bora wa kiswahili (bendi) uitwai Shika ushikapo.
Tuzo ya reppa bora ilinyakuliwa na mwanamuziki Khalid Chokoraa.
Mwenyekiti wa Tanzania Mitindo House ,Khadija Mwanamboka akimkabidhi msanii wa kizazi kipya Linah tuzo ya msanii bora wa kike,Linah pia aliibuka na tuzo ya msanii mpya anayechipukia.
Tuzo ya wimbo bora wa hip hop ilinyakuwaliwa na msanii Joh Makini (kulia pichani) akiwa ameambatana na wasanii wenzake kadhaa.
Tuzo ya prodyuza bora ilikwenda kwa Lamar wa Fish Crub.
Msanii wa Bongo Flava,Ali Kiba akilishambulia jukwaa usiku huu ndani ya ukumbi wa diamond jubilee hall.
Msanii wa Bongo Flava,Diamond akiwaburudisha mashabiki usiku huu.
Wimbo Bora wa Reggae, What u Feel Inside - Hardmad.Msanii C-Pwaa alikabidhiwa tuzo yake ya video bora ya muziki wa mwaka uitwao ACTION aliomshirikisha DullySykes,Ngwair pamoja na Ms Trinity.C-Pwaa bia ameibuka na tuzo ya wimbo bora wa ragga/dancehall uitwa Action.
Wimbo bora wa RnB Nikikupata ulienda kwa msanii Ben Pol. Muigizaji na msanii wa muziki wa kizazi kipya Mpoki tuzo yake ya wimbo bora wa asili wa Tanzania uitwao Shangazi.
Mwimbaji bora wa kike tuzo ilienda kwa Lady JD.
Pichani kushoto ni mtayarishaji wa muziki kutoka studio ya Combinations Sound a.k.a Combinenga,Man Water akipokea tuzo ya mwimbaji bora wa kiume (kwa niaba ya ) 20% kutoka kwa Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd Juhyana Kusaga,anaefuatia ni Mkurugenzi wa Masoko kampuni ya bia TBL,David Minja.Katika hali ya shangwe furaha na vifijo vilivyotokea ukumbini,ambavyo vimesababishwa na msanii muziki wa kizazi kipya 20% ,kwamba ameweza kunyakua tuzo tano kuliko msanii mwingine yeyote aliyewahi kuchukua tuzo hizo tangu zianzishwe hapa nchini.
20% Akomba Tuzo za Kili Tanzania Music Awards 2011, Ukumbi Wazizima Kwa Shangwe ,haijawahi tokea!!

1.Tuzo ya wimbo bora wa Afro Pop-Tamaa mbaya.
2.Tuzo ya Mtunzi bora wa nyimbo.
3.Tuzo ya mwimbaji bora wa kiume.
4.Tuzo ya wimbo bora wa mwaka.
5.Tuzo ya msanii bora wa muziki wa kiume.
Mdau Hot Pot akichukua tuzo ya wimbo bora wa Afrika Mashariki ambayo ilinyakuliwa na Kidumu pamoja na Lady jay dee.Lady Jay Dee pia alinyakuwa tuzo ya Mwimbaji bora wa kike.
Baadhi ya wasanii wa Hip Hop Kushoto ni msanii Bonta, JayMoe, K-singo, Nikki wa Pili na Ruben (Ncha Kali).
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Jay Moe na Jcb walinyakua tuzo ya wimbo bora wa kushirikiana/kushirikishwa uitwao Ukisikia Paah!.

THT wakitumbuiza kwenye tuzo hizo.
Wahudhuriaji katika Tuzo za Kili Music Awards 2011 wakifuatilia kwa umakini.