Vikosi vinavyomuunga mkono Alassane Ouatarra anayetambuliwa na Jumuiya ya Kimataifa kuwa rais halali wa Ivory Coast kwa sasa vinaidhibiti miji miengine minne muhimu. Kwa mujibu wa msemaji wa kiongozi anayeng’ang’ania madaraka nchini humo Laurent Gbagbo aliyehojiwa na kituo cha Radio ya Ufaransa cha RFI, kambi yao inatoa wito wa kusitisha mapigano kwa kuwa wanaelekea kushindwa. Hata hivyo kambi ya Outarra imesema kuwa muda umeshapita wa kutafuta suluhu ya amani au kugawana madaraka. Laurent Gbagbo amekuwa akiendelea kung’ang’ania madaraka hata baada ya Jumuiya ya Kimataifa kumtambua Alassane Ouattara kama mshindi halali wa awamu ya pili ya uchaguzi wa rais uliofanyika mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka jana.
Wednesday, March 30, 2011
GBAGBO ATAKA MAPIGANO YASITISHWE IVORY COAST
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Wednesday, March 30, 2011
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
0 comments:
Post a Comment