SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, October 13, 2010


Makamu wa Rais wa Kenya atangaza nia yake ya kugombea urais 2012


Makamu wa Rais wa Kenya Kalonzo Musyoka mapema leo ametangaza kuwa mbio za kutafuta ridhaa ya wananchi ili aiongoze nchi hiyo ya Afrika Mashariki imeanza rasmi. Amesema kwamba nia yake ni kuzunguka Kenya nzima akiomba kura na haoni wakati mwingine bora zaidi isipokua wakati huu. Akizungumza katika jimbo la Bungoma, magharibi mwa Kenya Kalonzo amewataka wananchi wawe macho na kuwachagua viongozi wenye sifa nzuri na ajenda ya maendeleo. Weledi wa siasa za Kenya wanasema kuwa iwapo Kalonzo ataamua kugombea urais akiwa peke yake basi atakabiliwa na kibarua kigumu kwani kuna uwezekano mkubwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Raila Odinga akaunda muungano na vyama kadhaa jambo ambalo weledi hao wanasema kuwa litamkosesha usingizi Kalonzo Musyoka. Uchaguzi Mkuu nchini Kenya unatarajiwa kufanyika mwaka 2012.

0 comments:

Post a Comment