SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, September 7, 2010

Mume aeleza alivyoporwa mke na Dk. Slaa
Bw. Amaniel Mahimbo

“NAKUACHIA kibanda chako, nakwenda kwenye nyumba yangu.”

Hayo yalikuwa maneno ya mwisho ambayo Aminiel Mahimbo aliambiwa na mkewe, Josephine Mushumbusi siku alipoachwa na mkewe huyo aliyeamua kwenda kwa mgombea wa urais wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa.

Mahimbo ambaye ni mume halali wa Josephine, (kwa ndoa ya kanisani) alisema anakumbuka kuwa ilikuwa Machi mwaka huu na hakujua mke wake alipokuwa akienda na wala hakuhisi dalili yoyote ya kuwepo kwa mwanamume mwingine katika ndoa yao mpaka siku mwanawe wa kwanza Upendo (7) alipomwambia “baba tunaishi na daddy”.

Akisimulia kisa hicho kilichoanza takribani miezi saba iliyopita, katika mahojiano maalumu na gazeti hili jana, Mahimbo ambaye ndoa yake ilifungwa Agosti 16, 2002 na Mchungaji Lewis Hiza katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Kijitonyama, jijini Dar es Salaam, alisema hakujua kama huyo ‘daddy’, ni Dk. Slaa mpaka siku moja alipoambiwa na mama mkwe wake.
Chanzo na Habari Kamili Nenda Habari Leo
ANGALIZO: MAWAKILI WA BW. MAHIMBO INASEMEKANA WATAFUNGUA KESI MAHAKAMA KUU KUHUSIANA NA UTATA HUU. TUTAWALETEA HABARI ZAIDI KADI ZITAVYOPATIKANA

0 comments:

Post a Comment