
Habari kutoka Sri Lanka zinasema kuwa, kwa akali watu 70 wamepoteza maisha yao katika mripuko wa mapipa matatu yaliyokuwa yamesheheni madini ya dynamite karibu na mji wa Batticaloa, mashariki mwa nchi hiyo. Msemaji wa jeshi la nchi hiyo Meja Jenerali Ubaya Medawela amesema kuwa, mapipa hayo yaliyokuwa na madini hayo hatari, yameripuka ghafla katika kituo cha polisi cha Karadiyanaru, kilomita 260 mashariki mwa Colombo na kusababisha maafa hayo. Ameongeza kuwa, raia wa nchi hiyo na wajenzi 2 raia wa Uchina ni miongoni mwa walioaga dunia katika ajali hiyo. Madini hayo yaliyokuwa yamehifadhiwa katika kituo cha polisi kwa sababu za usalama, yalikusudiwa kutumika katika ujenzi wa barabara, mradi ambao ulikuwa umepewa shirika moja la Kichina.
0 comments:
Post a Comment