Dreva Tax Maarufu Wa Maeneo Ya Villa Na The Kiss Club Auwawa Kikatili Jijini Mwanza
Dereva Tax maarufu wa maeneo ya VILLA na The KISS CLUB zote za jijini Mwanza,aitwaye Karoli mwenye umri kati ya miaka 30-35 mwenye gari Toyota Premio lenye namba za usajili T406BCX ,ameuwawa kikatili na mtu asiyejulikana kwa kuchomwa kisu shingoni na baadhi ya maeneo ya kichwani.
Tukio hilo la kutisha na kuhuzunisha limetokea usiku wa jana mnamo majira ya saa 5:30 katika barabara ya Makongoro,mtaa wa Furahisha Kirumba jijini Mwanza jirani kabisa na kanisa la KKKT MAKONGORO.Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi-Amin.
Pichwa kwa hisani ya Mdau G Sengo-Mwanza
0 comments:
Post a Comment