SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, August 9, 2010

Kundi la al Shabaab lasambaratishwa katika eneo la kaskazini wa Somalia

Sample Image
Yussuf Ahmad Waziri wa Usalama wa eneo lililotangaza kujitenga la Somaliland amesema kuwa, vikosi vya usalama vya eneo hilo vimefanikiwa kulisambaratisha kundi la waasi wa al Shabaab wa Somalia wanaoongozwa na Mohamed Said Atom katika eneo la kaskazini mwa Somalia. Yussuf Ahmad ameongeza kuwa, vikosi vya usalama vya eneo hilo vimefanikiwa pia kuiteka kambi ya kundi hilo la waasi, ambalo hujishughulisha pia na magendo ya silaha nchini Sudan. Amesema kuwa, vikosi vyake vinadhibiti kikamilifu milima ya Galagala iliyoko kati ya eneo la Somaliland na kaskazini mwa Somalia. Waziri wa Usalama wa Somaliland amesema kuwa, kwenye mapigano hayo makali, wanamgambo kumi wa kundi la al Shabaab waliuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa.

0 comments:

Post a Comment