
Rais Omar Hassan Al-Bashir wa Sudan anatarajiwa kuelekea Chad hapo kesho ili kukutana na Rais Idris Deby wa nchi hiyo. Duru kutoka ofisi ya Rais Bashir zinasema kuwa kiongozi huyo atahudhuria mkutano wa viongozi wa nchi wanachama wa Sahel Saharan na kwamba ziara hiyo itadumu kwa siku 3. Hii itakuwa safari ya kwanza ya Rais Bashir katika nchi mwanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC ambayo mwaka uliopita ilitoa waranti ya kutiwa nguvuni kiongozi huyo kwa tuhuma za kutenda jinai za kivita katika eneo la Darfur nchini Sudan. Baadhi ya washauri wake wamemtaka Rais Al-Bashair asiende Chad lakini kiongozi huyo amesema ana imani kuwa mwenyeji wake Rais Deby hawezi kumsaliti
Rais Kagame awahakikishia Wanyarwanda uchaguzi mkuu wa huru na wa haki
|

Vyama vingine vya kisiasa bado vinakabiliwa na matatizo huku vingine vikiwa bado havijasajiliwa rasmi na hivyo kukifanya chama tawala kiendelee kupata nguvu.
0 comments:
Post a Comment