SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, June 19, 2010

Wananchi wa Marekani hawana imani na Rais Barack Obama


Sample Image    Uchunguzi wa maoni uliofanywa hivi karibuni unaonyesha kwamba wananchi wa Marekani wamepoteza imani na utendaji kazi wa Rais Barack Obama baada ya serikali yake kushindwa kuziba kisima cha mafuta katika Ghuba ya Mexico. Kwa mujibu wa uchunguzi huo wa maoni uliofanywa na kanali ya televisheni ya CNN, karibu zaidi ya nusu ya Wamarekani wanaamini kuwa, Obama hana uwezo wa kutosha wa kushughulikia matatizo yanayoikabili nchi hiyo na wananchi wake.
   Uchunguzi huo aidha umeeleza kwamba, mtazamo wa watu wengi wa Marekani ni kwamba kushindwa Obama kutatua mgogoro wa kuvuja mafuta katika kisima cha shirika la Uingereza la British Petroleum BP huko baharini ni sawa na kushindwa George Bush rais wa zamani wa Marekani kushughulikia matatizo ya tufani ya Katrina.
   Hii ni katika hali ambayo Mkuu wa Shirika la Mafuta la Uingeza BP amejigamba kuwa shirika hilo bado ni imara hata kama limekumbwa na matatizo kutokana na kisima chake cha mafuta kuvuja kwenye Ghuba ya Mexico.Carl Henric Svanberg pia amekanusha matamshi ya Rais wa Russia kwamba shirika hilo linaweza kusambaratika
   Mbunge mmoja wa Ujerumani ataka uhusiano wa nchi hiyo na Israel uvunjwe    
Kiongozi wa chama cha Ujerumani cha National Democratic Party (NDP) ameitaka nchi hiyo ivunje uhusiano wa aina yoyote ile na utawala wa Kizayuni wa Israel na pia ametaka utawala huo ghasibu uwekewe vikwazo vya kiuchumi.
   Holger Apfel amesema katika hotuba yake iliyozusha mjadala mkubwa kwenye Bunge la Ujerumani kwamba, inabidi uhusiano na Wazayuni makatili wa Israel uvunjwe mara moja na haipaswi kuunga mkono ngano zisizo na ukweli za Holocaust.
   Mbunge Apfel pia alikataa kuondoka jukwaani baada ya muda wake kuisha, na alipoondolewa kwa nguvu aliendelea kuwaita Wazayuni kuwa ni magaidi.
   Kwa upande mwingine Bunge la Umoja wa Ulaya limepitisha azimio dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Azimio hilo linataka kufanyike uchunguzi huru wa kimataifa kuhusu jinai zilizofanywa na makomandoo wa Israel dhidi ya msafara wa meli zilizokuwa zinaelekea Ghaza zikiwa na misaada ya kibinaadamu. Swahili Radio

Hali bado tete nchini Kirgistan 
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa , Ban Ki-moon ametoa wito kwa mataifa wanachama wa umoja huo kuchangia misaada ya kiasi cha euro milioni 58 kwa ajili ya nchi ya Kirgistan
Waandamanaji  wanajikusanya  
mbele  ya  jengo  la  serikali  
wakizuiwa  na  polisi  katika  mji  wa  Talas,  nchini Kyrgyzstan.
Waandamanaji wanajikusanya mbele ya jengo la serikali wakizuiwa na polisi katika mji wa Talas, nchini Kyrgyzstan.
NEW YORK:
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon ametoa mwito kwa wanachama wa umoja huo kuchanga msaada wa kiasi cha Euro milioni 58 kwa ajili ya nchi ya Kyrgyzstan iliyokumbwa na machafuko ya kikabila. Ban ki-moon amesema fedha hizo zitatumiwa kuwasaidia kiasi ya wakimbizi 300,000 na raia wengine walioathirika kwa machafuko hayo.
Hapo awali,Rais wa mpito wa Kyrgyzstan, Rosa Otubajewa alikiri kuwa idadi ya watu waliouawa huenda ikawa ni 2,000 - hiyo ni mara kumi zaidi ya vile ilivyotathminiwa hapo awali. Wakati huo huo Urusi inafikiria kupeleka wanajeshi wake nchini Kyrgyzstan ili kulinda vituo muhimu nchini humo. Lakini uamuzi bado haujapitishwa. Hiyo ni kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Urusi vilivyoinukulu  wizara ya ulinzi mjini Moscow.

0 comments:

Post a Comment