Simba mmoja amemwuua mfanyakazi
wa hifadhi ya wanyama pori yatima nchini Zimbabwe.
Mnyama huyo alitoroka kwenye chumba
alichofungiwa kilichoachwa wazi kwa bahati mbaya na kumshambulia Robyn
Lotz mwenye umri wa miaka 26.
Taarifa iliyotolewa na hifadhi hiyo ya
Chipangali imesema simba huyo mwenye manyoya shingoni, ajulikanayae kama
Lobi, alimbwaga chini binti huyo na kushikilia kichwa cha Lotz kwenye
mdomo wake.
Mkurugenzi wa hifadhi hiyo alimpiga risasi simba
huyo lakini Bi Lotz alikufa kutokana na majeraha muda mfupi baada ya
kupelekewa kwenye hospitali mjini Bulawayo.
Shambulio hilo lilitokea siku ya Jumanne asubuhi
wakati wafanyakazi walipokuwa wakisafisha malazi ya wanyama hao na
kuwatandikia majani.
Mkurugenzi Kevin Wilson alichapisha katika
mtandao wa Chipangali, " Kwa hofu kubwa nilimwona Lobi akijikunyata juu
ya Robyn, alimwingiza mdomoni mwake huku akiwa amemshikilia kichwani
mwake."
Hifadhi hiyo ilianzishwa mwaka 1973 na kuwatunza
wanyama yatima, waliotengwa, waliojeruhiwa na waliozaliwa nje ya eneo
lao la asili.
BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment