SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, June 19, 2010

MO Atembelea Chuo Cha Uhasibu Tanzania Tawi la Singida

Pichani Mh.Mohammed Dewji Mbunge wa Singida mjini akiangalia Picha yenye ramani ya Mjengo wa Chuo Cha Taasisi ya Uhasibu Tanzania Tawi la Singida alipotembelea Chuoni hapo week end iliyopita,anayeshuhudia ni Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Bw.Emmanuel Kingu alipomkaribisha MO ofisini kwake.
MO akiwa na Viongozi wa Chuo cha Uhasibu akiongozwa na Mkuu wa Chuo Bw.Emmanuel Kingu(wa pili kulia) wakati wa kukagua Majengo ya Chuo hicho(Kushoto) Rais wa Chuo Bw.Evans Crispin(Kulia) Waziri Mkuu wa Chuo Bw.Mbaraka Ismail.
MO akizindua Viti Maalum kwa ajili ya kukalia wanafunzi wakati wa Kujisomea”VIMBWETA”.
MO akiwa na Uongozi wa Chuo hicho pamoja na Wanafunzi wakiwa wanaonekana wamekalia viti hivyo(VIMBWETA).
Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu TIASO wakimsikiliza Mh.Mohammed Dewji Mbunge wa Singida Mjini(hayupo pichani) alipokuwa akiongea na Wanafunzi wa Chuo hicho kuwahimiza kusoma kwa bidii na pia aliwaahidi wanafunzi hao kuwapa Jezi za Michezo seti 5 pamoja na Mipira 20.
MO akimkabidhi cheti mmoja wa viongozi wa wanafunziMO akimkabidhi cheti Waziri wa Wanawake na Maendeleo ya Jamii(TIASO) Mh.Fatuma Hamisi akipokea cheti cha Uongozi bora. MO akimkabidhi cheti cha Uongozi Bora Rais wa TIASO,Mh.Evans Crispin. Mo akipiga picha na baadhi ya wanafunzi wanaoonekana kufurahia ujio wakeMO Katika Picha ya Pamoja na Uongozi wa Chuo cha TIASO.

0 comments:

Post a Comment