Mshambuliaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20
Ngorongoro Heroes , Thomas Ulimwengu (kulia) akimtoka beki wa timu ya
vijana ya Malawi, Lucky Malata (5) katika mchezo wa kuwania kufuzu
fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana uliofanyika leo kwenye Uwanja
wa Uhuru, Dar es Salaam. Ngorongoro ilishinda 3-1. Mshambuliaji
wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 Ngorongoro Heroes
, Thomas Ulimwengu (kulia) akiwania mpira sambamba na beki wa timu ya
vijana ya Malawi, Limbikani Mzava katika mchezo wa kuwania kufuzu
fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana uliofanyika leo kwenye Uwanja
wa Uhuru, Dar es Salaam. Ngorongoro ilishinda 3-1.
Golikipa wa timu ya taifa ya Malawi ya vijana chini ya miaka 20, Alex
Makina akiuangalia mpira ukitinga wavuni na kuhesabu bao la pili kwa
timu ya taifa ya Ngorongoro Heroes. kocha wa timu ya taifa ya vijana ya Malawi akiwa ameeduwaa baada ya mchezo kumalizika
Kocha wa timu ya vijana chini ya 20, Rodrigo Stockler akimpongeza
mfungaji wa bao la pili la timu hiyo, Omega Seme wakati mchezo wa
kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana uliofanyika leo
kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Ngorongoro ilishinda 3-1. Kwa
matokeo hayo timu ya ngorongoro itakutana na timu ya vijana ya Ivory
Coast wiki ya tatu ya mwezi mei ambapo mchezo wa kwanza utafanyika
katika nchini Ivory Coast na baada ya wiki mbili timu hizo zitarudiana
katika dimba uwanja wa taifa, Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment