SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, May 5, 2010

Mshukiwa wa kulipua bomu akamatwa

Time Square
Time Square, New York
Mtu mmoja anayeshukiwa kujaribu kulipua bomu kwenye gari mjini New York amekamatwa.
Faisal Shahzad, raia wa Marekani mwenye asili ya Pakistan, anashutumiwa kuendesha gari lenye bomu huko Times Square Jumamosi jioni.

Anatarajiwa kufikishwa mahakamani baadae hii leo huko Manhattan.

Mwanasheria Mkuu wa Marekani Eric Holder amesema Bw Shahzad alikamatwa katika uwanja wa ndege wa John F Kennedy akijaribu kupanda ndege kuelekea Dubai.

Chanzo cha usalama cha Pakistan kutoka mji mkuu wa Islamabad ameiambia BBC hakikujua lolote kuhusu Bw Shahzad.

Pia ametupilia mbali taarifa iliyotolewa na kundi la Taliban la Pakistan likidai kuhusika na shambulio hilo lililoshindwa na kuahidi mashambulio mengine yataibuka.

Taarifa kutoka Marekani zinasema Bw Shahzad alirudi kutoka ziara ya miezi mitano nchini Pakistan hivi karibuni.

Shirika la kijasusi la Marekani FBI limesema limepekua nyumba yake huko Bridgeport, Connecticut, siku ya Jumanne.
Gari lililokuwa na bomu lililotengenezwa kwa mbolea, fashfashi, petroli na tangi la gesi ya kulipuka ya propane ziliachwa Time Square siku ya Jumamosi.

Gari aina ya Nissan Pathfinder liliachwa likiwa limeegeshwa huko Times Square, likiwa bado limewashwa na taa zake zikiwa zinawaka.

Bomu hilo liligunduliwa na kuteguliwa kabla haijalipuka.

Bw Holder ameuambia mkutano wa waandishi wa habari kwamba wachunguzi walikuwa wanaendelea vizuri, wakiongeza: "Hatutapumzika mpaka kila mmoja anayehusika afikishwe mbele ya haki."

Amewasihi raia wa Marekani kubaki na tahadhari na kuripoti jambo lolote linalotia shaka.

Bw Eric Holder, Mwanasheria Mkuu wa Marekani amesema jaribio la bomu hilo la gari "lingeua watu wengi sana iwapo lingelipuka."

Amesema: "Ni wazi kuwa nia ya tendo hili la ugaidi ni kuua Wamarekani."
Times Square ilisheheni watalii wengi wakati mchuuzi alipotoa taarifa ya kuwepo bomu hilo.

0 comments:

Post a Comment