Waziri
Mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai anafanya ziara nchini Marekani
kujadili hatua za mageuzi nchini mwake pamoja na miradi inayostahili
kufadhiliwa.
Tsvangirai amekutana na waziri wa mambo ya nje Hillary Clinton ambaye amepongeza hatua zilizopigwa kuafikia mageuzi.Aidha Bi. Clinton amempongeza Bw. Tsvangirai kwa kusaidia nchi yake kujikwamua kutoka hali ngumu ya kuchumi.
Marekani ndiyo mfadhili mkubwa zaidi wa miradi ya kibinadamu nchini Zimbabwe.
Mwaka jana Zimbabwe ilipokea dola milioni mia tatu kutoka kwa Marekani kama msaada ya kibinadamu.
0 comments:
Post a Comment