
Michael
Ballack alipoumizwa.
Kiungo wa Ghana Kevin Prince
Boateng ameomba radhi kutokana na rafu aliyocheza iliyomfanya nahodha
wa Ujerumani Michael Ballack kutoweza kucheza Kombe la Dunia nchini
Afrika Kusini.
Ballack alijeruhiwa baada ya kukabiliwa na
mchezaji huyo wa Portsmouth siku ya Jumamosi.Boateng, ambaye atakuwemo katika kikosi cha Ghana kitakachokabiliana na Ujerumani katika kundi D kwenye fainali za Kombe la Dunia, amesisitiza hakukusudia kumuumiza Ballack.
Boateng amesema "Naomba radhi. Sikukusudia kumuumiza. Ilikuwa ni tukio lililotokea bila kupanga."
"Ni tukio lililoonekana la kupuuzi, mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana alieleza kupitia gazeti la michezo la Bild la Ujerumani.
Msamaha huo umetolewa siku tatu baada ya Ballack kuchezewa rafu wakati wa fainali ya kuwania kombe la FA baina ya Portsmouth na klabu anayochezea na haujawapunguzia ghadhabu Wajerumani wanayoilekeza kwa Boateng.
Ballack aliumia katika kipindi cha kwanza kwenye mchezo huo wa Jumamosi, baadae timu yake ilishinda bao 1-0.
BBC Sawhili.




0 comments:
Post a Comment