Maafisa nchini Libya wamesema ndege ya abiria imeanguka katika uwanja wa ndege mjini Tripoli na kuua takriban watu 104.
Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la ndege la Afriqiyah ilikuwa safarini kutoka mjini Johannesburg, Afrika Kusini.
Maafisa
wamesema ilianguka wakati ikjaribu kutua karibu na uwanja huo.Takriban
abiria 93 walikuwa ndani ya ndege hiyo aina ya Air Bus 330.Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la ndege la Afriqiyah ilikuwa safarini kutoka mjini Johannesburg, Afrika Kusini.
Watu hao wanaaminika kutoka mataifa mbalimbali zikiwemo nchi za Uingereza na Afrika Kusini.Wafanyikazi 11 wa ndege hiyo wameripotiwa kuwa raia wa Libya.
Ndege hiyo ilitarajiwa kuelekea eneo kwenye uwanja wa ndege wa Gatwick mjini London baada ya kusimama kwa muda mjini Tripoli.
Mwandishi wa BBC mjini Tripoli Rana Jawad amesema haijabainika ikiwa ndege hiyo ilikuwa imekwishatua wakati ajali hiyo ilipotokea.Walioshuhudia wamesema hawakuiona ndege hiyo kwenye uwanja wa ndege.
Magari ya kuwabebea wagonjwa yameonekana kuelekea kwenye uwanja huo. Shirika la ndege la Afriqiyah lilianzishwa nchini Lybia mwaka wa 2001.
0 comments:
Post a Comment