SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, April 30, 2010

KAPUYA ATANGAZA KIMA CHA CHINI CHA MSHAHARA KWA SEKTA BINAFSI!!

 Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana Prof. Juma Kapuya(kulia) akitangaza viwango vipya vya mishahara kwa kima cha chini kwa wafanyakazi wa sekta binafsi leo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.Viwango hivyo vya kima cha chini cha mshahara kwa wafanyakazi vinazigusa sekta za Afya,Huduma za Kilimo, Viwanda na Biashara, Mawasiliano, Sekta ya Madini, Bandari na sekta ya Uvuvi, Wafanyakazi wa majumbani,sekta ya ulinzi Binafsi na Hoteli. (Picha na Aron Msigwa wa Maelezo) Waziri Kapuya amevitaja baadhi ya vima vya chini vya mishahara hiyo kwa sekta mbalimbali binafsi, ambapo amesema wafanyakazi wa Sekta ya kilimo kima chao cha mshahari kinakuwa shilingi 70.000, Sekta ya Viwanda 80.000, sekta ya Mawasiliano 350.000 upande wa wafanyakazi wa ndege, wafanyakazi wa mashirika ya Crealing Foward 230.000, Kampuni za simu 300.000, Sekta ya madini 350.000, Sekta ya uvuvi 165.000 wafanyakazi wa majumbani 90.000 walioajiriwa kwa mabalozi wanaofanya kazi kwenye makampuni binafsi ya usafi maofisini 80.000 na majumbani, kwa habari zaidi fuatilia vyomba mbalimbali vya habari.

0 comments:

Post a Comment