Waziri Sofia Simba katikati akicheza ngoma ya asili.
.
Imeelezwa
kuwa, Mwanamke mmoja hufa kwa ugonjwa wa Saratani kila baada ya sekunde
moja Duniani kote.hususani walio na tatizo la Saratani ya Matiti. Hayo
yalisema jana na Waziri wa Maliasili na Utalii,Shamsa Mwangunga katika
matembezi ya Hisani ya kuchangia mfuko wa Saratani ya Matiti Tanzania
,iliyofanyika katika viwanja vya taasisi ya hospitali ya magonjwa ya
kansa Ocean Road .
.
Katika
hotuba yake hiyo, Shamsa ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu Mizengo
Pinda, ambapo Mabalozi mbalimbali waliwakilisha katika matembezi hayo
yaliyowakilisha pamoja na vikundi mbalimbali vya kijamii na wanafunzi
waliotembea kwa mwendo wa kilometa 6 yakiongozwa na Mwangunga.
Katika Hotuba yake hiyo,
Mwangunga aliitaka jamii kufunguka macho na kujitokeza kwa wingi
kuangali afya zao na kutambua dalili za ugojwa huo mapema.
Katika matembezi hayo, Waziri
Mkuu aliweza kuchangia shilingi Milioni tano huku kwa upande wake,
Mwangunga alichangia mfuko huo kupipitia taasisi na idara ya wizara
yake shilingi milioni nne.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Chipukizi Wilya ya Kinondoni na Mwanaharakati wa kutetea haki za watoto
nchini, Nimka Lameck (10) ambaye alikuwa maalum kutoa ujumbe kwa
wananchi kuwa ugonjwa ni hatari hivyo kila mtoto anahaki ya kutoa
ujumbe kwa jamii.
Naye Mkurugenzi na Mwanzilishi
iwa Mfuko Asasi hiyo, Angela Kuzilwa aliwashukuru wadau mbalimbali
walifanikisha katika taasisi hiyo pamoja na kutumikia Akina mam
karibuni nchi nzima huku akitoa wito kwa wadau kujitokeza kuisaidia
taasisi hiyo kwa michango ya hali na mali .
.
Taasisi
hiyo ambayo makao yake makuu yapo jijini Dar es Salaam , Mwananyamala,
inaendesha shughuli za ushahuri kwa waakina mama ilikujitambua na
kushahuriwa kupima mapema ilikuepuka kupata matatizo makubwa huku
matembezi hayo kwa mwaka huu yakifanyika kwa mara ya pili baada ya yale
ya mwaka juzi.
Kwa upande wake Dkt Twalib
Ngoma wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road , aalitoa wito kwa akina
mama kujitokeza kwa wingi kuchunguzwa afya zao ilikujijua mapema kama
wameambuzaikwa au la, “ Tunawaomba akimama kujitokeza kwa wingi kupima
afya juu ya ugonjwa huu mapema ilikuondoa ukubwa wa tatizo” alisema Dkt
Ngoma. Huku mlezi wa taasisi hiyo, mke wa rais wa awamu ya tatu, Anna
Mkapa alitoa wito kwa taasisi mbalimbali kujitokeza na kuichangia
ilikupunguza kwa asilimia kubwa ya ugonjwa huo ambao unawapata akina
mama walio na umri wa miaka 40 na kuendelea pamnoja na idadi ndogo ya
wanaume
0 comments:
Post a Comment