Rais
Mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi akiwasili katika viwanja vya
Karimjee kuhudhuria Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es
salaam Saidi Meck Sadiki (wa pili kutoka kushoto) kwa watoto yatima
kutoka vituo mbalimbali vya kulelea watoto hao vya jiji la Dar es
salaam. Wengine wanaoonekana kutoka kulia ni Kamanda wa Kanda Maalum ya
Dar es salaam, Kamishna Suleiman Kova na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es
salaam Alhadi Mussa Salum.
Kamanda
wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Suleiman Kova (katikati)
akifafanua jambo kwa viongozi wa mkoa wa Dar es salaam Mkuu wa Mkoa wa
Dar es salaam Bw. Saidi Meck Sadiki (wa pili kutoka kulia), Mkuu wa
Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi(kulia) na Mkuu wa wilaya ya Temeke Bi.
Sophia Mjema (kushoto) wakati wa Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa
huo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.
Mkuu
wa wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema (kushoto) akizungumza jambo na Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Saidi Meck Sadiki (katikati), Mkuu wa
Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi(kulia) na Kamanda wa Kanda Maalum ya
Dar es salaam, Kamishna Suleiman Kova (wa pili kutoka kushoto) wakati wa
Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam katika viwanja
vya Karimjee jijini Dar es salaam.
Sheikh
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Alhadi Mussa Salum (wa kwanza kushoto) na
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahmani Kinana
wakijumuika katika Futari hiyo.
Baadhi
watoto yatima kutoka vituo mbalimbali vya kulelea watoto hao vya jiji
la Dar es salaam wakijumuika pamoja katika Futari iliyoandaliwa na Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki.
Rais
mstaafu wa Awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi ambaye alikuwa mgeni rasmi
wakati wa Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kwa
watoto yatima kutoka vituo mbalimbali vya kulelea watoto hao vya jiji la
Dar es salaam akijumuika pamoja na watoto hao na wageni mbalimbali
walioalikwa katika Futari hiyo.
Baadhi ya akina mama na watoto waliohudhuria Futari hiyo wakipata Chakula.
Rais
wa Tanzania wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi ambaye alikuwa mgeni
rasmi wakati wa Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam
akisisitiza umuhimu wa kulinda na kutunza amani iliyopo kwa kuendelea
kudumisha upendo na ukarimu ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo
yaliyomo katika vitabu vitakatifu.
Mkuu
wa mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa
Songea Dkt. Christine Ishengoma(kulia) wakiungana na viongozi wengine
kushiriki Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kwa
watoto yatima kutoka katika vituo mbalimbali katika viwanja vya Karimjee
jijini
Dar es salaam.
Picha na Aron Msigwa- MAELEZO.
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
Rais
mstaafu wa awamu ya pili , Ali Hassan Mwinyi ,amewataka watanzania kuwa
makini kwa kutoruhusu tofauti za dini zilizopo hapa nchini kuwa chanzo
cha mgawanyiko miongoni mwao.
Kauli
hiyo ameitoa jana usiku jijini Dar es salaam wakati wa Futari
iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki kwa
watoto wanaoishi katika vituo vya kulelea watoto yatima, wananchi na
viongozi mbalimbali iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar
es salaam.
Mzee
Ali Hassan Mwinyi ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa Futari hiyo
amesema kuwa kila Mtanzania bila kujadili itikadi na dini aliyonayo ana
wajibu wa kulinda na kutunza amani iliyopo kwa kuendelea kudumisha
upendo na ukarimu kwa wenzake ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo
yaliyomo katika vitabu vitakatifu.
“Nawasihi
Watanzania wenzangu tuendelee kupendana, tuwe wamoja katika
kushirikiana, kamwe tusiruhusu wala kukubali mgawanyiko wa dini wala
itikadi zetu” Amesisitiza.
Amewashukuru
viongozi wa mkoa wa Dar es salaam wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Saidi
Meck Sadiki kwa uamuzi walioufanya wa kuandaa Futari iliyowaunganisha
watoto yatima, wananchi na viongozi mbalimbali bila kujadili itikadi na
dini zao ikiwa ni ishara ya kuonyesha upendo na ukarimu walio nao.
Kwa
upande wake Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki akizungumza
wakati wa Futari hiyo aliyowaandalia wageni hao amesema kuwa serikali
ya mkoa inaendelea kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo ikiwemo
ukarabati na ujenzi wa miundombinu iliyoharibiwa vibaya wakati wa msimu
wa mvua jijini Dar es salaam.
Bw.
Sadiki ameziagiza Halimashauri za Wilaya za Temeke, Ilala na Kinondoni
na Wakala wa Barabara (TANROAD) mkoa wa Dar es salaam kuhakikisha kuwa
wanarejesha hali ya kupitika kwa barabara iliyokuwepo mwanzo ili
kuwaondolea kero ya usafiri wananchi.
Amezitaka
mamlaka hizo kutumia fedha za ndani na zile zilizotolewa na Serikali
Kuu kukamilisha ukarabati wa miundombinu hiyo yakiwemo madaraja
yaliyosombwa na maji kwa muda muafaka ili kuruhusu magari kuweza kufika
katika maeneo hayo.
Katika
hatua nyingine Bw. Meck Sadiki ametoa wito kwa wakazi wa jiji la Dar es
salaam kushiriki kikamilifu katika suala la usafi na uhifadhi wa
mazingira kwa kujenga utaratibu wa kusafisha mazingira ya jiji ili
kulinda heshima ya jiji huku akisisitiza kuwa dini zote zinamtaka
mwanadamu awe mwadilifu na mwenye kuzingatia usafi.
Amezitaka
mamlaka zinazosimamia utekelezaji wa sheria za kuhifadhi mazingira
jijini Dar es salaam kufanya kazi kwa kuzingatia weledi ili kuhakikisha
maeneo yote ya jiji yanaendelea kuwa katika hali ya usafi. Naye Sheikh
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum akuzungumza
wakati wa Futari hiyo ameeleza kuwa viongozi wa dini na serikali kote
nchini wanalo jukumu kubwa la kuwaongoza wananchi kutenda mema na
kuendelea kuvumilia.
0 comments:
Post a Comment