Ndege ya Uholanzi iliyobeba miili 16 ikiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kharkiv, Ukraine kuelekea nchini Uholanzi.
Baadhi
ya maofisa wakipiga saluti wakati miili ya watu waliopoteza maisha
katika ajali ya ndege ya Malaysia MH17 ikipelekwa kwenye ndege.
Mmoja wa mwili ukiingizwa kwenye ndege.
Miili ikiletwa tayari kupakiwa katika ndege.
Zoezi la kupakia miili likiendelea.
Ndege aina ya Boeing C-17 iliyobeba miili ikijiandaa kuondoka Eindhoven kuelekea eneo lililoandaliwa kupokea miili hiyo.
NDEGE
zilizobeba miili ya watu waliopoteza maisha katika ajali ya ndege ya
Malaysia MH17 zimeondoka kutoka Ukraine kuelekea nchini Uholanzi kwa
ajili ya kutambuliwa.
Katika ajali hiyo iliyotokea Julai 17 mwaka huu, jumla ya watu 298 walipoteza maisha huku 193 wakiwa raia wa Uholanzi.
Maofisa
wa Uholanzi wanadai kupokea jumla ya miili 200 kutoka kwa wapiganaji
wanaoiunga mkono Urusi japo wapiganaji hao wanadai kupakia miili
iliyokamilika 282 na viungo vya miili 16 katika treni iliyopeleka miili
hiyo eneo lililo chini ya serikali ya Ukraine huko Kharkiv.
0 comments:
Post a Comment