UONGOZI WA KAMPUNI YA RELI TANZANIA -TRL UNAWATAARIFU WAKAZI WA JIJI NA WANACHI KWA JUMLA KUSITISHWA KWA HUDUMA YA TRENI YA JIJI HAPO KESHO JUMAMOSI JULAI 19, 2014, ILI KUPISHA UKARABATI WA MIUNDO MBINU YA RELI KATI YA DAR STESHENI HADI UBUNGO MAZIWA ITAKAYOFANYIKA KWA SIKU ZA JUMAMOSI NA JUMAPILI.
HATA HIVYO HUDUMA HIYO ITAREJEA TENA KAMA KAWAIDA KUANZIA JUMATATU JULAI 21, 2014 . ATAKAYESIKIA AU KUSOMA TAARIFA HII AMUARIFU NA MWENZIYE.
UONGOZI WA TRL UNASIKITIKA KWA USUMBUFU UTAKAOJITOKEZA.
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL
Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu,
Dar es Salaam,
Julai 18, 2014
0 comments:
Post a Comment