WAZIRI
WA UJENZI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI KATIKATI AKIKATA UTEPE KUASHIRIA
UZINDUZI WA KIVUKO KIPYA CHA MV MARA KITAKACHOTOA HUDUMA KATI YA MAENEO
YA IRAMBA BUNDA NA MAJITA MUSOMA VIJIJINI. KUTOKA KUSHOTO NI KAIMU MKUU
WA MKOA WA MARA MHANDISI EVARIST NDIKILO AKIFATIWA NA MBUNGE WA JIMBO
LA MWIBARA ALPHAXAD KANGI LUGORA, WENGINE KUTOKA KULIA NI KATIBU MKUU WA
WIZARA YA UJENZI MHANDISHI MUSSA IYOMBE AKIFATIWA NA MBUNGE WA MUSOMA
VIJIJINI NIMROD MKONO PAMOJA NA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MARA
CHRISTOPHER SANYA.
WAZIRI
WA UJENZI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKIBONYEZA KITUFE CHA KIVUKO CHA MV
MARA KUASHIRIA KUKIZINDUA RASMI KWA AJILI YA KUANZA KUTOA HUDUMA KATI YA
MAENEO YA IRAMBA NA MAJITA KATIKA WILAYA MBILI ZA BUNDA NA MUSOMA
VIJIJINI.
WAZIRI
WA UJENZI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AAKIFURAHIA JAMBO NA MWENYEKITI WA
BODI YA TEMESA BALOZI HERBERT MRANGO HUKU MBUNGE WA MUSOMA VIJIJINI
NIMROD MKONO ALIYESSIMAMA KULIA NA MBUNGE WA MWIBARA KANGI LUGORA
WAKWAANZA KUSHOTO WAKIANGALIA.
WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKIPUNGIA WAKAZI WA MWIBARA MARA BAADA YA KUFUNGUA KIVUKO CHA MV MARA.
WADAU WAKIFATILIA TUKIO HILO
PICHA YA BOTI AMBAYO ILIKUWA IKITUMIKA AWALI KUVUSHA WATU KATI YA MAJITA NA IRAMBA KWA GHARAMA YA SHILINGI 2000/=.
KIVUKO CHA MV MARA
WAZIRI
WA UJENZI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKIPOKEA ZAWADI ZA KIMILA KUTOKA KWA
WENYEJI WA BUNDA ZA KUMTAMBUA KUWA MKAZI WA MJI HUO KWA KIMILA.
WAZIRI
WA UJENZI MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKIHUTUBIA WAKAZI WA IRAMBA
KATIKA JIMBO LA MWIBARA KABLA YA KUZINDUA KIVUKO CHA MV. MARA CHENYE
UWEZO WA KUBEBA TANI 25 YANI MAGARI MANNE NA ABIRIA 50.
WAZIRI
WA UJENZI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKIFURAHIA NA WANACHAMA WAPYA WA
CHAMA CHA MAPINDUZI CCM WALIOAMUA KUJIUNGA NA CHAMA HICHO MARA BAADA YA
WAZIRI MAGUFULI KUMALIZA KUHUTUBIA MKUTANO.
Waziri
wa Ujenzi, Dkt. John P. Magufuli amewataka wakazi wa Iramba na Majita
kutunza kivuko kipya cha MV Mara ili kiweze kuwasaidia katika kuinua
uchumi wa maeneo hayo.
Waziri
Magufuli alitoa tamko hilo jana kabla ya kuzindua kivuko hicho kipya
katika kijiji cha Iramba wilayani Bunda mkoani Mara.
“Ndugu zangu wa Iramba kitunzeni kivuko hiki kwani ni mkombozi mkubwa
katika kuwaletea maendeleo yenu pamoja na maeneo ya jirani” Alisema
Waziri Magufuli
Pia Waziri Magufuli aliwaasa wavuvi kutotega nyavu kwenye njia za kivuko
ili kiweze kudumu kwa muda mrefu kwani kwa kufanya hivyo watasababisha
injini za kivuko hicho kuharibika mapema.
Aidha
Waziri Magufuli aliwapongeza Mbunge wa Mwibara Kangi Lugora pamoja na
Mbunge wa Musoma vijijini Nimrodi Mkono kwa juhudi zao zilizochochea
kupatikana kwa kivuko hicho.
Aidha,
Dkt. Magufuli alisema kuwa kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba tani
25, yaani magari manne 4 na abiria 50, kitaokoa maisha ya wananchi wengi
ambao walikuwa wanapata adha kubwa ya usafiri kutokana na kukosa
usafiri wa uhakika ambao ulikuwa unahatarisha maisha yao.
“Nimeambiwa
hapa nauli ilikuwa Shilingi 2000/= kuvuka upande wa pili kwa kutumia
boti za watu binafsi lakini kwa kivuko hiki natangaza rasmi kuwa nauli
kwa kivuko chetu kipya ni shilingi 500/= tu, na wanafunzi waliovaa sare
watapanda bure, watoto sh.100” Alisema Waziri Magufuli.
Dkt.Magufuli aliongeza kuwa nauli za magari na mizigo zitapangwa na
Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA ambao ndio wasimamizi wa kivuko hicho.
Aidha,
Waziri Magufuli aliongeza kuwa Serikali itaendelea kuboresha
miundombinu bila kuangalia itikadi zozote za kisiasa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi wa kijiji cha Iramba,
walisema kuwa walikuwa wanapata taabu sana ya usafiri kwani ilikuwa
inawalazimu kuvuka kwa mitumbwi ambayo ilikuwa inahatarisha maisha ya
wakazi wa maeneo hayo.
0 comments:
Post a Comment