Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Nchini Tanzania,
Profesa Sifuni Mchome akiwasilisha Mada ihusuyo Urudiaji wa Vifungo
Magerezani kwa Wahalifu(Recividism) katika Mkutano wa Tatu wa Umoja wa
Taasisi za Urekebishaji(Magereza) Barani Afrika uliofanyika hivi
karibuni Maputo, Msumbiji.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania, John Casmir Minja
akichangia Mada katika Mkutano wa Tatu(03) wa Umoja wa Taasisi za
Urekebishaji(Magereza) Barani Afrika uliofanyika hivi karibuni kuanzia
July 14 - 17, 2014 Maputo, Msumbiji.
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa Tatu(03) wa Umoja wa Taasisi za
Urekebishaji(Magereza) Barani Afrika wakifuatilia Majadiliano ya Mkutano
huo uliofanyika hivi karibuni Maputo, Msumbiji(wa kwanza kulia) ni
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja(wa
kwanza kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Uganda, Dkt.
Johnson Byabashaija(mstari wa nyuma) ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi la
Magereza Nchini Tanzania wakifuatilia mjadala katika Mkutano huo wa
Kimataifa.
Maafisa na Askari Magereza wa Msumbiji wakimsikiliza Mgeni rasmi, Rais
wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji, Mhe. Dkt. Armando Guebuza(hayupo
pichani) katika ufunguzi wa Mkutano wa Tatu(03) wa Umoja wa Taasisi za
Urekebishaji(Magereza) Barani Afrika uliofanyika Maputo, Msumbiji.
Rais wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji, Mhe. Dkt. Armando Guebuza(katikati)
akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Taasisi za
Urekebishaji(Magereza) Barani Afrika pamoja na Washiriki Wengine wa
Mkutano mara baada ya kufungua rasmi Mkutano wa Tatu wa Umoja wa Taasisi
za Urekebishaji Barani Afrika, Maputo Msumbiji(wa Nne kushoto mstari wa
pili) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(wa kwanza
kushoto) ni Rais Mstaafu wa Msumbiji, Joaquim Chisasano(wa kwanza kulia)
ni Kamishna wa Magereza Nchini Zambia, Percy Chato(wa tatu kulia mstari
wa mbele) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia, Raphael
Hamunyela.Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza
0 comments:
Post a Comment