MASHINDANO ya Pepsi Kombe la Meya Jiji la Mwanza
2014 kuanza kutimua vumbi Agosti 2 mwaka huu na Bingwa kujinyakulia mzigo wa kitita cha
Sh. Milioni sita, wilayani Nyamagana mkoani Mwanza.
Mwaka huu jumla ya timu 22 zitashiriki ambapo timu 12 zitatoka katika Kata
12 za Jimbo la Nyamagana na timu
nyingine 12 zitatoka katika vikundi na asasi mbalimbali za kijamii zilizopo
jimboni humo.
Balozi wa Habari wa Pepsi Kombe la Meya 2014, Albert G. Sengo akizungumza na wanahabari kuhusiana na taratibu za michuano hiyo zitakavyokuwa. |
Mashindano
haya yanafanyika kwa mwaka wa pili mfululizo chini ya udhamini wa
Kampuni ya SBC inayotengeneza vinywaji baridi kupitia kinywaji chake cha
Pepsi ambapo kwa mwaka huu yameboresha zaidi kwa kuhakikisha vifaa
vitakavyotolewa vinakuwa na ubora ikiwa pia na ongezeko la ukubwa wa
zawadi za washindi. “Lengo
kubwa la mashindano haya ni kuwezesha vikundi vya vijana wajasiriamali,
kuleta umoja, hamasa, kuendeleza vipaji vya soka, mshikamano na
burudani, lakini pia kuviwezesha mitaji ya kuendesha shughuli zao
kupitia mashindano ya soka ili kuvijengea uwezo,”
Zawadi
kwa washindi mwaka huu zimeongezeka ambapo bingwa atajinyakulia Bajaji
ya kisasa ya kubeba mizigo na watu wanne yenye thamani ya milioni 4.5 na
fedha tasilimu milioni 1.5 (jumla milioni sita), mshindi wa pili
milioni 2, mshindi wa tatu milioni 1 huku mfugaji bora, timu yenye
nidhamu na mwamuzi bora kuzawadiwa Sh. Laki mbili.
Awali
meneja wa kamati ya mashindano ya Pepsi Kombe la Meya 2014, Bitegeko
(wa kwanza kulia) alieleza kwamba timu zitakazoshiriki michuano hiyo
zimegawanywa katika makundi manne ambapo kundi A litakuwa na timu sita,
kundi B, C na D kila moja litakuwa na timu tano, mzunguko wa kwanza
utachezwa kwa mtindo wa ligi katika makundi na hatua ya robo fainal timu
zitacheza kwa mtoano hadi kupata timu mbili zitakazo cheza fainali ili
kumpata bingwa kwa mwaka 2014.
“Viwanja
vitakavyotumika katika michuano ya Kombe hilo ni Nyamagana, Nyegezi
Kona, Mabatine Polisi, Buhongwa, Igoma Mnadani na Mkolani na waamuzi
watakaochezesha mashindano hayo ni vijana wanafunzi kutoka katika Kituo
cha Michezo cha Alliance cha jijini hapa,” alieleza.
Moja
kati ya kanuni za mashindano ya Pepsi Kombe la Meya 2014, zinaeleza
kuwa timu itaruhusiwa kusajili wachezaji wasiozidi 25 kwa fomu
zilizotolewa, Wachezaji wa Ligi kuu ya Vodacom na Ligi Daraja la Kwanza
hawataruhusiwa katika mashindano haya.
Ni kosa kumchezesha mchezaji ambaye hajasajiliwa. Timu itakayo mchezesha mchezaji ambaye hayupo kwenye orodha ya wachezaji waliosajiliwa itapoteza michezo yote ambayo mchezaji huyo aliichezea.
Mchezaji hatoruhusiwa kusajiliwa kwenye timu zaidi ya moja. Iwapo mchezaji huyo akibainika ataondolewa kwenye mashindano na timu hiyo haitoruhusiwa kuweka mchezaji mwingine mbadala, timu itanyang'anywa pointi kwa michezo aliyo cheza mchezaji huyo.
Pepsi
Kombe la Meya 2014 itafuata sheria zote 17 za soka. Kubadili wachezaji
(substitution) mwisho watano. Mchezaji akipewa kadi nyekundu
hatoruhusiwa kucheza mechi moja inayofuata.
Mashindano yatasimamiwa na Kamati ya Mashindano ambayo inamamlaka ya kuifuta katika mashindano timu yoyote ambayo wachezaji wake watakuwa ni chanzo cha vurugu katika mashindano.
"Matayarisho yako safi kwa asilimia 100" says Nicolas Coetz. |
* Kila
timu ina wajibu wa kutunza nidhamu ya wachezaji na washabiki wake ndani na nje ya
mchezo.
* Maamuzi
ya refa yatakuwa ya mwisho katika mchezo.
* Ni
kapteni wa timu pekee ndiye anaruhusiwa kupeleka malalamiko kwa muamuzi ndani ya
mchezo.
* Timu
itakayogomea mchezo itakuwa imepoteza mchezo husika na Kamati ya mashindano itakaa
kuijadili timu hiyo kwa adhabu nyingine kama itaona inafaa.
* Mchezo
utaanza saa 10:30 jioni. Kila timu inatakiwa kufika uwanjani saa moja kabla ya mchezo
kuanza.
* Viongozi
wa timu watatakiwa kusaini kwenye nakala ya kanuni itakayobaki kwa muandaaji wa
mashindano ikiwa ni ishara ya kuwa wamezielewa na wataziwasilisha vyema kwenye timu
zao ili kuboresha mchezo.
Kwa
upande wake Meneja Masoko wa Kampuni ya SBC Sharif Taki alisema kwamba
tangu kuanza kudhamini mashindano hayo kwa sasa yamepanua wigo na kuwa
na sula ya kitaifa na tayari yamefanyika Morogoro, Mbeya, Dodoma na
wanategemea Arusha kufanyika baada ya kumalizika haya ya Jiji la Mwanza
huku pia wakianda ya kukutanisha timu za bingwa kwenye Majiji ya Mwanza,
Tanga, Arusha, Mbeya na Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment