Mkurugenzi
Mtendaji wa Azania Bank Limited,Bwa.Charles Singili akizungumza mbele
ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kupata ftari ya pamoja
iliyoandaliwa na Benki ya Azania,mwishoni mwa wiki kwenye moja ya ukumbi
uliopo ndani ya jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Bwa.Singili
alisema kuwa Benki ya Azania ni kama sehemu ya jamii, watajitahidi
kutoa msaada kwa jamii katika Nyanja za elimu,afya na kusaidia yatima
kila nafasi na uwezo unaporuhusu.Benki ya Azania pia iliwaalika Watoto
waishio katika mazingira magumu kutoka kituo cha Mitindo House
Foundation.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa benki ya Azania imekuwa sasa na kufikia matawi 15 ikilinganishwa na matawi matatu waliyokuwa nayo mwaka 2007,alisema kwa Dar es salaam pekee wana jumla ya matawi 05. ''tunawashukuru wateja wetu,kwani bila uwepo wao tuingefika hapa,tunapenda kuwahakikishia kuwa tunaendelea na juhudi zetu za nia ya kutaka kuwa na teknolojia ilio sahihi'',alisema MKurugenzi huyo.

Mtendaji wa Azania Bank Limited,Bwa.Charles Singili (kwanza kulia)
akiwa na baadhi ya wageni wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbi humo
pamoja na waalikwa wengine kupata ftari ya pamoja iliyoandaliwa na benki
hiyo,mwishoni mwa wiki kwenye moja ya ukumbi uliopo ndani ya jengo la
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),jijini Dar.
Afisa
mkuu maendeleo ya biashara kutoka benki ya Azania,Bwa.Othman Jibrea
akiwakaribisha wageni waalikwa mbalimbali waliofika kupata ftari ya
pamoja iliyoandaliwa na Benki ya hiyo,mwishoni mwa wiki kwenye moja ya
ukumbi uliopo ndani ya jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA),jijini Dar Es Salaam.
Watoto
waishio katika mazingira magumu kutoka kituo cha Mitindo House
Foundation wakipata futari ya pamoja iliyoandaliwa na Benki ya Azania
sambamba na wadau wengine wa benki hiyo,hafla hiyo ilifanyika mwishoni
mwa wiki kwenye moja ya ukumbi uliopo ndani ya jengo la Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA),jijini Dar Es Salaam.
Sheikh
Abdulrahman Ali Issa akitoa shukurani za dhati (kwa niaba ya sheikh wa
Mkoa Dar Es Salaam),kwa uongozi wa benki ya Azania kwa kutoa mwaliko wa
futari kwa wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo watoto yatima kutoka
kituo cha Mitindo House Foundation..
Mkurugenzi
Mtendaji wa Azania Bank Limited,Bwa.Charles Singili (kwanza kulia)
akiwa na baadhi ya wageni wakipakua ftari ya pamoja iliyoandaliwa na
benki hiyo,mwishoni mwa wiki kwenye moja ya ukumbi uliopo ndani ya
jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),jijini Dar.
Wageni waalikwa wa benki hiyo ya Azania wakiendelea kuchukua futari tayari kwa futuru.
Mazungumzo ya hapa na pale yalikuwepo pia .
NA ANKAL MICHUZI
0 comments:
Post a Comment