SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, June 20, 2014

Uingereza 1- 2 Uruguay

Suarez ashangilia bao lake dhidi ya Uingereza
Uruguay wameilaza Uingereza 2-1 katika mechi yao ya pili ya kundi D. Luiz Suarez ndiye amefunga mabao yote mawili ya Uruguay
Uingereza walikuwa wameshindwa mabao 2-1 na Italia katika mechi yao ya ufunguzi. Uruguay kwa upande wao


Matokeo :Uruguay wameilaza Uingereza 2-1
Uingereza sasa watafurushwa kutoka kwenye kombe la duniaBrazil 2014 iwapo wapinzani wao katika kundi hilo Costa Rica watatoka sare ama kushinda Italia katika mechi yao ya pili itakayochezwa Ijumaa.
23:51 Mechi imekamilika
23:48 Uruguay 2-1 Uingereza
23:47 Dakika 5 za ziada.
23:45 Suarez anaondoka uwanjani zikiwa zimesalia dakika mbili mechi hii ikamilike .
23:43 Uruguay 2-1 Uingereza
23:43 Luiz Suarez anaifungia Uruguay bao la pili
23:32 Uruguay 1-1 Uingereza Rooney 75''
23:31 ROOOONEY !
23:31 Uingereza wanashambulia
23:26 Welbeck anaondoka anaingia Adam Lallana
23:24 Uruguay 1-0 Uingereza 70''
23:24 Steve Gerrard anaoneshwa kadi ya njano baada ya kumwangusha Rodriguez
23:23 Nickolas Lodeiro anapumzishwa
23:20 Rooney anafanya mashambulizi lakini inakuwa bure Muslera anaupokea
23:20 Raheem Sterling anaondoka na nafasi yake inachukuliwa na Ross Barkley
23:15 Uruguay 1-0 Uingereza 60''
23:14 Ushirikiano baina ya Cavani na Luiz Suarez unawatatiza waingereza.
23:12 Kipa wa Uruguay Muslera anajeruhiwa na Muslera lakini Refarii anasema si hoja hiyo
23:10 Rooooooney anakosa nafasi nzuri akiwa amesalia na Muslera
23:09 Suarez anapiga tobwe lakini inatoka nje ni free kick.
23:04 Uingereza imenusurika kufungwa bao la pili kutokana kona ya Luiz Suarez
23:02 Luiz Suarez 37''
Luiz Suarez 37''
23:01 Uruguay bado inaongoza kwa bao moja kwa nunge.
23:00 Kipindi cha pili kimeanza bila ya mabadiliko yeyote kwa timu zote
22:45 Kipindi cha kwanza kimekamilika Uruguay ikiongoza kutokana na bao la pekee la Luiz Suarez
22:45 Uruguay 1-0 Uingereza 45''
22:43 Uingereza inatafuta bao la kusawazishakwa udi na uvumba
22:42 Kona ya tatu kwa Uingereza .
22:40 Uruguay 1-0 Uingereza
22:39 Luiz Suarez 39''
22:38 Luiz Suarez anaiweka Uruguay mbele
Uingereza 0-0 Uruguay
22 :38GOOOOOOOAL
22:37 Uingereza 0-0 Uruguay 37''
22:36 Uruguay nayo lazima ishinde iwapo inataka kuendelea mbele na dimba hili
22:36 Uingereza inatafuta alama zitakazoinusuru aibu ya kubanduliwa nje ya kombe hili baada ya kulazwa 2-1 na Italia.
22:33 Freekick kuelekea lango la Uingereza inapigwa na Suarez
22:32 Uruguay 0-0 Uingereza 32
22:31 Rooney anapokea mkwaju wa Gerrard lakini unagonga mwamba na kurudi uwanjani.
22:30 Feekick kuelekea kwenye lango la Uruguay
22:26 Uingereza inapeana Kona ya tatu kwa Uruguay
22:25 Uingereza 0-0 Uruguay 25''
22:17 Sturridge anafyatua mkwaju unaokwenda nje na inakuwa ni Kona kuelekea lango la Uruguay.
22:17 Cristian Rodríguez Uruguay anatupa nje nafasi ya kufunga bao. Golkick.
22:10 Uruguay 0-0 Uingereza
22:09 Wayne Rooney ndiye anayeipiga Freekick
22:08 Diego Godin anaoneshwa kadi ya kwanza ya Njano nje ya eneo
22:07 Suarez anamenyana na mwenzake wa Liverpool Steve Gerrard
Mashabiki wa Uingereza walivumilia timu yao iliposhindwa katika mechi ya kwanza
22:06 Freekick kuelekea upande wa Uruguay,,inadenguliwa
22:03 Luiz Suarez ndiye anayeipiga na inaondoshwa na kuwa kona ya pili
22:02 Kona ya kwanza ya mechi hii kuelekea lango la Uingereza
22:01 Kiti cha Tabarez kocha wa Uruguay kina misumari
22:01 Uingereza ikiongozwa na Dan Sturridge wanafanya mashambulizi ya mapema
22:00 Mechi imeanza
22:00 Uruguay inatafuta pointi ya kwanza katika kombe la dunia inapokabiliana na Uingereza.
21:58 Luiz Suarez anacheza katika mechi hii ambayo lazima Uruguay ishinde ilikufufua kampeini yake ya Kombe la Dunia
21:57 Hii ni mechi ya 23 ya kombe la dunia la Brazil 2014
Uruguay inatafuta pointi ya kwanza katika kombe la dunia inapokabiliana na Uingereza.Timu zote zilishindwa katika mechi zao za ufunguzi.
21:56 Timu zote zilishindwa katika mechi zao za ufunguzi.

21:55 Uruguay inakabiliana na Uingereza katika mechi ya pili.