SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, June 20, 2014

Kijana akutwa amekufa kwenye kituo cha mabasi yaendayo kasi jijini Dar

Mwili wa marehemu ....
Kijana mmoja wa kiume aliyedaiwa kuwa ni mfanyabiashara ndogondogo amekutwa amefariki katika kituo cha mabasi yaendayo kasi Manzese, jijini Dar, leo asubuhi.

Inasemekana vijana wengi huwa wana tabia ya kulala ndani ya vituo hivyo kwa hiyo watu iliwachukua muda mrefu kubaini kama amefariki.

Kwa mujibu wa mtendaji wa serikali wa Kata ya Midizini-Manzese, Penford Kizo, wa eneo hilo na mashuhuda wengine, kifo cha kijana huyo hakijafahamika kimesababishwa na nini.

Mtendaji wa eneo hilo na baadhi ya Wasamaria wakiufunika mwili wa marehemu